Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

KOSA LAKO KUBWA NI UONGO....
-Kwann ulidanganya at the firstplace?
-Chakufanya kwasasa mjulishe MKEO, mwambie hali halisi ili naye umsikie ANASEMAJE
-Next time ukirudi tena nchi za watu kwa MASTERS au PHD nadhani hutarudia tena Kosa..
 
MwanaDiaspora, pole kwa unayopitia. You have crossed the line, you are just facing the consequences.
Swali kwamba ufanyaje sio sahihi kwa sasa, kwa waliowahi kukosea kwa namna hii wanajua kuwa ni swala la muda tu Kabla dunia haijakujua vizuri.
Mkeo atajua vile ulivyo, hata watoto wako pia.
Haya ni aina ya makosa ambayo ukijaribu kuzuia matokeo yake basi inazidisha damage.
Unaweza kufanya yafuatayo.
1. Mweleze binti wa Kikorea kuwa una mke na watoto ( haitamshangaza maana Waafrika hatuaminiki Sana)
2. Kwa mkeo subiri kidogo, huna haja ya kukwambia chochote kwa sasa mpaka utakapopata response ya Mkorea ambaye she will likely opt for abortion.
3. Don't feel guilty..haisaidii you are guilt already
4. Sio wakati wa kutangazia ulimwengu kuwa unampenda sana mkeo kilichofanyika ni kinyume kabisa na maneno hayo labda Kama una maana nyingine ya Upendo.

Acha tusubiri.
 
Mkuu kwa hili jambo, ukweli ndio utakaokuweka huru ata kama ni mchungu, Nakushauri maliza kwanza mitihani then mwambie mkorea ukweli kuhusu marital status yako, kisha yeye atatafakari. Ukirudi nyumbani mueleze mkeo, cha muhimu usitelekeze damu yako yaani mtoto atakayezaliwa na mkorea, ukitelekeza ni mbaya sana hata kwa Mungu.
 
Mkuu wazo ni zuri sana ila nafikiri nikikosa wazo mbadala lililozuri nitalifanya aidha airport ya huku Seoul tukiwa tumeshacheck in au Doha ili akachachamaa nampotezea.
Do not do that! Kwanza tuliza mawazo ili ujipange vizuri. Je, uwezekano wa wewe kukaa na kutafuta shillingi huko upo vipi?
 
Aise pole sana, hapo naona fanya umlete Tz alafu danganya familia utachelewa kidogo, mpangishie mahali alafu nenda kwa mke na watoto. Alafu ufanye uwe unatembelea potepote, maana kwamba huyo ashakuwa nyumba ndogo regardless dini yako bro. Akijifungua mwambie ukweli wote na kwamba yeye atakuwa nyumba ndogo na akusamehe kwa uongo, maisha yasonge.

Ila umebugi kinyama we jamaa, na nyie ndio mnafanya hadi race yetu as black melanin peeps tuonekane hovyo.
Ushauri wako nitauzingatia. Huyu binti tulipokuwa marafiki hakuwahi niuliza habari za mimi kama nimeoa wala mimi sikuona sababu ya kumwambia kuwa nimeoa. Tukiwa marafiki hakutaka kuona mimi nazungumzia habari za wanawake wengine anatabia fulani ya wivu.

Taratibu tukajikuta tumevuka mipaka, mimi sikuona sababu ya kuweka wazi kwa sababu nilijua ni mahusiano ya muda mfupi na hatuna mpango wa kuoana, bahati mbaya zaidi mwenzangu akanogewa moyo huruma ukawa unaingia ili nisimuumize.

Mimi technique yangu ilikuwa ni kwamba nikisharudi bongo ndio nivunje mahusiano kumbe yeye yuko mbele yangu 300 km. Huo ujauzito kashika makusudi mana siku zote alikuwa makini sana.
 
Nahofu nikimwambia nikiwa bado ndani ya ardhi ya naweza pata matatizo. Huyu binti aliwaahi kusimama kidete kumpinga mama yake na ndugu zake wengine. Alikuwa yuko radhi tuache kuache kusoma Korea twende tukasomee South Afrika ili tuishi kwa ama mimi na yeye bila bughudha za ndugu zake.
Usicheze na mwanafunzi wa mapenzi, anaweza kukuondoa hivi hivi. Jipange kijana ndiyo uanaume huo
 
Mwambie mkeo kuwa unae mchepuko wa kikorea na anakuzingua.
 
Sikiliza wewe kakate tiketi yako kwa pesa yako siku nyingine na ndege nyingine halafu mtoroke ila akikisha unamwandikia mail yenye ukweli wote kisha ama hapo ulipo nenda kapige shopping kwa ajili ya familia kisha unasepa kimya kimya. Hqkijua ukweli hawezi kukutafuta tena maana roho itamwingia nyongo na kama akikutafuta au akija Bongo ujue huyo kaja kukuua
 
Pole sana, pia ufikirie mtoto wako huyo mkorea ni damu yako hiyo, unaiacha vipi? Pia umwambie ukweli mkeo kuwa unatarajia mtoto na mkorea umpe story nzima. Hakuna kitu nakithamini kama damu yangu. Ukimkimbia huyo mkorea baadae utakuja kuwaza kuhusu mtoto wako, na unaweza kujutia maamuzi yako. Ulishindwa kusema ukweli mwanzo, useme wote sasa Lubebenamawe
 
Huyo
Wadau,

Nahitaji mchango wa mawazo yenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kisa chenyewe ni hivi mimi ni diaspora ambaye nipo Korea kimasomo tangu November 2014. Mwezi Juni 2016 nahitimu masomo. Nimeoa na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili.

Nikiwa huku Korea ya Kusini nilianza mahusiano na mdada wa kikorea, ni mrembo ila si wa kutisha sana si unajua watu wa ukanda huu kinachowapendezesha ni rangi tu waliyonayo vinginevyo kama wangelipakwa rangi nyeusi hakuna atakaye watamani.

Mdada huyu anajiheshimu sana tulianza kuzoeana kama classmate tu. Alikuwa karibu sana na mimi mpaka tukaanza kuvuka mipaka na kuwa wapenzi. Kosa nililofanya ni kwamba sikuwahi kumweleza ukweli kuhusu hali yangu ya ndoa, yaani nilimdanganya kwamba mimi sijaoa.

Tulianza mahusiano kwa siri kwasababu ya kuhofia jamaa zake wasijue kuwa anamahusiano na ngozi nyeusi. Ilifika wakati usiri ukawa unashindikana maana tulikuwa tunaenda club pamoja na kurudi na kulala aidha sehemu ninayoishi au anayoishi yeye. Kuna wakati mama yake aliwahi kuja juu sana akasema kwamba niachane na bintiye vinginevyo ataliwasilisha swala hilo polisi na ninaweza kufutiwa visa ya kuishi Korea.

Tulishauriana na binti kuwa tuachane ili nisije nikaharibu future yule binti akadai yeye akadai hawezi kuachana na mimi kwasababu hajawahi mjua mwanamume mwingine zaidi yangu tangu azaliwe. Na swala la yeye na mama yake anasema hawezi fanya chochote kwasababu yeye ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu. Nilimsihi tuendelee kwa siri ili nisije nikaharibikiwa kimasomo.

Mwezi uliopita mdada kanimaliza kabisa kaniambia anaujazito wangu, nimechoka mpaka sasa anasisitiza kuwa tunarudi wote Tanzania. Mwanzo nilijua ni utani lakini mpaka nimejua kuwa hatanii. Kwasababu ya urahisi jana Jumatatu nilimtuma yeye aende kunikatia ticket ya ndege amerudi na ticketi mbili yangu na ya kwake tunayosafiri pamoja.

Nimeshikwa na mfadhaiko, nimejaribu kumwambia tu kwa busara kwamba yeye angebaki kwanza ili nikafanye maandalizi ya kumpokea maana mimi nilipotoka nilikabidhi nyumba niliyokuwa naishi hivyo kwenda mahali na mgeni sina mahali pa kufikia itakuwa si vizuri.

Yeye amesisitiza kuna shida gani nikatapo lala naye atalala hata kama kibarazani. Pia akasema hawezi kuendelea kuwepo Korea maana ndugu zake wanaweza hata kumwambia atoe ujauzito wangu na pia wanaweza kumtenga ni heri akaondoka akaenda kuishi na mtu anayempenda hata kama ni sehemu ya tabu.

Kuhusu pesa yeye anasema sio shida anakiasi cha fedha ambazo ukizibadili zinaweza kufikia hadi 150 m ambazo zilikuwa ni mirathi ya marehemu baba yake. Kiukweli mdada huyu amenisaidia sana kifedha. Sikuwahi kuwa na shida ya kifedha muda wote nikiwa Korea.

Hofu yangu ni nyumbani ambako mke na watoto wangu wananingojea kwa hamu, nimeshindwa hata kuwanunulia zawadi maana huyu mdada anajua kila kitu ninachofanya. Ndani kwangu ni kama kwake. Jana nilipanga nimwambie ukweli lakini nilipokuwa namtazama nikajua anaweza nivuruga mpaka nikashindhwa kufanya mitihani yangu ya mwisho. Pia nilimwonea huruma sana kwamba naye anaweza asifanye vizuri hiyo mitihani yake. Ananipenda sana mpaka namuonea huruma sijui nikimwangalia.

Nilikuwa nafikiri nimwache wakati narudi nikifika Doha wakati wa kubadili ndege nimchenge potelea mbali hata kama nitakula hasara ya ticket. Lakini nimejikuta naona hiyo itakuwa ni kazi bure maana mdada huyu anajua mpaka ninapofanya kazi anwani yangu ya Tz anazo hata akaunti namba ya benki yangu anayo mana kuna wakati nikiwa likizo Tz alishawahi kunitumia pesa kwenye akaunti zangu.

