Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Mwambie mkeo, umueleweshe kosa ulilofanya, akikataa,mkimbie mkorea ila akielewa, muoe kwa siri mkorea na endelea na mkeo. Usimuache mkeo.
 
Tafadhari sana Ndugu yangu, usimuache huyo mdada wa kikorea, nakuomba ndugu, Cha msingi, Vumilia mmalize mitihani ninyi nyote, baada ya kumaliza, mje Tanzania wote na mpange nyumba, kikubwa cha kufanya hapa, ni kwamba andaa mazingira ya kumweleza ukweli mkeo na ndugu zako wa karibu hasa Dada na mama na baba, ili muone jinsi ya kufanya...

Dada wa watu ataumia sana na ataumbuka mbele ya mama yake...!
 
Wadau,

Nahitaji mchango wa mawazo yenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kisa chenyewe ni hivi mimi ni diaspora ambaye nipo Korea kimasomo tangu November 2014. Mwezi Juni 2016 nahitimu masomo. Nimeoa na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili.

Nikiwa huku Korea ya Kusini nilianza mahusiano na mdada wa kikorea, ni mrembo ila si wa kutisha sana si unajua watu wa ukanda huu kinachowapendezesha ni rangi tu waliyonayo vinginevyo kama wangelipakwa rangi nyeusi hakuna atakaye watamani.

Mdada huyu anajiheshimu sana tulianza kuzoeana kama classmate tu. Alikuwa karibu sana na mimi mpaka tukaanza kuvuka mipaka na kuwa wapenzi. Kosa nililofanya ni kwamba sikuwahi kumweleza ukweli kuhusu hali yangu ya ndoa, yaani nilimdanganya kwamba mimi sijaoa.

Tulianza mahusiano kwa siri kwasababu ya kuhofia jamaa zake wasijue kuwa anamahusiano na ngozi nyeusi. Ilifika wakati usiri ukawa unashindikana maana tulikuwa tunaenda club pamoja na kurudi na kulala aidha sehemu ninayoishi au anayoishi yeye. Kuna wakati mama yake aliwahi kuja juu sana akasema kwamba niachane na bintiye vinginevyo ataliwasilisha swala hilo polisi na ninaweza kufutiwa visa ya kuishi Korea.

Tulishauriana na binti kuwa tuachane ili nisije nikaharibu future yule binti akadai yeye akadai hawezi kuachana na mimi kwasababu hajawahi mjua mwanamume mwingine zaidi yangu tangu azaliwe. Na swala la yeye na mama yake anasema hawezi fanya chochote kwasababu yeye ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu. Nilimsihi tuendelee kwa siri ili nisije nikaharibikiwa kimasomo.

Mwezi uliopita mdada kanimaliza kabisa kaniambia anaujazito wangu, nimechoka mpaka sasa anasisitiza kuwa tunarudi wote Tanzania. Mwanzo nilijua ni utani lakini mpaka nimejua kuwa hatanii. Kwasababu ya urahisi jana Jumatatu nilimtuma yeye aende kunikatia ticket ya ndege amerudi na ticketi mbili yangu na ya kwake tunayosafiri pamoja.

Nimeshikwa na mfadhaiko, nimejaribu kumwambia tu kwa busara kwamba yeye angebaki kwanza ili nikafanye maandalizi ya kumpokea maana mimi nilipotoka nilikabidhi nyumba niliyokuwa naishi hivyo kwenda mahali na mgeni sina mahali pa kufikia itakuwa si vizuri.

Yeye amesisitiza kuna shida gani nikatapo lala naye atalala hata kama kibarazani. Pia akasema hawezi kuendelea kuwepo Korea maana ndugu zake wanaweza hata kumwambia atoe ujauzito wangu na pia wanaweza kumtenga ni heri akaondoka akaenda kuishi na mtu anayempenda hata kama ni sehemu ya tabu.

Kuhusu pesa yeye anasema sio shida anakiasi cha fedha ambazo ukizibadili zinaweza kufikia hadi 150 m ambazo zilikuwa ni mirathi ya marehemu baba yake. Kiukweli mdada huyu amenisaidia sana kifedha. Sikuwahi kuwa na shida ya kifedha muda wote nikiwa Korea.

