Mchepuko anataka anizalie mtoto

Mchepuko anataka anizalie mtoto

Ni kweli mkuu,mbaya zaidi amekuwa akiniita mume badala ya mpenzi

Teh teh hahahahaa. Nacheka mkuu jinsi anavyokubembeleza na kukuita mume. Ila hajakosea kwa vile mmeshakuwa mwili mmoja. Hebu fikiria mahusiano yenu sasa sio ya zero distance ni NEGATIVE distance. Yaani mmegusana miili hadi mkapilitiza kwa kuingiziana mizamo.

Ila tambua hilo neno analotamka yaani MME ana maanisha kwa hiyo fanya uamuzi ukijua hilo na kwamba una wake wawili.

Pia umenikumbusha hili andiko rafiki....
1 Wakorintho 6:12 -20

12. Kila kitu ni halali kwangu,”lakini si kila kitu kina faida. “Kila kitu ni halali kwangu,”lakini sitatawaliwa na chochote. 13 “Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula,” lakini Mungu ataviharibu vyote viwili. Mwili wa mwanadamu haukuumbwa kwa ajili ya zinaa bali kwa ajili ya Bwana, na Bwana kwa ajili ya mwili.
14 Mungu alimfufua Bwana na atatufufua na sisi pia kwa uwezo wake. 15 Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni sehemu ya Kristo? Je, naweza kuchukua sehemu ya mwili wa Kristo na kuiunganisha na mwili wa kahaba? Hata kidogo! 16 Hamjui kwamba mtu aushirikishaye mwili wake na kahaba ana kuwa mmoja naye kimwili? Maandiko yanasema, “Hao wawili watakuwa mwili mmoja.” 17 Lakini mtu anayejiunga na Bwana ana kuwa mmoja naye kiroho.
18 Kimbieni dhambi ya zinaa. Dhambi nyingine zote anazotenda mwanadamu hufanyika nje ya mwili wake, lakini anayezini, ana tenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 Hamjui kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu anayekaa ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe; 20 mmenunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
 
Don't try this at home or anywhere kama unataka usalama wa ndoa yako. Yaani hapo ubongo wake unafanya kazi 100% na anajua anachokitafuta. Ila ubongo wako uko 0% kiutendaji kwa sasa na huoni mbele na ni hali ambayo inawatokea wanaume tulio wengi hasa tukiwa tunaona shimo mbele yetu. Ubongo hugoma kazi na kutoweza kupambanua mambo kwa umakini. Zinduka mkuu. Haijawahi tokea mtu akabaki salama kwenye hili jaribu kufuatilia.
 
Watoto mkeo anauwezo wa kuzaa! Huyo binti miaka 27 sio ya kutaka kuzaa na mume wa mtu!
Madhara hutayaona sasa hivi ni huko baadae akuite saa saba usiku mtoto anaumwa!

Usiiweke ndoa yako pabaya sababu ya mihemko!
 
Kabla ya 6 kwa 6 mbona hukuandika uzi tukushauri? Kama hutaki akuzalie basi mzalie wewe
 
Katika harakati zangu za hapa na pale,nilikutana na dada mmoja 27yrs ambaye kimuonekano alinivutia sana.Nikatafuta namna ya kuzungumza naye,na nikamuambia kiutani kama ningekuwa single ningemchukua yeye;yeye alicheka tu akasema haina shida tuwe tunabadilishana mawazo tu na tukapeana namba.
Baada ya kama wiki moja hivi aliomba nimthibitishie kweli kuwa nina familia kwa picha,nami nilifanya hivyo tukaendelea kuwasiliana.
Kuna siku aliomba tukutane tujadili mambo ya biashara za hapa na pale,na nilifanya hivyo..baada ya hapo tukawa tunakula na kunywa,na kilichofuata baada ya hapo ni 6 kwa 6.
Sasa anaomba nizae nae angalau mtoto 1 na ananiahidi hawezi kuingilia familia yangu ili mradi tu nimlee huyo mtoto atakayezaliwa.
Nipo njia panda nikiwa na wasi wasi kuwa nikifanya hivyo mambo yanaweza yakabadilika huko mbeleni; nipeni ushauri wakuu,ingawa napenda watoto ila sipendi shari.
Kiongozi janga hilo..
Hayo aliyoyasema kwamba hataingilia familia yako ni maneno tu ya kawaida... SIKU AKIZAA NDO UTAJUA

