Mchezo wa draft

Mchezo wa draft

Mimi ni nomaa kwa mchezo wa draft kama kuna mtaalamu mwingine aombe mechi na mm nina michezo 5 ya hatari
 
FB_IMG_15161283812348550.jpg
 
Draft ni mchezo wa akili tu. Kuna formula (copy)nyingi tu. "Mguu wa jini, kilosa, five ball, kingi fala, na mingine. Mtu akikuwekea copy ya fiveball tayari yeye ana sare wewe utafute. Mguu wa jini ukiuingia hutoki. Kilosa huu mimi ndio naukubali, ni full msuli. Ukiuangalia unaona kila mtu ana nafasi ya kushinda. Ila mara nyingi aliyeanxa kucheza anashinda.

Hawa ndio mabingwa wa Tanzania.

1. Mangwelele. Huyu anapatikana buguruni.
2. Juma mchafu huyu hana kijiwe maalumu. Yeye kacheza draft dsm nzima kila kijiwe.
3. Ronaldo huyu yupo sinza nadhani palestina. Ni sheeder.
4. Godziller huyu maskani yake ifakara. Ila yeye anatembea mikoani. Hii ni kazi yake na inamwingizia kipato.

Note

Ili ijue draft ukubali mambo mawili.
1. Uwe mchafu kwa maana unashinda vijiwe vya draft huna muda wa kufua na kuoga.
2. Ukonde. Maana huna muda wa kula. Muda wooote unagonga kete tu.

Ref. Juma mchafu niliyemtaja hapo juu, jina lake ni juma. mchafu ni nick name yake. Na ni kweli ni mchafu. Hafui wala haogi.
Juma mchafu amefariki aisee...
R.I.P.
 
Hao wote mliowasema hawajui kitu, kuna kichwa kinaitwa Msundafilo ni hatari tupu, kete tatu ashakumaliza
 
drafti ni kujua copy tu. kuna namna saba za kuanza game na zote zina majina. ni namna mbili tu unaweza kushinda kama unacheza na mafundi. kuanza na kete ya kati wanaita oldfaithful na kuanza na kete ya kwenye kona wanaita double corner. namna zingine zote ukikutana na anayejua copy atakukimbiza sana. nilijifunza hizi copy na counter zake hata miezi sita siku hizi napiga drafti kila mtu anashangaa. zamani nilikuwa naendaenda bila copy nilikuwa napigwa sana japo ilinisaidia uzoefu ikitokea mtu ametoka nje ya copy. mchezo poa sana huu.
 
Unapocheza draft zingatia hesabu ya steps (hatua), yaani kabla haujasukuma kete jiulize kuwa nikisukuma hapa yeye atacheza vipi kuhusu hiyo kete? UNAWEZA KUWA UMEPUNJWA KETE (Mfano wewe una kete 4 yeye 5 au 6) HALAFU BADO UKAMFUNGA AU DROO
 
Niliowahi kucheza nao, wanakijua kiwango changu.
Ni mchezo mzuri ambao inabidi ubadilishe mbinu kwa kadri ya mpinzani wako anavyocheza.
Kwa sehemu kubwa,unahitaji kulinda na kushambulia kwa akili kubwa sana.
 
Njia rahisi ya kushinda huu mchezo unaenda mbele na kete tatu tatu. Lakini hivi juzi nilikutana na jamaa alikua na mchezo wake unaitwa ebola. Alinipiga nne firster mpaka nimejiuliza. Ni mchezo mzuri
Ni mchezo mzuri sana
 
Nchi nyingi wanacheza draft la kwenda mbele na nyuma, lakini kwa Tanzania yapo ya aina mbili, kuna hilo la mbele na nyuma na kuna la mbele tu

We ni mtaalamu wa lipi?
Binafsi yote nacheza...lile la two way linaitwa French kwa kuwa limeibuliwa Ufaransa.
 
Back
Top Bottom