Hofu yangu ni nyumbani ambako mke na watoto wangu wananingojea kwa hamu, nimeshindwa hata kuwanunulia zawadi maana huyu mdada anajua kila kitu ninachofanya. Ndani kwangu ni kama kwake. Jana nilipanga nimwambie ukweli lakini nilipokuwa namtazama nikajua anaweza nivuruga mpaka nikashindhwa kufanya mitihani yangu ya mwisho. Pia nilimwonea huruma sana kwamba naye anaweza asifanye vizuri hiyo mitihani yake. Ananipenda sana mpaka namuonea huruma sijui nikimwangalia.

Nilikuwa nafikiri nimwache wakati narudi nikifika Doha wakati wa kubadili ndege nimchenge potelea mbali hata kama nitakula hasara ya ticket. Lakini nimejikuta naona hiyo itakuwa ni kazi bure maana mdada huyu anajua mpaka ninapofanya kazi anwani yangu ya Tz anazo hata akaunti namba ya benki yangu anayo mana kuna wakati nikiwa likizo Tz alishawahi kunitumia pesa kwenye akaunti zangu.

Mke wangu na wanangu wananisubiria kwa hamu sana, na wanadai niwapelekee zawadi japo natoa kisingizio kwamba nimebakiwa na fedha ya nauli tu. Cha ajabu wife akasema basi atanitumia kwa Western Union mana kuna vitu nilishawahi kuwapelekea ni vizuri sana na vilikuwa vinauzwa bei ya chini sana. Huku mrembo wa kikorea naye anahesabu siku zilizobakia ili aweze kuruka nami kuja Tz.

Msaada wa kutatua tatizo hilo wadau. Niko njia panda nampenda mke wangu nawapenda wanangu. Namhurumia Mkorea alivyojitoa kwangu.

Nawasilisha kwa ajili ya ushauri.
Bro mimi sikushauri umtoroke kea namba yoyote ile,hili wazo futa kabisa kwani kila solution unayoitafuta mfikirie huyo mkorea.Mimi nakushauri face the problem head on,malizeni mitihani then mtafutie siku,mpeleke outing mahali halafu mweleze ukweli kuwa una mke na ulimdanganya kwakuwa ulikuwa unampenda,kuhusu maisha ya baadaye mwambie mfungue biashara korea na tanzania yeye abaki kuwa mke wa korea na wewe uwe unaenda huko na utaishi nae tu,baada ya miaka 2 mweleze mkeo kuwa umeoa korea,kwa njia hiii utawaokoa wske zako wote
 
Ila inauma eeh!!! Wengi mmemshauri amwambie mkewe ukweli kua anaoa mke mwingine yaani huyu Korea hamjawaza kua hata mke nae ataumia amelea familia toka 2014 akijua mmewe yuko masomoni
Leo fadhila yake kuletewa mke mwingine? Kweli? Wewe kaka bora hiyo ndege utakayopanda ipoteze mawasiliano huko angani familia italia weeee eeee baada ya
muda watazoea kuliko kuwaletea mke mwenza atayeleta ufa ktk hii familia.
Sijawahi kucheka wakati wa kilio, ila hii comment mamito ahaaaaaa
 
Wanaume kuweni na huruma basi, nikivaa kiatu cha mkewe nahisi kuzimia. Ukute anakusubiria na kwa uaminifu wote daah
 
Mkuu sikuweza kueleza kila kitu, ukweli ni kwamba huyu mdada alianza muda kusema kuwa nitarudi naye Tz mimi nikawa nadhani anatania. Tukawa tumefika muafaka kwamba mimi nitatangulia ili nimtengenezea mazingira ya yeye kuja Tanzania na pia ningemwalika kama business partiner ili apate visa hata ya miezi miwili kwanza lakini akija Tz atafanya process ya kuomba kuongezewa visa. Tukawa tumeelewana hivyo ndipo akaenda kufanya booking. Ajabu akarudi na akiwa amefanya booking mbili yangu na yake. Nikamuuliza kuhusu visa atafanyaje akasema hakuna shida anaomba kama mtalii na kesho ndo anaenda kwa wakala iliamtumie maombi yake ya visa kwenye ubalozi wa wetu ulioko Japan. Nataka nifanye mchezo kama nitapata mtu pale ubalozini aweke pending application yake.
Ukweli ni kwamba baada matatizo ndio nimegundua kuwa the girl is so smart.
Hivi ukimfikiria mkeo anaehangaika na familia kwa muda wote huo humwonei huruma???? Do something mkeo ataumia sana.
 