ACHANA NAYE, ACHIA MBALI KUZAA NAYE
 
Mkuu acha iyo kitu itakuja ikukosti mbeleni huko isitoshe mungu kakujalia kid 3 sasa unataka uzae nnje hili iweje kama kungekuwa na sababu sawa wewe inachotakiwa kufanya kula mzigo jiondokee
 
Katika harakati zangu za hapa na pale,nilikutana na dada mmoja 27yrs ambaye kimuonekano alinivutia sana.Nikatafuta namna ya kuzungumza naye,na nikamuambia kiutani kama ningekuwa single ningemchukua yeye;yeye alicheka tu akasema haina shida tuwe tunabadilishana mawazo tu na tukapeana namba.
Baada ya kama wiki moja hivi aliomba nimthibitishie kweli kuwa nina familia kwa picha,nami nilifanya hivyo tukaendelea kuwasiliana.
Kuna siku aliomba tukutane tujadili mambo ya biashara za hapa na pale,na nilifanya hivyo..baada ya hapo tukawa tunakula na kunywa,na kilichofuata baada ya hapo ni 6 kwa 6.
Sasa anaomba nizae nae angalau mtoto 1 na ananiahidi hawezi kuingilia familia yangu ili mradi tu nimlee huyo mtoto atakayezaliwa.
Nipo njia panda nikiwa na wasi wasi kuwa nikifanya hivyo mambo yanaweza yakabadilika huko mbeleni; nipeni ushauri wakuu,ingawa napenda watoto ila sipendi shari.
We kenge wahed kweli.Zaa naye uje uone kama anayoyasema ni ya kweli.Atafanya kila njia ili mkeo ajue.Ni wajinga sana wa HIVYO.We piga mti ulale mbele.Umzalie ili iweje?Mkeo ni tasa?Maneno matatu tu kwako yanakufaa"acha upumbavu wako"

Alishachakazwa na kila aina ya mikuyenge,sasa anataka akupate jinga wewe usiye na akili ili apunguze stress zake.

Tusipotoshane.
 
Sio tasa mkuu 3 kids,ndio maana naona maamuzi yanakuwa magumu.
Au mkeo kakuzalia watoto wa jinsia moja tu?Kwa hiyo unataka akuzalie wa jinsia nyingine?

Mkeo nao anapambana apate kidume ili abahatishe Mtoto wa jinsia nyingine.Kwa hiyo wewe na mkeo ngoma droo.

Haya mkazane kusaka mtafanikiwa tu watoto wa jinsia tofauti.

Wajinga wajinga tunawapa ushauri kama huu.

Hahahahaha, sikupotoshi.
 
Katika harakati zangu za hapa na pale,nilikutana na dada mmoja 27yrs ambaye kimuonekano alinivutia sana.Nikatafuta namna ya kuzungumza naye,na nikamuambia kiutani kama ningekuwa single ningemchukua yeye;yeye alicheka tu akasema haina shida tuwe tunabadilishana mawazo tu na tukapeana namba.
Baada ya kama wiki moja hivi aliomba nimthibitishie kweli kuwa nina familia kwa picha,nami nilifanya hivyo tukaendelea kuwasiliana.
Kuna siku aliomba tukutane tujadili mambo ya biashara za hapa na pale,na nilifanya hivyo..baada ya hapo tukawa tunakula na kunywa,na kilichofuata baada ya hapo ni 6 kwa 6.
Sasa anaomba nizae nae angalau mtoto 1 na ananiahidi hawezi kuingilia familia yangu ili mradi tu nimlee huyo mtoto atakayezaliwa.
Nipo njia panda nikiwa na wasi wasi kuwa nikifanya hivyo mambo yanaweza yakabadilika huko mbeleni; nipeni ushauri wakuu,ingawa napenda watoto ila sipendi shari.
Lazima uwe na malengo maishani.
Kwani una mpango wa kuwa na watoto wangapi? Unawazaa na nani?

Unaruhusuje mambo yanayotokea ghafla kushape future yako na familia..?
 
Maisha ya mtu kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya maamuzi tunayofanya kila siku....

Kama unataka kuja kuwa zombie wa mahusiano na kupoteza dira ya maisha basi jaribu kuzaa nae. Hukupaswa kuweka nae mazoea kiasi hicho....

Karma is real usishangae na wewe katika hao watoto wa3 kuna ambao wewe sio biological father....malipo ni hapahapa.
Be smart, usitake starehe za muda mfupi zi define future yako yote.
 
Back
Top Bottom