Mchumba wangu amezaa na mume wa mtu!

Mchumba wangu amezaa na mume wa mtu!

Achana nae, itakuuma hapa mwanzoni but later utazoea ukimng'ang'ania ujue utakuwa umeamua kujitwisha gunia la misumari for the rest of your life.
 
Hitaji la moyo vs hitaji la mwili.uamuzi upo mikononi mwako.ila ningekuwa wewe ningeendelea na huyo binti! Hatuwezi jua ndani ya huo mwaka mmoja nini kimetokea kati yenu.then Wanawake wangapi wanalea watoto wa waume zao?
 
Wanajamvi ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini Afrika Kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.

Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.

Wadau kiufipi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu.

Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...ninyi mnaniambia nini. Shukrani hapa nimeweka kwa ufupi hasa mawazo makuu ya mkasa wenyewe.

Mchumba wako wakati huyu ni mke wa aliyezaa naye? Nafikiri ingekuwa vema kama ungesema aliyekuwa mchumba wangu. Hapo umesema kama anayesema "nimemkuta hayupo". Ni ushauri tu!
 
Wanajamvi ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini Afrika Kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.

Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.

Wadau kiufipi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu.

Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...ninyi mnaniambia nini. Shukrani hapa nimeweka kwa ufupi hasa mawazo makuu ya mkasa wenyewe.

Sijui mahusiano yenu yalikuwaje, lakini nikiwa kama mwanamke ambaye nimeshakumbwa na dhoruba nyingi ndani ya mahusiano, ni kwamba kuna vitu huwa wanaume mnakosea. Inawezekana moyoni mwako ulikuwa na malengo mazuri kuhusu mahusiano yenu lakini hayakuwa wazi, namaanisha inawezekana haukuwa wazi nini kinafuata baada ya kuwa wazazi wenu wanafahamu mahusiano yenu, na kwa muda gani (committments). Wanawake wengi (na mimi nikiwemo) hatuwezi kuvumilia dilema kwenye mahusiano. Maisha ya kusadikika, hatima yangu kwako iko kinadhalia zaidi kuliko kivitendo. Hali kama hii ikiwepo ni rahisi sana kwa mwanamke kujikuta anatoka nje ya mstari, akiamini huko atapata kile anachokiitaji.

Wakati uko south Africa, mawasiliano yenu yalikuwaje? bado ulikuwa unamuonesha kuwa nafasi yake iko palepale. Siku hizi mawasiliano yamerahisishwa sana, sitegemei ukae SA miezi bila hata kuwasiliana na mwenzio. MAWASILIANO MAWASILIANO MAWASILIANO, ukikaa kimya siwezi kujua unawaza nini, inawezekana umeshaanza maisha mengine huko uliko.
Sio kwamba najaribu kumtetea mchumba wako, la hasha nilichokuwa najaribu kuonyesha ni loop hole gani amabazo usipozizingatia, zinaweza zikasababisha haya yaliyokukuta especially mnapokuwa mbali (long distance relationships)
 
Kiukweli hali kama hiyo si ya uamuzi wa moja kwa moja.

1) Vipi kama msichana anakupenda kweli na aliteleza siku moja tu ndo akapata hiyo mimba? Je angeteleza na asipate mimba usingemuoa? Is it a question of cheating or is it the pregnancy? Have u ever cheated on her?

2) Pia inawezekana msichana hajielewi anachotaka maishani, labda kafall kwa aliyempa mimba na jamaa anadalili za kusepa. Labda msichana yuko sorry kwa sababu anaafuta wa kumbebesha zigo la kulea mimba na mtoto! Unaweza ukamuoa na maisha yake yakiwa freshi akakucheat tena!

Kwa mimi namuona ana matatizo yake kwa sababu kama mwema sana, kwanini alisubiri hadi uone mimba ndo aombe msamaha?
 
Sijui mahusiano yenu yalikuwaje, lakini nikiwa kama mwanamke ambaye nimeshakumbwa na dhoruba nyingi ndani ya mahusiano, ni kwamba kuna vitu huwa wanaume mnakosea. Inawezekana moyoni mwako ulikuwa na malengo mazuri kuhusu mahusiano yenu lakini hayakuwa wazi, namaanisha inawezekana haukuwa wazi nini kinafuata baada ya kuwa wazazi wenu wanafahamu mahusiano yenu, na kwa muda gani (committments). Wanawake wengi (na mimi nikiwemo) hatuwezi kuvumilia dilema kwenye mahusiano. Maisha ya kusadikika, hatima yangu kwako iko kinadhalia zaidi kuliko kivitendo. Hali kama hii ikiwepo ni rahisi sana kwa mwanamke kujikuta anatoka nje ya mstari, akiamini huko atapata kile anachokiitaji.

Wakati uko south Africa, mawasiliano yenu yalikuwaje? bado ulikuwa unamuonesha kuwa nafasi yake iko palepale. Siku hizi mawasiliano yamerahisishwa sana, sitegemei ukae SA miezi bila hata kuwasiliana na mwenzio. MAWASILIANO MAWASILIANO MAWASILIANO, ukikaa kimya siwezi kujua unawaza nini, inawezekana umeshaanza maisha mengine huko uliko.
Sio kwamba najaribu kumtetea mchumba wako, la hasha nilichokuwa najaribu kuonyesha ni loop hole gani amabazo usipozizingatia, zinaweza zikasababisha haya yaliyokukuta especially mnapokuwa mbali (long distance relationships)

Madame uko sahihi sana kwenye suala la commitments!
Ila sasa mi nimeshindwa kuelewa msichana ameshachumbiwa right, huko kwa MUME WA MTU alikuwa anategemea commitments gani tena?

Angekuwa ni kijana asiyeoa ningeelewa na kumtetea kwa vile wanaume hawatabiriki unaeza kukataa kuolewa hapa alaf yule unaemsubiria naye akaingia mitini.
Huyu ni kicheche tuu. Na pengine asingepata mimba angeolewa na huyu jamaa lakini mume wa mtu angekuwa anajiservia pia!
 
Mh sa hapo unataka ushauriwe nini...na yeye kachagua kuwa kimada mwache alione jiji vizuri..jumapili jamaa yuko busy na familia yeye anavizia ofisini..maisha mafupi mbona mabinti wako wengi.
 
Wanajamvi ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini Afrika Kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.

Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.

Wadau kiufipi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu.

Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...ninyi mnaniambia nini. Shukrani hapa nimeweka kwa ufupi hasa mawazo makuu ya mkasa wenyewe.

Hivi Mkuu huyu mchumba wako ni ana ujauzito wa mme wa mtu au amezaa na mume wa mtu?
 
Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.
Yani pamoja na story ndeeeefu naona we ndo unaleta movie ya kibongo sasa.
 
tunaweza kukushauri kumbe huyo dada ndo anakuweka mjini.ooh majanga mbona majanga
 
Check it out,kama alihiari mwenyewe,manake anampenda,ni ukwel usiopingika huwez kupenda watu wawili kwa usawa na kwa wakati mmoja.
Anakuzingua achana nae songa mbele
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom