Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Wadau,

Nahitaji mchango wa mawazo yenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kisa chenyewe ni hivi mimi ni diaspora ambaye nipo Korea kimasomo tangu November 2014. Mwezi Juni 2016 nahitimu masomo. Nimeoa na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili.

Nikiwa huku Korea ya Kusini nilianza mahusiano na mdada wa kikorea, ni mrembo ila si wa kutisha sana si unajua watu wa ukanda huu kinachowapendezesha ni rangi tu waliyonayo vinginevyo kama wangelipakwa rangi nyeusi hakuna atakaye watamani.

Mdada huyu anajiheshimu sana tulianza kuzoeana kama classmate tu. Alikuwa karibu sana na mimi mpaka tukaanza kuvuka mipaka na kuwa wapenzi. Kosa nililofanya ni kwamba sikuwahi kumweleza ukweli kuhusu hali yangu ya ndoa, yaani nilimdanganya kwamba mimi sijaoa.

Tulianza mahusiano kwa siri kwasababu ya kuhofia jamaa zake wasijue kuwa anamahusiano na ngozi nyeusi. Ilifika wakati usiri ukawa unashindikana maana tulikuwa tunaenda club pamoja na kurudi na kulala aidha sehemu ninayoishi au anayoishi yeye. Kuna wakati mama yake aliwahi kuja juu sana akasema kwamba niachane na bintiye vinginevyo ataliwasilisha swala hilo polisi na ninaweza kufutiwa visa ya kuishi Korea.

Tulishauriana na binti kuwa tuachane ili nisije nikaharibu future yule binti akadai yeye akadai hawezi kuachana na mimi kwasababu hajawahi mjua mwanamume mwingine zaidi yangu tangu azaliwe. Na swala la yeye na mama yake anasema hawezi fanya chochote kwasababu yeye ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu. Nilimsihi tuendelee kwa siri ili nisije nikaharibikiwa kimasomo.

Mwezi uliopita mdada kanimaliza kabisa kaniambia anaujazito wangu, nimechoka mpaka sasa anasisitiza kuwa tunarudi wote Tanzania. Mwanzo nilijua ni utani lakini mpaka nimejua kuwa hatanii. Kwasababu ya urahisi jana Jumatatu nilimtuma yeye aende kunikatia ticket ya ndege amerudi na ticketi mbili yangu na ya kwake tunayosafiri pamoja.

Nimeshikwa na mfadhaiko, nimejaribu kumwambia tu kwa busara kwamba yeye angebaki kwanza ili nikafanye maandalizi ya kumpokea maana mimi nilipotoka nilikabidhi nyumba niliyokuwa naishi hivyo kwenda mahali na mgeni sina mahali pa kufikia itakuwa si vizuri.

Yeye amesisitiza kuna shida gani nikatapo lala naye atalala hata kama kibarazani. Pia akasema hawezi kuendelea kuwepo Korea maana ndugu zake wanaweza hata kumwambia atoe ujauzito wangu na pia wanaweza kumtenga ni heri akaondoka akaenda kuishi na mtu anayempenda hata kama ni sehemu ya tabu.

Kuhusu pesa yeye anasema sio shida anakiasi cha fedha ambazo ukizibadili zinaweza kufikia hadi 150 m ambazo zilikuwa ni mirathi ya marehemu baba yake. Kiukweli mdada huyu amenisaidia sana kifedha. Sikuwahi kuwa na shida ya kifedha muda wote nikiwa Korea.

Hofu yangu ni nyumbani ambako mke na watoto wangu wananingojea kwa hamu, nimeshindwa hata kuwanunulia zawadi maana huyu mdada anajua kila kitu ninachofanya. Ndani kwangu ni kama kwake. Jana nilipanga nimwambie ukweli lakini nilipokuwa namtazama nikajua anaweza nivuruga mpaka nikashindhwa kufanya mitihani yangu ya mwisho. Pia nilimwonea huruma sana kwamba naye anaweza asifanye vizuri hiyo mitihani yake. Ananipenda sana mpaka namuonea huruma sijui nikimwangalia.

Nilikuwa nafikiri nimwache wakati narudi nikifika Doha wakati wa kubadili ndege nimchenge potelea mbali hata kama nitakula hasara ya ticket. Lakini nimejikuta naona hiyo itakuwa ni kazi bure maana mdada huyu anajua mpaka ninapofanya kazi anwani yangu ya Tz anazo hata akaunti namba ya benki yangu anayo mana kuna wakati nikiwa likizo Tz alishawahi kunitumia pesa kwenye akaunti zangu.

Mke wangu na wanangu wananisubiria kwa hamu sana, na wanadai niwapelekee zawadi japo natoa kisingizio kwamba nimebakiwa na fedha ya nauli tu. Cha ajabu wife akasema basi atanitumia kwa Western Union mana kuna vitu nilishawahi kuwapelekea ni vizuri sana na vilikuwa vinauzwa bei ya chini sana. Huku mrembo wa kikorea naye anahesabu siku zilizobakia ili aweze kuruka nami kuja Tz.

Msaada wa kutatua tatizo hilo wadau. Niko njia panda nampenda mke wangu nawapenda wanangu. Namhurumia Mkorea alivyojitoa kwangu.

Nawasilisha kwa ajili ya ushauri.
hizo wanaziita nyeg.......mshindo
 
utazini sirini ...ila matokeo hayatakuwa sirini tena...Pole bro.....nyegee ni nyouuukooooo
 
Kweli kaka damu yangu ni muhimu sana, ila cha muhimu ni kutafuta suluhisho wa tatizo hili lilipo kwanza.

Haya basi ukishafanya mtihani mwambie ukweli huyo Mkorea. Baada ya hapo uangalie reaction yake ili ujue cha kufanya. Ukitaka tena ushairi baada ya kumwambia na reaction yake uje tena hapa tushauriane, lakini anza na hilo kwanza
 
Nahofu nikimwambia nikiwa bado ndani ya ardhi ya naweza pata matatizo. Huyu binti aliwaahi kusimama kidete kumpinga mama yake na ndugu zake wengine. Alikuwa yuko radhi tuache kuache kusoma Korea twende tukasomee South Afrika ili tuishi kwa ama mimi na yeye bila bughudha za ndugu zake.
Siku zote uongo ni gharama, ungemwambia ukweli tokea mwanzo usingekuwa unaumiza kichwa namna hii. Mwambie ukweli achague kusuka au kunyoa.
 
Mpole sana .kwa hapo ulipofikia ni kufanya vitu viwili tu .kuomba msmaha. Msamaha na Kutubu kwa Mkorea,Kwa wife na Kwa Baba wa Mbinguni.her love was so pure .what a waste!

Kwa maelezo huyo Mkorea ana true love kabisa, kwa kweli what a waste. Namuonea huruma sana maana yuko kwenye peak ya upendo hadi kuwa tayari kuja TZ alafu ghafla upendo unaingiwa na dosari. Ndio maana huwa wanajinyonga. Sasa hapo anaweza kujiua yeye na mtoto pia akapotea kwa sababu tu ya kutosema ukweli
 
KOSA LAKO KUBWA NI UONGO....
-Kwann ulidanganya at the firstplace?
-Chakufanya kwasasa mjulishe MKEO, mwambie hali halisi ili naye umsikie ANASEMAJE
-Next time ukirudi tena nchi za watu kwa MASTERS au PHD nadhani hutarudia tena Kosa..
Mh haya kheri ayafanye wakiwa ana kwa ana. Anaweza kuchukua uamuzi wa kipuuzi siku mbili hizi jamaa hajarudi.
 
be a man kata tiketi nyingine ya ndege, tarehe ya mapema then toroka , badili namba ya simu email, hela iliyo benki yote chukua
 
Ajoshiii...Anyohaseyoooo!!

Option 1:
Wakati mnajiandaa kumalizia mitihani, anza kujipanga mapema kumuweka chini umweleze kuhusu kutofurahishwa nayeye kushika mimba bila kukushirikisha. Muonyeshe umekasirika sana unahitaji muda wa pekee kutafakari.

Akikupa muda wa kutafakari, hapo ndo michoro yooote utaichora ikiwa ni pamoja na kununua zawadi (unaweza kumpa hata mshikaji akakaa nazo) then kata ticket yako ya mapema zaidi mpe mshikaji wako akakae nayo pia. Harafu siku unamaliza tu mtihani (anza mishe mishe za kusafiri) achana na mambo ya graduation kabisa.

Wewe bwana kama unataka mambo yaende sawa, hakikisha unamtoroka kabla ya siku hiyo mliokata ndege. Umekata ticket ya kampuni gani? Ethiopian, Qatar Airways, Etihad? Kata ndege ya shirika lingine siku ambayo ni ya mapema zaidi.

Option 2: Kama utaona kazi kubwa kumtoroka, basi siku ya mtihani wa mwisho (last day) ndo usafiri ...singizia hata kuwa una msiba mzito nyumbani na hauko sawa. Hapo kwa gharama yeyote lazima uondoke na utawasiliana naye ukiwa umeshafika bongo kuhusu kumwambia ukweli.

Option 3: Naimani mimba bado iko trimester ya kwanza, bado inamzengua haswa. Sasa basi unaweza kusubiri hadi mitihani ikaisha, hope pia kuna gap kati ya siku ya kusafiri na siku ya kumaliza mitihani: mwambie unataka kwenda Shangai, China kwa ajili ya kununua mizigo ya biashara kuipeleka Tanzania ili upate pakuanzia, akikataa mwambie unataka kwenda kuchukua mizigo kwa rafiki yako amekupa basi ndo gia ya kwenda Busan ukapande meli huyoo Japan. Ukifika Japan umeshaula...unatafafuta namna ya kusepa kwenda bongo kiulainiiiii.

Mdogo wangu ukiendelea kuwa kwenye himaya yake, uwe tayari kukubali matokeo. Nawajua hao jamaa hawana mchezo.

Anyohikaseyooooo!!!
 
Wadau,

Nahitaji mchango wa mawazo yenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kisa chenyewe ni hivi mimi ni diaspora ambaye nipo Korea kimasomo tangu November 2014. Mwezi Juni 2016 nahitimu masomo. Nimeoa na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili.

Nikiwa huku Korea ya Kusini nilianza mahusiano na mdada wa kikorea, ni mrembo ila si wa kutisha sana si unajua watu wa ukanda huu kinachowapendezesha ni rangi tu waliyonayo vinginevyo kama wangelipakwa rangi nyeusi hakuna atakaye watamani.

Mdada huyu anajiheshimu sana tulianza kuzoeana kama classmate tu. Alikuwa karibu sana na mimi mpaka tukaanza kuvuka mipaka na kuwa wapenzi. Kosa nililofanya ni kwamba sikuwahi kumweleza ukweli kuhusu hali yangu ya ndoa, yaani nilimdanganya kwamba mimi sijaoa.

Tulianza mahusiano kwa siri kwasababu ya kuhofia jamaa zake wasijue kuwa anamahusiano na ngozi nyeusi. Ilifika wakati usiri ukawa unashindikana maana tulikuwa tunaenda club pamoja na kurudi na kulala aidha sehemu ninayoishi au anayoishi yeye. Kuna wakati mama yake aliwahi kuja juu sana akasema kwamba niachane na bintiye vinginevyo ataliwasilisha swala hilo polisi na ninaweza kufutiwa visa ya kuishi Korea.

Tulishauriana na binti kuwa tuachane ili nisije nikaharibu future yule binti akadai yeye akadai hawezi kuachana na mimi kwasababu hajawahi mjua mwanamume mwingine zaidi yangu tangu azaliwe. Na swala la yeye na mama yake anasema hawezi fanya chochote kwasababu yeye ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu. Nilimsihi tuendelee kwa siri ili nisije nikaharibikiwa kimasomo.

Mwezi uliopita mdada kanimaliza kabisa kaniambia anaujazito wangu, nimechoka mpaka sasa anasisitiza kuwa tunarudi wote Tanzania. Mwanzo nilijua ni utani lakini mpaka nimejua kuwa hatanii. Kwasababu ya urahisi jana Jumatatu nilimtuma yeye aende kunikatia ticket ya ndege amerudi na ticketi mbili yangu na ya kwake tunayosafiri pamoja.

Nimeshikwa na mfadhaiko, nimejaribu kumwambia tu kwa busara kwamba yeye angebaki kwanza ili nikafanye maandalizi ya kumpokea maana mimi nilipotoka nilikabidhi nyumba niliyokuwa naishi hivyo kwenda mahali na mgeni sina mahali pa kufikia itakuwa si vizuri.

Yeye amesisitiza kuna shida gani nikatapo lala naye atalala hata kama kibarazani. Pia akasema hawezi kuendelea kuwepo Korea maana ndugu zake wanaweza hata kumwambia atoe ujauzito wangu na pia wanaweza kumtenga ni heri akaondoka akaenda kuishi na mtu anayempenda hata kama ni sehemu ya tabu.

Kuhusu pesa yeye anasema sio shida anakiasi cha fedha ambazo ukizibadili zinaweza kufikia hadi 150 m ambazo zilikuwa ni mirathi ya marehemu baba yake. Kiukweli mdada huyu amenisaidia sana kifedha. Sikuwahi kuwa na shida ya kifedha muda wote nikiwa Korea.

Hofu yangu ni nyumbani ambako mke na watoto wangu wananingojea kwa hamu, nimeshindwa hata kuwanunulia zawadi maana huyu mdada anajua kila kitu ninachofanya. Ndani kwangu ni kama kwake. Jana nilipanga nimwambie ukweli lakini nilipokuwa namtazama nikajua anaweza nivuruga mpaka nikashindhwa kufanya mitihani yangu ya mwisho. Pia nilimwonea huruma sana kwamba naye anaweza asifanye vizuri hiyo mitihani yake. Ananipenda sana mpaka namuonea huruma sijui nikimwangalia.

Nilikuwa nafikiri nimwache wakati narudi nikifika Doha wakati wa kubadili ndege nimchenge potelea mbali hata kama nitakula hasara ya ticket. Lakini nimejikuta naona hiyo itakuwa ni kazi bure maana mdada huyu anajua mpaka ninapofanya kazi anwani yangu ya Tz anazo hata akaunti namba ya benki yangu anayo mana kuna wakati nikiwa likizo Tz alishawahi kunitumia pesa kwenye akaunti zangu.

Mke wangu na wanangu wananisubiria kwa hamu sana, na wanadai niwapelekee zawadi japo natoa kisingizio kwamba nimebakiwa na fedha ya nauli tu. Cha ajabu wife akasema basi atanitumia kwa Western Union mana kuna vitu nilishawahi kuwapelekea ni vizuri sana na vilikuwa vinauzwa bei ya chini sana. Huku mrembo wa kikorea naye anahesabu siku zilizobakia ili aweze kuruka nami kuja Tz.

Msaada wa kutatua tatizo hilo wadau. Niko njia panda nampenda mke wangu nawapenda wanangu. Namhurumia Mkorea alivyojitoa kwangu.

Nawasilisha kwa ajili ya ushauri.
Ukipika chai make sure inakuwa ya maziwa siyo kutupikia chai ya rangi kwa kutumia mavi ya ngombe halafu haina sukari au vipi? btw shule ipi ya Kata unayosoma?
 
Ukisikia kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi ndio hii sasa.
 
Pole sana kamanda, fanya yoote ila sio kumuambia ukweli (at least for now)!
Kwako ni rahishi sana kuozea gerezan au kurudishwa huku wakati hujamaliza chuo, hapo kufa na tai shingoni kila kitu kiishe then utajua la kufanya,

Rahisi kuliko vyooote ni kubadili mawazo ya kurudi bongo, atakusaidia kutafuta kazi nzurina maisha yataendelea,
 
Back
Top Bottom