GE2025 Mchinjita: Raia kuokotwa kwenye mabasi mchana kisha wakafa, halafu Serikali iseme ni Wasiojulikana, hiyo ni Serikali au Takataka?

GE2025 Mchinjita: Raia kuokotwa kwenye mabasi mchana kisha wakafa, halafu Serikali iseme ni Wasiojulikana, hiyo ni Serikali au Takataka?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Walio muua mzee Kibao ndio wenye lugha ya kistaarabu?
Ama unataka kusema kuua watu mchana ni jambo la kistaarabu?
Sio wastaarabu ni wauwaji na hawastahili kuwa barabarani

Lakini e cant tukana everyone

But again, you cant demean everyone
 
Bado watu wa Mama Samia hawajamuita kumuhoji? kisha tusubiri upelelezi ukamilike miezi 17.

Hizi Lugha wanatumia hadharani, ni dalili ya watu KUCHOKA na kuwa tayari kwa Lolote.

Samia amekuwa predictable sana, watu sasa wameshajua kuwa nikifanya hivi nitakamatwa, na wapo TAYARI.

Hii ni ishara ya Hatari kubwa sana hapo mbeleni endapo hali ikiendelea hivi.

Ewe sikio la kufa, tafadhali zibuka na usikie hii dawa.
Chura hachemshiwi maji ya kuoga
 
Alafu anasema kifo ni kifo tuu kana kwamba yeye ndo mungu wetu.

Mungu huwajibu wanyonge kwa wakati. Roho za ndugu zetu tulizihitaji sanaa☹️☹️
 
.kuuwawa na maiti yake kutobolewa macho haliwezi kuwa jambo dogo kwa chama cha siasa.
Usipunguze makali ya ukatili wa wauaji wa mjumbe wa Kamati Kuu.

Hatujui kama maiti ilitobolewa macho au mtu hai alitobolewa macho kabla hajauliwa.

Tofauti kama hizi, umakini katika kung'amua tofauti kama hizo ndo zinafanya wenzetu wana solve ma cold case crimes.

Mswahili akikuta maiti na kamba shingoni ana assume kwamba ilianza kamba kikaja kifo. Kajinyonga! Wivu wa mapenzi! Kumbe ni kifo halafu maiti ikavalishwa kamba gheresha!

Haiyumkini Mzee alitobolewa macho na bisibisi akiwa hai, akamwagiwa tindikali anasikia, akapigwa tofa la kichwa.
 
Lugha yake sio ya kistaarabu
Na shida ya Tz ndio hii. Mtu anapotea watu wanagadhibika kwa hasira wanaongea kwa uchungu, aliyeuwawa uchunguzi haufanyiki na wala kwao hauwakeli ila kinachowakela ni maneno tu ya watu waliopoteza mtu wao . Kazi ipo sana.
 
Back
Top Bottom