Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Kuna mmbongo alikuwa jirani yetu miaka hiyo, alikwenda Urusi kusoma miaka 7. Alijaliwa kupata watoto 3 katika miaka hiyo 7. Alipomueleza mama yao kuwa ana mke nyumbani, yule mama alimumbia chukua wanao uondoke. Yule baba alimueleza mkewem akamuelewa, basi ilikua familia kumbwa mle ndani. Mama yao mmbongo aliwalea kwa upendo sana.
 
Mkuu mm nakushauri tulia kwanza mpaka utakapo maliza papers zenu then kaa nae mwambie ukweli wote koz hyo tayari ni mzazi mwenzako...baada ya hapo ndio mtajua cha kufanya bora uanze Huko kumaliza hiyo mishe kuliko kumleta huku na hata pia ukimtoroka unadhan Tanzania mbali kama mbinguni? Anaweza kuja huku kukutafuta tuu! May be kupitia Jina lako au ofisini. Cha msingi tulia Kwanza mwambie ukweli Ww Mwanaume bhana pambana kwanza ugenini Huko koz una mke tayari. Bora yy Huko kuna maisha mazur kuliko huku Tanzania usije wapa mzigo watoto wako baadae.
 
Nimelipenda hili wazo, nitalizingatia. Ila itabidi niache baadhi ya vitu vyangu ili asishitukie mapema.
Aaaaah! Utazingatiaje Mawazo tofauti!?? Nataka nikushauri mkuu, Mimi mwanaume mwenzako, na shida yako Ni yangu, Mimi mwenyewe nimedanganya kwa Mzungu, kabla sijakushauri nambie......Huyo Mkorea anajua kuwa Una Mtoto au Watoto???
 
Kama ni chai feki huulazimishwi kunywa.
Sawa lakini umetuwekea chai mezani bila sisi kujua ni chai ya samadi ya ngombe,bahati mbaya mimi nimemeza bila kujua na sasa tumbo langu linanguruma,halafu wewe unaniuliza eti sikulazimishwa,.,.,sasa huoni ni afadhali ningelazimishwa ningeshtukia lakini wewe umenitrick kitapeli ili niumwe tumbo.
 
Nimekusoma mkuu, nitachanganya na za kwangu.
 
Angekuwa ameshajifungua si tatizo.
 
kosa kubwa ulilofanya ni kumpa yeye akakate tiketi,,,wenzako huwa hawaagi,,ungeendelea kuwa nae then ungemtoroka bila kujua siku unayoondoka, ukifika Tz unawasiliana nae kumweleza ukweli. nakushauri fanya juu chini badilisha tarehe ya safari ikiwezekana weka ya siku za karibu kabla ya tarehe ya mwanzo halafu mtoroke. ukifika huku utawasiliana nae kumwambia ukweli. Lazma ujue kwamba wa korea na wa japan ndio wanawake wanaoongoza duniani kote kwa uaminifu na kuwa na mapenzi ya kweli. nakushauri usimwambie ukweli kwamba umeoa kwasasa atakufanyia kitu kibaya sana. nimeshuhudia wengi wamefanyiwa mabaya. jitahidi toroka halaf umwambie ukweli ukiwa Tz
 
Naogopa kutoa maneno matamu kwani utajihisi mwenye haki, natumai we ni msomi wa ngazi ya masters na katatizo ulikonacho ni O level tena Div 5. Iyo n simultaneous equation solve bila four figure. Hakikisha no intersection. To make long story short.....njoo na mkorea Tz kaa nae kwa muda tafuta Dada wa ndan kabla ya kufika Tz na nyumba + thaman za ndan . Mkifika mnaendeleza maiaha then utariport kwa wife baadae na usimwambie chochote mpaka ujue hatma ya mkorea/mke mdogo. Ni game rahisi ukijitoa ufahamu vinginevo ....ndi ndi Ndiiindiii ndi
 
Aaaaah! Utazingatiaje Mawazo tofauti!?? Nataka nikushauri mkuu, Mimi mwanaume mwenzako, na shida yako Ni yangu, Mimi mwenyewe nimedanganya kwa Mzungu, kabla sijakushauri nambie......Huyo Mkorea anajua kuwa Una Mtoto au Watoto???
Hajui.
 
Yaani anajikatia tu tiketi, no visa no "nothing"!! Strange bro
 
Kaka chonde chonde usije lopoka ukamwambia ukwel huyo mkorea.....hutorud Tz nakuambia, utafanyiwa zengwe hutosahau maishani mwako..kama una hela kata ticket mpya ya nyuma ya siku ulizotaka kuondoka, then nyanyuka kimia kimia...hayo ya mimba wale ni wazaz wake watarudiana tu kuwa familia.
Ukiona imebuma" fanya kama walivyoshaur wadau, njoo nae Tz bora ajue kila kitu uko hapa kwenu madhara ya kudhuliwa yanweza kuwa machache...japo anaweza nunua bastola pia ukapigwa ......
Mpangie nyumba arusha...mwambie ukwel...safiri kwenda kwako..kaa week moja...then mrudie utakuta akili imemtulia na atakuwa na jibu
 
Rafiki Kwa sasa upo ugenini na jinsi huyo binti alivyokupenda ukifanya kosa dogo litakalo sababisha maamuzi mabaya juu yake tambua kua hio familia inayokusubiri Tz inaweza isikuone so kua makini sana ktk nyakati hizi za mwisho isijekua yale ya Ng'oswe, nivyema ata ukaja nae na ayo mengine yakatokea ukiwa huku Ila c huko kk.
 
Mkuu hiï issue yako ni ndogo sana,
Njoo na Mkorea mpaka dar,nyumbani usiwaambie siku rasmi ya kurudi.
Chukua hotel na Mkorea kwa walau siku 2,then mkiwa katika mapumziko yaliyotukuka mwambie ukweli kwamba una mke na watoto wanakutegemea

Then mpe opption,kwamba mpange nyumba aishi kama mchepuko tena kwa siri kubwa, mpaka utakapo maliza kufile mambo yako na mkeo,mdanganye sheria za nchi haziruhusu kua nae kabla hujaachana na mkeo,otherwise nae anaweza kua matatizoni.

Option ya pili ni yeye kurudi korea.
Hope ataumia lakini lazima atachagua either option ya kwanza au ya pili.
 
Well, tambua huyo Mkorea Ana Damu yako tumboni, angekua Hana Mimba yako ungefikilia kumkimbia, so wazo la kumkimbia ondoa.

Huyo Mkorea Ana true love, kumbuka keshapoteza kila kitu kwa ajiri yako, ndugu mpaka marafiki, wewe ndo ndugu na rafiki yake.

Still bado Ni mwanamke Wako, mwambie wife umesogeza mbele siku ya kuondoka, Rudi naye na mpangie nyumba, mtoe mpeleke hata Mbuga ya wanyama, then umwambie ukweli kuwa Una mke, mwambie bado unamwitaji, na ndo maana ukakubari kurudi naye TZ, na blah blah za kutosha, majibu yake yatafanya ama ukamweleze ukweli wife au vipi, siku ambayo unaenda kwa wife iwe baada ya kujua uwamuzi wa Mkorea!

Usimkimbie coz Ana damu yako, usimkimbie coz ulishamkosanisha na ndugu zake!
 
Aiseeee haya mapenzi toka nizaliwe niliyaona kwenye tamthilia ya ENDLESS LOVE PEKEE star tv....kumbe kwel yapo! Umependwa sana na hiki kiumbe bro ila sasa ndio hivyo....tumia akili sana hapa, huyu kujiua au kukua nje nje kwa kiwango hicho cha mapenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…