Dr Hor
JF-Expert Member
- Dec 1, 2015
- 231
- 162
Inawezekana Mkuu tena kwa asilimia 100 kama wewe ulikuwa huku ukashindwa si wote.Huwezi kugonga mkorea ukiwa Korea
Inawezekana Mkuu tena kwa asilimia 100 kama wewe ulikuwa huku ukashindwa si wote.Huwezi kugonga mkorea ukiwa Korea
Ila inauma eeh!!! Wengi mmemshauri amwambie mkewe ukweli kua anaoa mke mwingine yaani huyu Korea hamjawaza kua hata mke nae ataumia amelea familia toka 2014 akijua mmewe yuko masomoni
Leo fadhila yake kuletewa mke mwingine? Kweli? Wewe kaka bora hiyo ndege utakayopanda ipoteze mawasiliano huko angani familia italia weeee eeee baada ya
muda watazoea kuliko kuwaletea mke mwenza atayeleta ufa ktk hii familia.
Ni kweli kumpenda mtu ni kuwa proud naye popote pale unapokuwa. Sasa wewe umemkana mkeo kuwa hujaoa. Kwa maneno mengine umekana kiapo ulichoapa mbele ya Mwenyezi Mungu. Sasa hiyo dhambi inakusulubu.Futa kwanza kauli yako Kuwa unampenda mkeo. HUMPENDI MKEO
Ha ha ha mkuu ushauri wako mzuri pia umenipunguzia stress kwamba watu wasiokuwa na P.O Box, nimecheka kwa sauti.sina ushauri, ila lolote laweza kuwa, Korea sio Bongo, wanawake wa Kiasia nawaelewa vema. Husijaribu kusema ukiwa kwenye ardhi yao. Ukimtoroka na anayo address atakuja tu maana anayo mimba yako. Umeficha hukusema ukweli hawa watu kuwa na mahusiano na ngozi nyeusi ni shida, wewe ana mimba yako. hawezi kukaa kwao lazima akufuate. Chalii wa Arusha wanasema imekula kwako.
Ondoka naye mlete Bongo, Mweke mahali, then mueleze ukweli na mwambie aamue na unampenda. mwambie utaishi nao wote. ninavyowaelewa hao mwanzoni ataoverlook ila kuna muda atachomoa na kurudi kwao, ila atakuwa ameshakuwa na maamuzi ya kukuacha kwani atakuwa amejua kama alivyoambiwa wanaume wa kiafrica ni matapeli. ni matepeli kweli. huo utakuwa mwisho wake wa kufuata watu wasiokuwa na P.o Box
Fanya maamuzi magumu,mwambie mila za kitanzania huwa mwanaume unatafutiwa mwanamke wa kuoa,sasa kama atakubali kuwa mke wa pili ajue toka anaondoka korea ili ukifika Tanzania ajue kabisa hayupo peke yake,otherwise tatizo ulilo create litakusumbua for the rest of ure life.Wadau,
Nahitaji mchango wa mawazo yenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kisa chenyewe ni hivi mimi ni diaspora ambaye nipo Korea kimasomo tangu November 2014. Mwezi Juni 2016 nahitimu masomo. Nimeoa na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili.
Nikiwa huku Korea ya Kusini nilianza mahusiano na mdada wa kikorea, ni mrembo ila si wa kutisha sana si unajua watu wa ukanda huu kinachowapendezesha ni rangi tu waliyonayo vinginevyo kama wangelipakwa rangi nyeusi hakuna atakaye watamani.
Mdada huyu anajiheshimu sana tulianza kuzoeana kama classmate tu. Alikuwa karibu sana na mimi mpaka tukaanza kuvuka mipaka na kuwa wapenzi. Kosa nililofanya ni kwamba sikuwahi kumweleza ukweli kuhusu hali yangu ya ndoa, yaani nilimdanganya kwamba mimi sijaoa.
Tulianza mahusiano kwa siri kwasababu ya kuhofia jamaa zake wasijue kuwa anamahusiano na ngozi nyeusi. Ilifika wakati usiri ukawa unashindikana maana tulikuwa tunaenda club pamoja na kurudi na kulala aidha sehemu ninayoishi au anayoishi yeye. Kuna wakati mama yake aliwahi kuja juu sana akasema kwamba niachane na bintiye vinginevyo ataliwasilisha swala hilo polisi na ninaweza kufutiwa visa ya kuishi Korea.
Tulishauriana na binti kuwa tuachane ili nisije nikaharibu future yule binti akadai yeye akadai hawezi kuachana na mimi kwasababu hajawahi mjua mwanamume mwingine zaidi yangu tangu azaliwe. Na swala la yeye na mama yake anasema hawezi fanya chochote kwasababu yeye ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu. Nilimsihi tuendelee kwa siri ili nisije nikaharibikiwa kimasomo.
Mwezi uliopita mdada kanimaliza kabisa kaniambia anaujazito wangu, nimechoka mpaka sasa anasisitiza kuwa tunarudi wote Tanzania. Mwanzo nilijua ni utani lakini mpaka nimejua kuwa hatanii. Kwasababu ya urahisi jana Jumatatu nilimtuma yeye aende kunikatia ticket ya ndege amerudi na ticketi mbili yangu na ya kwake tunayosafiri pamoja.
Nimeshikwa na mfadhaiko, nimejaribu kumwambia tu kwa busara kwamba yeye angebaki kwanza ili nikafanye maandalizi ya kumpokea maana mimi nilipotoka nilikabidhi nyumba niliyokuwa naishi hivyo kwenda mahali na mgeni sina mahali pa kufikia itakuwa si vizuri.
Yeye amesisitiza kuna shida gani nikatapo lala naye atalala hata kama kibarazani. Pia akasema hawezi kuendelea kuwepo Korea maana ndugu zake wanaweza hata kumwambia atoe ujauzito wangu na pia wanaweza kumtenga ni heri akaondoka akaenda kuishi na mtu anayempenda hata kama ni sehemu ya tabu.
Kuhusu pesa yeye anasema sio shida anakiasi cha fedha ambazo ukizibadili zinaweza kufikia hadi 150 m ambazo zilikuwa ni mirathi ya marehemu baba yake. Kiukweli mdada huyu amenisaidia sana kifedha. Sikuwahi kuwa na shida ya kifedha muda wote nikiwa Korea.
Hofu yangu ni nyumbani ambako mke na watoto wangu wananingojea kwa hamu, nimeshindwa hata kuwanunulia zawadi maana huyu mdada anajua kila kitu ninachofanya. Ndani kwangu ni kama kwake. Jana nilipanga nimwambie ukweli lakini nilipokuwa namtazama nikajua anaweza nivuruga mpaka nikashindhwa kufanya mitihani yangu ya mwisho. Pia nilimwonea huruma sana kwamba naye anaweza asifanye vizuri hiyo mitihani yake. Ananipenda sana mpaka namuonea huruma sijui nikimwangalia.
Nilikuwa nafikiri nimwache wakati narudi nikifika Doha wakati wa kubadili ndege nimchenge potelea mbali hata kama nitakula hasara ya ticket. Lakini nimejikuta naona hiyo itakuwa ni kazi bure maana mdada huyu anajua mpaka ninapofanya kazi anwani yangu ya Tz anazo hata akaunti namba ya benki yangu anayo mana kuna wakati nikiwa likizo Tz alishawahi kunitumia pesa kwenye akaunti zangu.
Mke wangu na wanangu wananisubiria kwa hamu sana, na wanadai niwapelekee zawadi japo natoa kisingizio kwamba nimebakiwa na fedha ya nauli tu. Cha ajabu wife akasema basi atanitumia kwa Western Union mana kuna vitu nilishawahi kuwapelekea ni vizuri sana na vilikuwa vinauzwa bei ya chini sana. Huku mrembo wa kikorea naye anahesabu siku zilizobakia ili aweze kuruka nami kuja Tz.
Msaada wa kutatua tatizo hilo wadau. Niko njia panda nampenda mke wangu nawapenda wanangu. Namhurumia Mkorea alivyojitoa kwangu.
Nawasilisha kwa ajili ya ushauri.
Nahofu nikimwambia nikiwa bado ndani ya ardhi ya naweza pata matatizo. Huyu binti aliwaahi kusimama kidete kumpinga mama yake na ndugu zake wengine. Alikuwa yuko radhi tuache kuache kusoma Korea twende tukasomee South Afrika ili tuishi kwa ama mimi na yeye bila bughudha za ndugu zake.