Sikiliza wewe kakate tiketi yako kwa pesa yako siku nyingine na ndege nyingine halafu mtoroke ila akikisha unamwandikia mail yenye ukweli wote kisha ama hapo ulipo nenda kapige shopping kwa ajili ya familia kisha unasepa kimya kimya. Hqkijua ukweli hawezi kukutafuta tena maana roho itamwingia nyongo na kama akikutafuta au akija Bongo ujue huyo kaja kukuua
Kidogo ukifanikiwa lakini kutoka
 
Hivi hawa wakorea si ndio kina JUMONG? na kina IRIS? Mkuu hilo unalo. Cha kufanya muandae rafiki yako wa Tz akuandalie nyumba mbali na kwako. Mwambie wife umeahirisha safari utamwambia ukiwa tayari, acha kuwasiliana na wife kwa muda. Njoo Tz ukifika jipange maisha mapya na mkorea. Baada ya Muda mpange sasa ili ajue A-Z.
Unazidisha matatizo
 
Hivi ukimfikiria mkeo anaehangaika na familia kwa muda wote huo humwonei huruma???? Do something mkeo ataumia sana.
Na hilo tu ndo limenifanya niache kazi zangu hapa nikawazaaa nikawazukaaa...nikaja na options 3 tofauti. Najua wamama wanavyopata shida wakiwa na watoto wadogo...kama atakaa chini na kuwaza vizuri, kutoroka ni solution ambayo itampa muda wa kujipanga akifika bongo lakini siyo kulazimisha waje naye. Aliondoka utawala ukiwa wa JK, arudi amkute JPM katunisha misuli, hela unapishana nayo inaelekea hazina, lazima ateme cheche.

Huyo Mkorea akiamua kuja basi atafika ameshajipanga vilivyo kuweza kumweka sehemu na familia yake isiparanganyike.
 
Wadau,

Nahitaji mchango wa mawazo yenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kisa chenyewe ni hivi mimi ni diaspora ambaye nipo Korea kimasomo tangu November 2014. Mwezi Juni 2016 nahitimu masomo. Nimeoa na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili.

Nikiwa huku Korea ya Kusini nilianza mahusiano na mdada wa kikorea, ni mrembo ila si wa kutisha sana si unajua watu wa ukanda huu kinachowapendezesha ni rangi tu waliyonayo vinginevyo kama wangelipakwa rangi nyeusi hakuna atakaye watamani.

Mdada huyu anajiheshimu sana tulianza kuzoeana kama classmate tu. Alikuwa karibu sana na mimi mpaka tukaanza kuvuka mipaka na kuwa wapenzi. Kosa nililofanya ni kwamba sikuwahi kumweleza ukweli kuhusu hali yangu ya ndoa, yaani nilimdanganya kwamba mimi sijaoa.

Tulianza mahusiano kwa siri kwasababu ya kuhofia jamaa zake wasijue kuwa anamahusiano na ngozi nyeusi. Ilifika wakati usiri ukawa unashindikana maana tulikuwa tunaenda club pamoja na kurudi na kulala aidha sehemu ninayoishi au anayoishi yeye. Kuna wakati mama yake aliwahi kuja juu sana akasema kwamba niachane na bintiye vinginevyo ataliwasilisha swala hilo polisi na ninaweza kufutiwa visa ya kuishi Korea.

Tulishauriana na binti kuwa tuachane ili nisije nikaharibu future yule binti akadai yeye akadai hawezi kuachana na mimi kwasababu hajawahi mjua mwanamume mwingine zaidi yangu tangu azaliwe. Na swala la yeye na mama yake anasema hawezi fanya chochote kwasababu yeye ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu. Nilimsihi tuendelee kwa siri ili nisije nikaharibikiwa kimasomo.

Mwezi uliopita mdada kanimaliza kabisa kaniambia anaujazito wangu, nimechoka mpaka sasa anasisitiza kuwa tunarudi wote Tanzania. Mwanzo nilijua ni utani lakini mpaka nimejua kuwa hatanii. Kwasababu ya urahisi jana Jumatatu nilimtuma yeye aende kunikatia ticket ya ndege amerudi na ticketi mbili yangu na ya kwake tunayosafiri pamoja.

