Mchumba wangu amezaa na mume wa mtu!

Mchumba wangu amezaa na mume wa mtu!

Pole sana mkuu. Ningekuwa wewe ningevunja tu huo uchumba, mi kwangu kosa kubwa kabisa la kuvunja uhusiano ni kucheat. Kama ameshindwa kuvumilia huku mwanzoni kwenye ndoa ndo ataweza. Ila mwamuzi ni wewe.
Shukrani Mwasi kwa neno la kunipa mwanga!
 
Dah. Pole sana kaka hayo ndiyo majaribu ya dunia hii, na hicho ndicho kipimo cha mwanamke kama anauvumilivu na upendo wa kweli.
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1379015439514.jpg
    uploadfromtaptalk1379015439514.jpg
    32.9 KB · Views: 157
Pole sana Mkuu kwa yaliyokukuta. Wewe ndio mwenye maamuzi ya mwisho kama unaweza kumsamehe au la ila washirikishe na Wazazi wako pia kabla ya kufanya uamuzi wako. Pole sana.
Shukrani kwa wazo Bak...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
pole mdau cha kufanya wewe anza maisha mapya u deserve more than that na sio drama za kipuuzi. huyo dada sio mwaminifu na hajalu afya yake. wakati wanafanya hlo tendo tena naaamini sio chini ya mara 10 alikuwa hajui huyo mwanaume ni married man, kinga hakuzijua. wewe ni mwanaume fanya maamuzi ambayo hutafedheheka mbele ya jamii inayokuzunguka. wazazi ni waelewa waeleze ukweli wote tena wao ndio watakushauri vizuri usiogope kuongea nao.
pole kwa kupenda mtu asiye na mapenzi kwako.
 
wanajamvi ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini afrika kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.

Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.

Wadau kiufipi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu.

Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...ninyi mnaniambia nini. Shukrani hapa nimeweka kwa ufupi hasa mawazo makuu ya mkasa wenyewe.

bora kuvunja uchumba kuliko kuvunja ndoa jamaa amka......!!!
 
pole mdau cha kufanya wewe anza maisha mapya u deserve more than that na sio drama za kipuuzi. huyo dada sio mwaminifu na hajalu afya yake. wakati wanafanya hlo tendo tena naaamini sio chini ya mara 10 alikuwa hajui huyo mwanaume ni married man, kinga hakuzijua. wewe ni mwanaume fanya maamuzi ambayo hutafedheheka mbele ya jamii inayokuzunguka. wazazi ni waelewa waeleze ukweli wote tena wao ndio watakushauri vizuri usiogope kuongea nao.
pole kwa kupenda mtu asiye na mapenzi kwako.
Shukrani ndugu kwa mawazo na ushauri!
 
oa then aje zaa na baba ako mzazi/boss wakondio utajiunza na msongo wa mawazo kukuishia
 
Wanajamvi ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini Afrika Kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.

Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.

Wadau kiufipi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu.

Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...ninyi mnaniambia nini. Shukrani hapa nimeweka kwa ufupi hasa mawazo makuu ya mkasa wenyewe.

Je wewe south hujagonga mzigo????mwanamke kuwa na mtoto mmoja ,wawili n.k sio ishun kama unampenda unamuona na maisha yanaendelea. Na hakika hatarudia tena.unapaswa kufahamu kuwa wanawake huwa hawawezi kuvumilia muda mrefu sana
 
Ok inaelimisha hii!
 
Mambo mengine yanatokea ili kuepusha baadhi ya shari mbeleni japo yanaumiza sana. Hapo cha kufanya ni kumshukuru Mungu kwa kukuonyesha picha halisi ya mchumba wako, japo inauma lakini mugnu amekusaidia.Yawezekana ungekua nchini ungebambikiziwa hiyo mimba bila kujua na ungelea mtoto ambae siyo wa kwako, hapo cha kufanya ni kufungua ukurasa mpya.
 
Mhhh hebu tuache masihara humu ndani,nileee mimba ya mwanaume mwenzangu,me always sina tatizo hata kidogo endapo namkuta mwanamke ana mtoto tayari huwa sina shida kabisaaAa ila sio kama mdau anavyosema kwamba alikuwa na mchumba wake then mwanamke akapata mimba never ever piga chini acha upuuzi hata kama ulimpenda wanawake wapo wengi sana waliotulia....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
shukrani kwa ushauri wako mzurimie ila basi yote katika maisha hupangwa na Mwenyezi Mungu...maana naona kwako wewe kila kitu ni kwa ujanja na uwezo wako...sidhani sana ila basi na kwa hili nazidi kujifunza jinsi wanadamu tulivyo hususan katika swala zima la mahusiano ya kimapenzi.
 
Wanajamvi ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini Afrika Kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.

Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.

Wadau kiufipi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu.

Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...ninyi mnaniambia nini. Shukrani hapa nimeweka kwa ufupi hasa mawazo makuu ya mkasa wenyewe.

Mkuu mi ni babu kikongwe. kama huyu mrembo ni mchumbako kwa maana halisi ya uchumba na akafanya hayo nakuşhauri achana naye kwa amani.

İla kama ni kagelofrendi, tumia akili ya kuzaliwa na za mbayuwayu uufuate moyo wako. Ni wachache sana waliioa walio wabikiri. Mimba ni utambulisho tu kuwa binti ni mzinzi asiyetumia kinga.

Kama anakubali kupata mimba ya mme wa mtu atakubali kupata mimba ya yoyote atakayelala nae. Hata beberu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom