Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz


Ndege za kuja bongo hazipoteagi labda apande ya malaysia au misri
 
Futa kwanza kauli yako Kuwa unampenda mkeo. HUMPENDI MKEO
Ni kweli kumpenda mtu ni kuwa proud naye popote pale unapokuwa. Sasa wewe umemkana mkeo kuwa hujaoa. Kwa maneno mengine umekana kiapo ulichoapa mbele ya Mwenyezi Mungu. Sasa hiyo dhambi inakusulubu.
Njia uliyoichagua ni ngumu bro. Hata huu ushauri wanaokupa sioni kama ni njia ya kutokea. Mkorea kakupenda kweli toka moyoni mpaka akaweka rehani uhusiano wake na Mama yake na familia kwa fisadi wa mapenzi. Daah inagine huyo Mkorea angekuwa ni binti yako?!! Tuwe na roho ya utu jamani. Tusiongozwe na kichwa cha chini tu...
 
Kuna mambo unatakiwa uyajue kabla ya wewe kupanda ndege na kurudi nyumbani. Kama kazi unayosomea huko korea ikiwa inakulipa ukibakia hukohuko korea basi ni vema na nibusara ukibakia huko na kuajiriwa huko.

Jambo la pili kwa sasa hapa tz wafanyakazi walio wengi wa serikalini wanalia ugumu wa kazi pesa imekuwa ngumu,sasa kwa kigezo hicho pia unatakiwa utazame kwa umakini maamuzi yako ya kurejea hapa nchini.

Huyo mwanadada kama ni mtu wa kujishughulisha endelea kutengeneza nae maisha,uwe unatuma pesa nchini ili huyu mswahili mwenzetu aendelee kulea wana.

Hayo ndiyo maono yangu,wadada wa kiswahili wanajulikana kwa uvumilivu sifuri,tena wanasifika kweli kuhonga michepuko kwa pesa za kujikimu mnazowatumia mara kwa mara.

Wale wa kaskazini wanasemaga aikambe
 
Ha ha ha mkuu ushauri wako mzuri pia umenipunguzia stress kwamba watu wasiokuwa na P.O Box, nimecheka kwa sauti.
 
Fanya maamuzi magumu,mwambie mila za kitanzania huwa mwanaume unatafutiwa mwanamke wa kuoa,sasa kama atakubali kuwa mke wa pili ajue toka anaondoka korea ili ukifika Tanzania ajue kabisa hayupo peke yake,otherwise tatizo ulilo create litakusumbua for the rest of ure life.
 

Sasa wakati anafanya hivyo kwa nini huku mwambia ukweli kuhusu marital status yako.
Hivi nyie wanaume mkipendwaga kwa dhati mnaona ni muvi au ?????
Yani hapo umeshaharibu life la mdada wa wAtu na huyo mtoto atakaye zaliwa.
Mini sina hata cha kukushauri kwa kweli
You are in a deep mess
Go for two wifes ukiweza.
 
Mkuu naomba unielewe sikuwa kukana kwamba nimeoa. Wala mkorea hakuwahi kujua kuwa nimeoa. Tena hakuwahi hata kuniuliza. Ila kuna kipindi aliwahi shitukia simu zilizokuwa zinatoka kwa wife akawa anahoji nimepokea simu kutoka kwa nani nikamjibu tu my family member from Tz, akaanza kudadisi mbona kama nilikuwa so romantic wakati naongea. Kwa upande wa msg yeye alikuwa hawezi kusoma kiswahili, wife muda wote huwa tunachati kiswahili.
Sikuwa na mpango wa kuwa na mahusiano naye ila tulikuwa marafiki tu. Nilionyesha tabia njema tofauti na vijana wa kinamibia tunawosoma nao maana wao walikuwa ni watu wa kujirusha sana. Mimi nilikuwa naonekana mstaarabu fulani. Akawa rafiki, tunadiscuss pamoja ukizingatia kozi ninayosoma mimi nilikuwa msaada sana kwake sababu uwezo wa lugha. Sikuwahi kujua kama tutakuja kuwa wapenzi.
Hata tulipokuja kuwa wapenzi sikujua kama yatakuwa ni muda mrefu. Nilijua tu tunapoteza muda lakini bahati mbaya mwenzangu akamaanisha kwenye mahusiano. Ghafla akawaamendelea mbele sana kimahusiano kwa hiyo nikawa pia na hofu ya kumuumiza kwa jinsi alivyokuwa amejitoa kwangu. Tatizo la mama yake lilipoibuka ndipo nilipotambua msimamo wake, nikaogopa zaidi kwamba huyu binti anaweza kufanya jambo la ajabu la kunidhuru au kujidhuru mana tayari ndugu zake wameshamtenga, hapo ndipo nikaanza juhudi za makusudi za kuficha habari zangu za ndoa.
Pamoja na maelezo yote hayo bado nakiri kwamba nimefanya kosa tena si kosa dogo ni deadly mistake nahitaji kusahihisha hilo kosa hata kama ni kufanya kosa jingine.
 
