Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Rudi nae Bongo waweke chini wake zako waeleze ukweli. Omba radhi. Hiyo ndo imani ya kikristo kaka. Hata MUNGU atakusamehe. Usiongeze dhambi zaidi kwa kumkimbia mkorea.
 
Nimelipenda hili wazo, nitalizingatia. Ila itabidi niache baadhi ya vitu vyangu ili asishitukie mapema.
Safirisha vitu kabla kwa ndege kabla siku hazijaisha mwambie unatanguliza vitu nyumbani ili mkiondoka msiwe na mizigo ataingia king. Usiache kitu chako ulichoangaikia huku bongo Magu kabana sana
 
Mkuu mwambie mkorea ukweli mwoneshe picha za watoto ..mke na harusi...usikilizie response yake......ukweli utakuweka huru
 
Dah kila nikisoma sielewi nikushauri nini ni kama umeamua kukomesha washauri, kama mwalimu anayetoa swali gumu lisilo na jibu. Tukisema uwambie mke+mchepuko au mmoja wapo bado ni full varangati, tukisema usiwambie wote bado ni full varangati, ushauri pekee ni wewe kuombea hiyo ndege ipotelee angani kama ambavyo huwa tunaombe ardhi ipasuke tunapokutwa na jambo la aibu ya karne.
 
Patamu hapo! Ongea na wazazi wako, uwaambie ukweli, then waambie wafanye mbinu wachukue watoto! Telekeza mke, chukua watoto kwa wazazi wako, then mdanganye Mkorea kuwa hao ni watoto wa KAKA yako marehemu, unawalea. Period

Wanawake wa kibongo hawana dhamana...!
 
Labda Malaya wanaojiuza
Umefika Korea Kusini mkuu? wanawake wa huku wako very charming sana muda wote wanatabasamu. Unaweza kuwa unaongea nao wanakujibu kawaida vizuri tabu huwa ni lugha tu wengi kingereza wanapata shida. Wako free sana binti kukutembelea chumbani si jambo la ajabu. Kama ni mwepesi unaweza ukabaka maana yeye kuja chumbani unaweza kudhani kuwa ameelekea kibra. Wao kwa wao wanaishi maisha ya kujirusha sana, hata mzungu anaweza kuja leo kisha akachukua mrembo hayo nimeyaona. Ngozi nyeusi huku japo hawatuambii waziwazi utajitambua tu kuwa wewe uko daraja lipi. Mara nyingi sana nimewahi kuona mrembo wa kikorea amekumbatiana na mzungu au na mkorea mwenzake huku wakitembea barabarani mchana kweupe, lakini huwezi kuona mweusi anatamba na mkorea ila tunawagonga kwa siri sana. Huyu yeye sana alikuwa amevuka mipaka hawezi kufanya siri. Ni mimi tu huwa namlazimisha iwe siri kwa ajili ya usalama wangu. Anataka twende beach, sehemu mbalimbali.
 
Yaani sasa hivi count kwamba una wake wawili na mtoto mwingine ambaye hajazaliwa!!!

Ninachojua ni kwamba mpaka mwanaume anafikia hatua ya kuomba ushauri ujue tayari ameshafanya maamuzi hivyo anataka kujiridhisha tu.
 
huu uboya kabisa ndio mnafanya tuonekane race ya ovyo....sa ya mimi hayo ya kumdanganya mtu aliyejitoa nakukupenda....bora ungemuambia una familia angejua cha kufanya ...umemdanganya huna mke mwisho ujauzito na mtu ameweka matumaini kwako.....hapo ngumu kumeza...mchukue tu maana huko kwao hujui balaa gani linaeza kukukuta kutoka na mapingamizi ya ndugu zao...af ugenini sio ukiharibu ishu
 
Yaani sasa hivi count kwamba una wake wawili na mtoto mwingine ambaye hajazaliwa!!!

Ninachojua ni kwamba mpaka mwanaume anafikia hatua ya kuomba ushauri ujue tayari ameshafanya maamuzi hivyo anataka kujiridhisha tu.
Kweli mkuu nilikuwa nimefikia maamuzi fulani lakini comment za wadau humu zinanipa mwanga kiasi kwamba ule uamuzi niliokuwa nimepanga awali nimeuona haufai. Bado naendelea kupokea comment maadamu bado nina muda. Muda muafaka ukifika nitafanya maamuzi kwa kuzingatia ushauri nilioupata.
Ukweli ni kwamba sijutii kufungua uzi huu japo wengine wamenikejeli, wengine wameniona mwongo yote nasema ni ya heri, maana kwa kosa hili pamoja na kejeli za wadau nimejifunza jambo kubwa sana.
 
Wadau,

Nahitaji mchango wa mawazo yenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kisa chenyewe ni hivi mimi ni diaspora ambaye nipo Korea kimasomo tangu November 2014. Mwezi Juni 2016 nahitimu masomo. Nimeoa na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili.

Nikiwa huku Korea ya Kusini nilianza mahusiano na mdada wa kikorea, ni mrembo ila si wa kutisha sana si unajua watu wa ukanda huu kinachowapendezesha ni rangi tu waliyonayo vinginevyo kama wangelipakwa rangi nyeusi hakuna atakaye watamani.

