Mchepuko anataka anizalie mtoto

Mchepuko anataka anizalie mtoto

Mkuu acha iyo kitu itakuja ikukosti mbeleni huko isitoshe mungu kakujalia kid 3 sasa unataka uzae nnje hili iweje kama kungekuwa na sababu sawa wewe inachotakiwa kufanya kula mzigo jiondokee
Uko sahihi mkuu,tatizo anataka aweke kambi kabisa hata kama hatoishi kwangu
 
Kuwa na msimamo usipelekeshwe kirahisi hivyo na mwanamke.

Asilimia kubwa akili zao haziwatoshi. Wala hawajali matokeo yake hao. Leo na kesho utakuja kujuta kwa kitendo hiko.
Shukuru Mungu kwa sasa kama ndoa yako ina amani,angalia wewe ndie usije ukawa chanzo cha kutoelewana na mke wako.
Otherwise muoe ndio uzae nae.
 
Du ukijisikia kwenda kujisaidia utuambie pia tukushauri.iz nyuzi nazo za ki mihemko mkuu
 
Kuwa na msimamo usipelekeshwe kirahisi hivyo na mwanamke.

Asilimia kubwa akili zao haziwatoshi. Wala hawajali matokeo yake hao. Leo na kesho utakuja kujuta kwa kitendo hiko.
Shukuru Mungu kwa sasa kama ndoa yako ina amani,angalia wewe ndie usije ukawa chanzo cha kutoelewana na mke wako.
Otherwise muoe ndio uzae nae.
Mkuu ningefanya hivyo,ila mi ni mkiristo
 
Watoto mkeo anauwezo wa kuzaa! Huyo binti miaka 27 sio ya kutaka kuzaa na mume wa mtu!
Madhara hutayaona sasa hivi ni huko baadae akuite saa saba usiku mtoto anaumwa!

Usiiweke ndoa yako pabaya sababu ya mihemko!
Ni kweli mkuu,hata kama nitaazimia kufanya hivyo nitamtafutia eneo akaishi mkoa mwingine ili niwe naye mbali.
 
ha ha ha ha ha,haya mambo huwa yanawakuta wengi tu
Ni kweli mkuu ila sio kila kitu Jf watakupa ushauri.Hauna marafiki unaowaamini,ndugu jamaa unaofanya nao kazi.shida ya hapa mawazo wanakupa mengi utashindwa kuchuja.some issues its confidentiality.unafikili sasa hayatupati?.Yapo ila tuna namna ya kuyakabili coz we have relatives at our community
 
Ni kweli mkuu,hata kama nitaazimia kufanya hivyo nitamtafutia eneo akaishi mkoa mwingine ili niwe naye mbali.
Hata kuwa nae mbali sio suluhisho, achana na hayo mawazo yako ya kuzaa na mchepuko! Gharama yake ni kubwa sana, kumbuka hakuna siri ya wawili. Itaondoa imani yote kwa mkeo, na huo ndo utakuwa mwanzo wa familia ya ugomvi na visasi
 
Nimekuelewa mkuu,ngoja nipunguze mawasiliano...
 
Back
Top Bottom