Mkuu naomba unielewe sikuwa kukana kwamba nimeoa. Wala mkorea hakuwahi kujua kuwa nimeoa. Tena hakuwahi hata kuniuliza. Ila kuna kipindi aliwahi shitukia simu zilizokuwa zinatoka kwa wife akawa anahoji nimepokea simu kutoka kwa nani nikamjibu tu my family member from Tz, akaanza kudadisi mbona kama nilikuwa so romantic wakati naongea. Kwa upande wa msg yeye alikuwa hawezi kusoma kiswahili, wife muda wote huwa tunachati kiswahili.Ni kweli kumpenda mtu ni kuwa proud naye popote pale unapokuwa. Sasa wewe umemkana mkeo kuwa hujaoa. Kwa maneno mengine umekana kiapo ulichoapa mbele ya Mwenyezi Mungu. Sasa hiyo dhambi inakusulubu.
Njia uliyoichagua ni ngumu bro. Hata huu ushauri wanaokupa sioni kama ni njia ya kutokea. Mkorea kakupenda kweli toka moyoni mpaka akaweka rehani uhusiano wake na Mama yake na familia kwa fisadi wa mapenzi. Daah inagine huyo Mkorea angekuwa ni binti yako?!! Tuwe na roho ya utu jamani. Tusiongozwe na kichwa cha chini tu...
All your question have been addressed....Hivi Korea kusini hawauzi condoms? Miaka yote mitatu hukuchukua picha ya mkeo na mwanao na kuviweka mezani au ukutani? Una uhakika unampenda mkeo kweli? Hata kumtaja kwa mtu yeyote hukuwahi kweli? Wenzio hutembea na picha za wenzao kwenye wallet wewe je? Naomba majibu hayo.
Hapo ndipo ulipomsaliti mwenzako(my wife wako) it was the right time there and then to break the ice kwamba mimi nimeoa kule nyumbani na nina familia, lakini kwa kuwa uliogopa kumueleza Mkorea ukihofia ataumia roho. Then ni wakati muafaka sasa umuelemze mkeo kuwa ulikuwa unaishi kindoa kule masomoni na huyo mama wa Korea ameridhia kujiunga na familia yetu katika hali yoyote...Mkuu naomba unielewe sikuwa kukana kwamba nimeoa. Wala mkorea hakuwahi kujua kuwa nimeoa. Tena hakuwahi hata kuniuliza. Ila kuna kipindi aliwahi shitukia simu zilizokuwa zinatoka kwa wife akawa anahoji nimepokea simu kutoka kwa nani nikamjibu tu my family member from Tz, akaanza kudadisi mbona kama nilikuwa so romantic wakati naongea. Kwa upande wa msg yeye alikuwa hawezi kusoma kiswahili, wife muda wote huwa tunachati kiswahili.
Naombea iwe hivyo ili inirahisishie hatua za kuanza kutatua.[/QUOTE
Cos not sababu there is no where you mentioned that you were using condoms, you had your wife and child pics on the wall or on your table otherwise your Korean GF would have asked and that would have been the chance to come out as a married man. You could have tried even to carry your child's pic in your wallet to address the issue. Now come here claiming you love your family really???All your question have been addressed....
Mkuu ukitaka kupata balaa mwambie kuwa una mke na watoto. Ukija nae ndo balaa zaidi aana unampeleka wapi? Fanya kila uwezalo usije nae. Tafuta rafiki huku tz wa kazini kwako akuandikie barua kwamba unarudi kwa mwezi mmoja kisha utatakiwa kurudi korea kwa kazi maalum. Mdanganye huyo mdada kuwa wewe ni usalama wa taifa.Ushauri wako nitauzingatia. Huyu binti tulipokuwa marafiki hakuwahi niuliza habari za mimi kama nimeoa wala mimi sikuona sababu ya kumwambia kuwa nimeoa. Tukiwa marafiki hakutaka kuona mimi nazungumzia habari za wanawake wengine anatabia fulani ya wivu.
Taratibu tukajikuta tumevuka mipaka, mimi sikuona sababu ya kuweka wazi kwa sababu nilijua ni mahusiano ya muda mfupi na hatuna mpango wa kuoana, bahati mbaya zaidi mwenzangu akanogewa moyo huruma ukawa unaingia ili nisimuumize.
Mimi technique yangu ilikuwa ni kwamba nikisharudi bongo ndio nivunje mahusiano kumbe yeye yuko mbele yangu 300 km. Huo ujauzito kashika makusudi mana siku zote alikuwa makini sana.
Mkuu wazo ni zuri sana ila nafikiri nikikosa wazo mbadala lililozuri nitalifanya aidha airport ya huku Seoul tukiwa tumeshacheck in au Doha ili akachachamaa nampotezea.