Mdada huyu anajiheshimu sana tulianza kuzoeana kama classmate tu. Alikuwa karibu sana na mimi mpaka tukaanza kuvuka mipaka na kuwa wapenzi. Kosa nililofanya ni kwamba sikuwahi kumweleza ukweli kuhusu hali yangu ya ndoa, yaani nilimdanganya kwamba mimi sijaoa.

Tulianza mahusiano kwa siri kwasababu ya kuhofia jamaa zake wasijue kuwa anamahusiano na ngozi nyeusi. Ilifika wakati usiri ukawa unashindikana maana tulikuwa tunaenda club pamoja na kurudi na kulala aidha sehemu ninayoishi au anayoishi yeye. Kuna wakati mama yake aliwahi kuja juu sana akasema kwamba niachane na bintiye vinginevyo ataliwasilisha swala hilo polisi na ninaweza kufutiwa visa ya kuishi Korea.

Tulishauriana na binti kuwa tuachane ili nisije nikaharibu future yule binti akadai yeye akadai hawezi kuachana na mimi kwasababu hajawahi mjua mwanamume mwingine zaidi yangu tangu azaliwe. Na swala la yeye na mama yake anasema hawezi fanya chochote kwasababu yeye ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu. Nilimsihi tuendelee kwa siri ili nisije nikaharibikiwa kimasomo.

Mwezi uliopita mdada kanimaliza kabisa kaniambia anaujazito wangu, nimechoka mpaka sasa anasisitiza kuwa tunarudi wote Tanzania. Mwanzo nilijua ni utani lakini mpaka nimejua kuwa hatanii. Kwasababu ya urahisi jana Jumatatu nilimtuma yeye aende kunikatia ticket ya ndege amerudi na ticketi mbili yangu na ya kwake tunayosafiri pamoja.

Nimeshikwa na mfadhaiko, nimejaribu kumwambia tu kwa busara kwamba yeye angebaki kwanza ili nikafanye maandalizi ya kumpokea maana mimi nilipotoka nilikabidhi nyumba niliyokuwa naishi hivyo kwenda mahali na mgeni sina mahali pa kufikia itakuwa si vizuri.

Yeye amesisitiza kuna shida gani nikatapo lala naye atalala hata kama kibarazani. Pia akasema hawezi kuendelea kuwepo Korea maana ndugu zake wanaweza hata kumwambia atoe ujauzito wangu na pia wanaweza kumtenga ni heri akaondoka akaenda kuishi na mtu anayempenda hata kama ni sehemu ya tabu.

Kuhusu pesa yeye anasema sio shida anakiasi cha fedha ambazo ukizibadili zinaweza kufikia hadi 150 m ambazo zilikuwa ni mirathi ya marehemu baba yake. Kiukweli mdada huyu amenisaidia sana kifedha. Sikuwahi kuwa na shida ya kifedha muda wote nikiwa Korea.

Hofu yangu ni nyumbani ambako mke na watoto wangu wananingojea kwa hamu, nimeshindwa hata kuwanunulia zawadi maana huyu mdada anajua kila kitu ninachofanya. Ndani kwangu ni kama kwake. Jana nilipanga nimwambie ukweli lakini nilipokuwa namtazama nikajua anaweza nivuruga mpaka nikashindhwa kufanya mitihani yangu ya mwisho. Pia nilimwonea huruma sana kwamba naye anaweza asifanye vizuri hiyo mitihani yake. Ananipenda sana mpaka namuonea huruma sijui nikimwangalia.

Nilikuwa nafikiri nimwache wakati narudi nikifika Doha wakati wa kubadili ndege nimchenge potelea mbali hata kama nitakula hasara ya ticket. Lakini nimejikuta naona hiyo itakuwa ni kazi bure maana mdada huyu anajua mpaka ninapofanya kazi anwani yangu ya Tz anazo hata akaunti namba ya benki yangu anayo mana kuna wakati nikiwa likizo Tz alishawahi kunitumia pesa kwenye akaunti zangu.

Mke wangu na wanangu wananisubiria kwa hamu sana, na wanadai niwapelekee zawadi japo natoa kisingizio kwamba nimebakiwa na fedha ya nauli tu. Cha ajabu wife akasema basi atanitumia kwa Western Union mana kuna vitu nilishawahi kuwapelekea ni vizuri sana na vilikuwa vinauzwa bei ya chini sana. Huku mrembo wa kikorea naye anahesabu siku zilizobakia ili aweze kuruka nami kuja Tz.

Msaada wa kutatua tatizo hilo wadau. Niko njia panda nampenda mke wangu nawapenda wanangu. Namhurumia Mkorea alivyojitoa kwangu.

Nawasilisha kwa ajili ya ushauri.
UMELIKOROGA MWENYEWE NA UTALINYWA MWENYEWE
 
Kunamtu kakushauri ujiue wakose wote.mi naunga mkono hoja yake au we unasemaje?
 
Korea ipi Seoul au Pyongyang? Kama ni kwa bwamdogo Kim jisalimishe kwenye vyombo vya usalama mwenyewe kabla hujakabidhiwa kwenye executed machine.
 
Ninachojua ni kwamba mpaka mwanaume anafikia hatua ya kuomba ushauri ujue tayari ameshafanya maamuzi hivyo anataka kujiridhisha tu.
hahahah..kwa muono wako..kashachukua yapi?
 
Back
Top Bottom