Nimeshikwa na mfadhaiko, nimejaribu kumwambia tu kwa busara kwamba yeye angebaki kwanza ili nikafanye maandalizi ya kumpokea maana mimi nilipotoka nilikabidhi nyumba niliyokuwa naishi hivyo kwenda mahali na mgeni sina mahali pa kufikia itakuwa si vizuri.

Yeye amesisitiza kuna shida gani nikatapo lala naye atalala hata kama kibarazani. Pia akasema hawezi kuendelea kuwepo Korea maana ndugu zake wanaweza hata kumwambia atoe ujauzito wangu na pia wanaweza kumtenga ni heri akaondoka akaenda kuishi na mtu anayempenda hata kama ni sehemu ya tabu.

Kuhusu pesa yeye anasema sio shida anakiasi cha fedha ambazo ukizibadili zinaweza kufikia hadi 150 m ambazo zilikuwa ni mirathi ya marehemu baba yake. Kiukweli mdada huyu amenisaidia sana kifedha. Sikuwahi kuwa na shida ya kifedha muda wote nikiwa Korea.

Hofu yangu ni nyumbani ambako mke na watoto wangu wananingojea kwa hamu, nimeshindwa hata kuwanunulia zawadi maana huyu mdada anajua kila kitu ninachofanya. Ndani kwangu ni kama kwake. Jana nilipanga nimwambie ukweli lakini nilipokuwa namtazama nikajua anaweza nivuruga mpaka nikashindhwa kufanya mitihani yangu ya mwisho. Pia nilimwonea huruma sana kwamba naye anaweza asifanye vizuri hiyo mitihani yake. Ananipenda sana mpaka namuonea huruma sijui nikimwangalia.

Nilikuwa nafikiri nimwache wakati narudi nikifika Doha wakati wa kubadili ndege nimchenge potelea mbali hata kama nitakula hasara ya ticket. Lakini nimejikuta naona hiyo itakuwa ni kazi bure maana mdada huyu anajua mpaka ninapofanya kazi anwani yangu ya Tz anazo hata akaunti namba ya benki yangu anayo mana kuna wakati nikiwa likizo Tz alishawahi kunitumia pesa kwenye akaunti zangu.

Mke wangu na wanangu wananisubiria kwa hamu sana, na wanadai niwapelekee zawadi japo natoa kisingizio kwamba nimebakiwa na fedha ya nauli tu. Cha ajabu wife akasema basi atanitumia kwa Western Union mana kuna vitu nilishawahi kuwapelekea ni vizuri sana na vilikuwa vinauzwa bei ya chini sana. Huku mrembo wa kikorea naye anahesabu siku zilizobakia ili aweze kuruka nami kuja Tz.

Msaada wa kutatua tatizo hilo wadau. Niko njia panda nampenda mke wangu nawapenda wanangu. Namhurumia Mkorea alivyojitoa kwangu.

Nawasilisha kwa ajili ya ushauri.
Fanya uwezavyo umtupe huko huko Korea ukija nae mpaka bongo unazidi kuongeza matatizo
 
Wanaume kuweni na huruma basi, nikivaa kiatu cha mkewe nahisi kuzimia. Ukute anakusubiria na kwa uaminifu wote daah

Vip kama hata mke wake nae huku home ana njia zake za pembeni...?
 
Safirisha vitu kabla kwa ndege kabla siku hazijaisha mwambie unatanguliza vitu nyumbani ili mkiondoka msiwe na mizigo ataingia king. Usiache kitu chako ulichoangaikia huku bongo Magu kabana sana
si bure wewe hujawahi kupanda ndege
 
A
Wanaume kuweni na huruma basi, nikivaa kiatu cha mkewe nahisi kuzimia. Ukute anakusubiria na kwa uaminifu wote daah
Acha mimi nimeumia sana nilivyojaribu kuvaa kiatu cha mke.ndo maana nikasema bora hiyo ndege atakayopanda ipoteze tu mawasiliano uko angani.
Asifikiri laana itatolewa na mkorea tu hata huyu mkeo hakika atakupa laana tu.
 
Back
Top Bottom