Mke wangu na wanangu wananisubiria kwa hamu sana, na wanadai niwapelekee zawadi japo natoa kisingizio kwamba nimebakiwa na fedha ya nauli tu. Cha ajabu wife akasema basi atanitumia kwa Western Union mana kuna vitu nilishawahi kuwapelekea ni vizuri sana na vilikuwa vinauzwa bei ya chini sana. Huku mrembo wa kikorea naye anahesabu siku zilizobakia ili aweze kuruka nami kuja Tz.

Msaada wa kutatua tatizo hilo wadau. Niko njia panda nampenda mke wangu nawapenda wanangu. Namhurumia Mkorea alivyojitoa kwangu.

Nawasilisha kwa ajili ya ushauri.
Ndio Shetani mkuu,ameshamaliza kazi yake na sasa kakuachia msala hana msaada wowote zaidi ya kukucheka ujinga.HAKUNA DHAMBI NZURI,ndio maana Mungu alituonya tukae nayo mbali.
 
Hivi hawa wakorea si ndio kina JUMONG? na kina IRIS? Mkuu hilo unalo. Cha kufanya muandae rafiki yako wa Tz akuandalie nyumba mbali na kwako. Mwambie wife umeahirisha safari utamwambia ukiwa tayari, acha kuwasiliana na wife kwa muda. Njoo Tz ukifika jipange maisha mapya na mkorea. Baada ya Muda mpange sasa ili ajue A-Z.
 
Ushauri wako nitauzingatia, ila umeharibu ulipotukana, hujui mazingira niliyokuwa nayo, huyu binti tulipokuwa marafiki hakuwahi niuliza habari za mimi kama nimeoa wala mimi sikuona sababu ya kumwambia kuwa nimeoa. Tukiwa marafiki hakutaka kuona mimi nazungumzia habari za wanawake wengine anatabia fulani ya wivu. Taratibu tukajikuta tumevuka mipaka, mimi sikuona sababu ya kuweka wazi kwa sababu nilijua ni mahusiano ya muda mfupi na hatuna mpango wa kuoana, bahati mbaya zaidi mwenzangu akanogewa moyo huruma ukawa unaingia ili nisimuumize. Mimi technique yangu ilikuwa ni kwamba nikisharudi bongo ndio nivunje mahusiano kumbe yeye yuko mbele yangu 300 km. Huo ujauzito kashika makusudi mana siku zote alikuwa makini sana.

Wanawake tukipenda kwenye uhusiano tunafikiria kinachotokea next, unafarijika pale mtu anapokuuliza maswali kama, uko tayari kuishi Afrika?, Ungependa kuzaa watoto wangapi, majina ya watoto, ukiona hivi vyote hakuna unaanza kusoma namba 'I'm here just for a ride'.
Either unaanza kupotezea, kuna wanaopenda kupita hao ndio wanawaza mbinu mbadala.
 
Huyo mwanamke sio mjinga, ukipotea Seoul ataripot na ndege inaweza kucheleweshwa, utaumbuka. Ni ngumu kumeza lakini kuwa mkweli. Hapa ndipo tunapowazidi kete wanaume. Mwanamke ukichepuka unazuia mimba tu labda magonjwa ya kuumbue lakini ukirudi home uko fresh.
Asante sana umenifunua hilo mana anaweza zusha nimemuibia, mpaka sasa anataka kiasi cha fedha alichonacho anataka ahamishie kwenye akaunti yangu kwa madai ya kwamba benki alimohifadhia hizo fedha sio international. Mimi nimweleza kuwa kiasi hicho cha fedha kikiingia kwenye account yangu ninaweza kuhisiwa kuwa natakatisha fedha hivyo nikamshauri afungue kwenye benki ambayo ni international hilo amenielewa. Lengo langu ni kupunguza kufungamana naye.
 
Kama suala la kuchagua mimi nashauri uchague kubaki na Mke kuliko huyo mkorea.

Sacrifice mahusiano ya huyo mkorea.

Kwa jinsi ninavyo wajua wazungu. Ukiamua kumuacha Mkeo ili uendelee kuishi na huyo Mkorea, hakika nakwambia ipo siku atakumbuka kwa na atakuambia anahitaji kurudi kwao na mtoto, tena kwa lengo la kuishi huko moja kwa moja.

(Wanasema mfuga nyani awe tayari siku nyani atakapo kumbuka pori na kuamua kurudi)

Hapo ndipo utakapo anza kumkumbuka mkeo na kujutia kwa nini ulimuweka pembeni na kumpa nafasi mkorea.
Mkuu sina mpango wa kumuacha mke wangu natafuta namna ya kumueleza huyo mkorea ili anielewe na tuachane kwa amani.
 
Njoo nae TZ ila mfikie hotel, then mkifika muambie ukweli tu na kwamba mtaishi wote ila mkeo wa ndoa hutamuambia. Itabidi umtafutie nyumba ili awe mke mdogo. Lete mbegu ya ki-korea Tz kaka. U never know ya mbeleni mana unaweza ukamuacha na akagoma kutoa mimba na itansumbua sana hiyo kitu. Wewe njoo nae ni bora ajulie ukweli akiwa huku tu.
 
Back
Top Bottom