Inaonekana una mtmb vizuri mtoto wa Kikorea mpaka kakung'ang'ania... Sasa huo msala kuumaliza ni bora utafute namna ya kuendelea kubaki Korea mpaka 'mkeo' ajifungue huku unatafakari cha kufanya... maana sio busara kuchukua maamuzi ya ghafla...
 
Hivi Korea kusini hawauzi condoms? Miaka yote mitatu hukuchukua picha ya mkeo na mwanao na kuviweka mezani au ukutani? Una uhakika unampenda mkeo kweli? Hata kumtaja kwa mtu yeyote hukuwahi kweli? Wenzio hutembea na picha za wenzao kwenye wallet wewe je? Naomba majibu hayo.
 
All your question have been addressed....
 
Hapo ndipo ulipomsaliti mwenzako(my wife wako) it was the right time there and then to break the ice kwamba mimi nimeoa kule nyumbani na nina familia, lakini kwa kuwa uliogopa kumueleza Mkorea ukihofia ataumia roho. Then ni wakati muafaka sasa umuelemze mkeo kuwa ulikuwa unaishi kindoa kule masomoni na huyo mama wa Korea ameridhia kujiunga na familia yetu katika hali yoyote...
 
Sasa unaogopa nini mkuu?kama baba yako yupo hai mwambie hii issue na yeye akaongee na mke wako kwanza kisha akishaongea wewe ndo uwasiliane na mkeo about it. Kisha njoo na mkorea hadi TZ then kaa naye chini muongee. ..wewe sio wa kwanza hii issue huwakuta watu wengi sana wakienda kusoma nje.
Naombea iwe hivyo ili inirahisishie hatua za kuanza kutatua.[/QUOTE
 
All your question have been addressed....
Cos not sababu there is no where you mentioned that you were using condoms, you had your wife and child pics on the wall or on your table otherwise your Korean GF would have asked and that would have been the chance to come out as a married man. You could have tried even to carry your child's pic in your wallet to address the issue. Now come here claiming you love your family really???
 
Mkuu ukitaka kupata balaa mwambie kuwa una mke na watoto. Ukija nae ndo balaa zaidi aana unampeleka wapi? Fanya kila uwezalo usije nae. Tafuta rafiki huku tz wa kazini kwako akuandikie barua kwamba unarudi kwa mwezi mmoja kisha utatakiwa kurudi korea kwa kazi maalum. Mdanganye huyo mdada kuwa wewe ni usalama wa taifa.
 
Mkuu wazo ni zuri sana ila nafikiri nikikosa wazo mbadala lililozuri nitalifanya aidha airport ya huku Seoul tukiwa tumeshacheck in au Doha ili akachachamaa nampotezea.

kijana,una tatizo la kutokuona mbali ufanyapo mambo yako!!!nakuonya fanya yote lakini usifikirie kumtoroka huyo dada,mbaya zaidi ana mimba yako,mbaya zaidi mimba ya mtu wa jamii wasiyopenda kuchangamana nao,amejitolea sana huyo dada kuwa na wewe!!

ushauri wangu,kwa vile umeshaharibu-la kuvunda halina ubani-weka mambo wazi kwa pande zote mbili!
 
Wewe muoe kabisa huyo mkorea kama roho yako inampenda, pia kama umekua kwenye mahusiano na huyo mrembo kwa muda wote huo inaonyesha kabisa huna upendo wa dhati kwa mkeo. Wewe hautakua wa kwanza kuachana na mke bwana,Mandela alimuacha winnie, mengi alimuacha mkewe hata mtume daudi alioa kimada aliekuja kumzalia mtoto Solomon. Wanao uta wasaport tu ukiwa na mke mpya pamoja na mama yao just do what your heart desires.
 
Huko si ni kwa yule mtata Kim Jong?
Mwanangu halahala huko!! Usije ukatumbuliwa
 
Hata mimi sioni sababu ya kumtoroka, kama ningekuwa mimi ningekuja nae, alafu familia yangu ya Tanzania ningeiambia nakuja wiki mbili mbele, ukija nae wiki mbili kabla tafuta nyumba mpangishe maana ulishaeleza kuwa huna nyumba.

Badae rudi kwako, kutana na familia kuanzia hapo mjulishe mkorea full story endeleza siri huku ukitfta namna yakumwambia mkeo kuwa huko korea uliacha mimba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…