Mchezo wa draft

Mchezo wa draft

unapeleka kete tatu za mstari mkuu (ikweta)...then unarudia mbili mkono wa kulia .....ukimaliza kabla hajaanza mashambulizi unaweza ukaanza wewe na kete mbele kati ya tatu za ikweta .....enjoy ....
Huu mtindo unacheza peke yako???kete tatu ni michezo sits tayari ukiongeza miwili ni 8 mpinzani hachezi???
 
Huu mtindo unacheza peke yako???kete tatu ni michezo sits tayari ukiongeza miwili ni 8 mpinzani hachezi???
Umehesabu vibaya 3+2=5....halafu kumbuka kwa hizo kete kama anatumia mfumo wa pembeni ni chache sana kuna wakati mnaweza sukuma kete hadi inafika wakati kila kete unayosukuma unapigwa double au triple ...jitahidi kufanya mazoezi na mifumo tofauti tofauti. ...
 
Ebana umenikumbusha mbali sana, nilikua nalicheza sana mchezo wa draft, mpaka sasa nacheza. enzi hizo miaka ya 1998 mpaka 2003. Mgeni akija ambae anawasumbua kijiwe chetu lazima nije kuitwa nyumbani nikaokoe jahazi. Ni mchezo mtamu sana.
 
ni mchezo mzuri sana na ninaupenda sana kuweza kuwa na kiwango cha kati unahitaji practice zaidi nikiwa na maana anza kucheza na wale unaolingana nao kiwango ambapo itakuchukua hata mwaka kuimprove baada ya hapo tafuta kijiwe kingine wanaokuzidi uwezo upambane nao nadhani itasaidia sana kujua zaidi.
Nb. kumbuka huu mchezo unahitaji kufanya mazoezi zaidi ya kuucheza kuliko kuelekezwa kinadharia
Mkumbushe ajitahid kucontrol hasira maana anaweza rusha ngumi pindi akifungwa na mpinzani wake akiwa anatoa maneno ya kejeli
 
Silaha kubwa ni domo chafu... km sio mropokaji hauwezi kushinda.... silaha ya pili ni akili.. km akili zako km mange kimambi au gigy money hauwez ucheza huu mchezo... tatu asili usitegemee umetoka moshi uko afu uwe fundi wa draft huu sio mchezo wa ukubwani aisee....
 
Uwe na uwezo wa kuiteka akili ya mpinzani wako. uwe na uwezo wa kufikiria at least mpaka mchezo wa tatu mbele. Ukiwa na uwezo huo ninaweza kucheza na wewe lakini British. Added advantage uwe na maneno ya nyondo kufurahisha watazamaji na kumdhoofisha mpinzani wako mentally.
hapo kwenye added advantage watu wanarusha ngumi
 
Silaha kubwa ni domo chafu... km sio mropokaji hauwezi kushinda.... silaha ya pili ni akili.. km akili zako km mange kimambi au gigy money hauwez ucheza huu mchezo... tatu asili usitegemee umetoka moshi uko afu uwe fundi wa draft huu sio mchezo wa ukubwani aisee....
 
Kuna Copy inaitwa Mbuzi Kavimba inasumbua kama Ndandambi Style.. hakuna chomoa nijambe kwenye mchezo wa Drafti
 
mabingwa wa draft ukicheza nao ukawabana saana ni wezi sana wa step ni wajanja saanaa ..utashangaa tu anatoa sare..ni mchezo unahitaji umakini sana
 
mabingwa wa draft ukicheza nao ukawabana saana ni wezi sana wa step ni wajanja saanaa ..utashangaa tu anatoa sare..ni mchezo unahitaji umakini sana
Wizi upo ni mbinu ya mchezo, anajifanya kakosea kula kete anavyorudisha ndio anapokuibia umakini unahitajika sana
 
Habari zenu wana jf wote

Hv unapokuwa unacheza mchezo wa draft inafaa kuzingatia vitu gani ili uweze kuziteka vizuri kete za mwenzako
Lazima ujue michezo ifuatayo:-
1.Kichupi cha motto - huu unatakiwa uwe msafi sana kila akilete yake wewe kazi yako kuikata
2.Maua mazuri - huu unabanana nae mpaka mwisho ukija kujiachia unakuwa umefika kingi.
etc.
ukijua walau hii miwilitu lazima game mbovu mbovu zote unashinda
 
Halafu Kuna wataalamu WA force king Hao ukijisahau kidogo linaisha hapohapo!!

Utasikia tu kula huku,Mara kula huku utaona ka unapewa bure unapigwa force mwanaume yulee anachukua kingi,wakati huo huo kakata mstari dude limeisha!!!

Mchezo mmoja mtam sana ukiujua, nililichezacheza zamani siku uwezo umepungua ila Lina formula nyingi ( copy ).
 
Huu mchezo ni mtamu ila hauhitaji hasira. Kuna watu wanacheza huku wanamaneno machafu ya kuudhi kiasi kwamba unaweza ukarusha ngumi. Kijiweni kwetu kimara Golani jana watu wamepigana kisa draft
 
Silaha kubwa ni domo chafu... km sio mropokaji hauwezi kushinda.... silaha ya pili ni akili.. km akili zako km mange kimambi au gigy money hauwez ucheza huu mchezo... tatu asili usitegemee umetoka moshi uko afu uwe fundi wa draft huu sio mchezo wa ukubwani aisee....
Draft ni mchezo wa akili tu. Kuna formula (copy)nyingi tu. "Mguu wa jini, kilosa, five ball, kingi fala, na mingine. Mtu akikuwekea copy ya fiveball tayari yeye ana sare wewe utafute. Mguu wa jini ukiuingia hutoki. Kilosa huu mimi ndio naukubali, ni full msuli. Ukiuangalia unaona kila mtu ana nafasi ya kushinda. Ila mara nyingi aliyeanxa kucheza anashinda.

Hawa ndio mabingwa wa Tanzania.

1. Mangwelele. Huyu anapatikana buguruni.
2. Juma mchafu huyu hana kijiwe maalumu. Yeye kacheza draft dsm nzima kila kijiwe.
3. Ronaldo huyu yupo sinza nadhani palestina. Ni sheeder.
4. Godziller huyu maskani yake ifakara. Ila yeye anatembea mikoani. Hii ni kazi yake na inamwingizia kipato.

Note

Ili ijue draft ukubali mambo mawili.
1. Uwe mchafu kwa maana unashinda vijiwe vya draft huna muda wa kufua na kuoga.
2. Ukonde. Maana huna muda wa kula. Muda wooote unagonga kete tu.

Ref. Juma mchafu niliyemtaja hapo juu, jina lake ni juma. mchafu ni nick name yake. Na ni kweli ni mchafu. Hafui wala haogi.
 
Duuuh ni noma sana, kujua draft Kuna uhusiano gani na kuwa mchafu
 
Back
Top Bottom