Mchumba niliyempata ni mwiko kwetu msaada jamani

Mchumba niliyempata ni mwiko kwetu msaada jamani

Alvin Slain

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
6,375
Reaction score
3,668
Habar,mchumba wangu niliyempata kwetu ni mwiko,kuna mmama aliwah kuolewa kwetu,hivyo alisema ni marufuku ndgu yake,kuolewa kwetu,
Hapa Nilipo naumia sana, Sababu ya huu Mwiko,Uliowekwa Miaka 50)iliyopita, Sababi kuu iliyotilewa na huyo mama, Ni kuuchwa kijijini huku mme wake akioa mke mwingine na kuishi nae Mjini, Kitendo hicho kilimuumiza huyo Mama sana,Bahati mbaya hakubahatika kua na mtoto, Siku za kifo chake akawa anaugua Kansa, Lakini Bwana wake hakumsaidia chochte, Akafikia Kusema.
Katika Nyumba hii.
Ni marufuku ndugu yangu ama Ukoo wangu kuolewa huku,Na hii alisema saa ya Mwisho kabisa ya kifo chake.
Leo hii mimi nimempata nimempenda binti,Katika Ukoo ule na sitarajii kumuoa mwingine, Ndugu wanajamvi nisaidien
 
Ndugu yake asiolewe tena kwetu endapo itatokea bas atapata matatizo
 
Ina maana kuwa huyo mama aliolewa kwenu aliteseka sana kiasi kwamba alilaani kuwa hakuna ndugu yake mwingine ataolewa kwa ukoo wenu. Haya mambo huwa yapo sana kwa baadhi ya koo ila ni mambo ya zamani sana.

Ninakumbuka wakati ninakua haya mambo yalikuwa katika koo Fulani na wanasema kabisa kuwa ni 'mwiko kuoa au kuolewa katika ukoo huo". Ilitokea dada mmoja alikuwa mzuri na mnyoofu sana. Akawa alipata mchumba kutoka katika ukoo ambao ulikuwa ni mwiko kuo au kuolewa kule. Ndugu wa pande zote walipuuzia mwiko ule na dada aliolewa. Baada ya muda alipata mimba mbili, ya kwanza mtoto alikufa, ya pili ilitoka na mwishowe alifariki. Mume yule alimpenda sana mke wake, alililia sana, alimzika kwa uchungu, nakumbuka alimvalisha ile nguo ya ndoa na kila wakati alikuwa anaibusu maiti ya mke wake. Mwishowe yule mume alikaa muda mrefu sana bila kuoa, alibeba sana mke wake moyoni ila sijaelewa siku hizi kama ameoa.

Kwa hiyo ndugu yangu kuna mambo mengine huwa yapo ila kwa neema ya Mungu ninaamini kuna maombi ya kuvunja laana ila sijajua how powerful they are.

Pole sana.
 
Habar,mchumba wangu niliyempata kwetu ni mwiko,kuna mmama aliwah kuolewa kwetu,hivyo alisema ni marufuku ndgu yake,kuole

Labda utueleze kwa kirefu mkuu, maana inakuwa ngumu kwetu kuandika chochote kwa kina...
 
Hizi mila niliziona ukuryani hayo ni maneno tu kama ukiamini yatakuathiri lkn usipoyaamini hakuna kitakachotokea jichulie mume/mke umpendae faster.
 
Ina maana kuwa huyo mama aliolewa kwenu aliteseka sana kiasi kwamba alilaani kuwa hakuna ndugu yake mwingine ataolewa kwa ukoo wenu. Haya mambo huwa yapo sana kwa baadhi ya koo ila ni mambo ya zamani sana.

Ninakumbuka wakati ninakua haya mambo yalikuwa katika koo Fulani na wanasema kabisa kuwa ni 'mwiko kuoa au kuolewa katika ukoo huo". Ilitokea dada mmoja alikuwa mzuri na mnyoofu sana. Akawa alipata mchumba kutoka katika ukoo ambao ulikuwa ni mwiko kuo au kuolewa kule. Ndugu wa pande zote walipuuzia mwiko ule na dada aliolewa. Baada ya muda alipata mimba mbili, ya kwanza mtoto alikufa, ya pili ilitoka na mwishowe alifariki. Mume yule alimpenda sana mke wake, alililia sana, alimzika kwa uchungu, nakumbuka alimvalisha ile nguo ya ndoa na kila wakati alikuwa anaibusu maiti ya mke wake. Mwishowe yule mume alikaa muda mrefu sana bila kuoa, alibeba sana mke wake moyoni ila sijaelewa siku hizi kama ameoa.

Kwa hiyo ndugu yangu kuna mambo mengine huwa yapo ila kwa neema ya Mungu ninaamini kuna maombi ya kuvunja laana ila sijajua how powerful they are.

Pole sana.

Ni kwa namna gani nitaivunja hii mwiko
 
Mi nimeona uvivu kusoma bana,kaeni na hayo mamwiko yenu labda mkitaka niwaelekeze yanapouzwa yale makubwa kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom