KERO Mchango wa Lazima wa Mwenge ni kero

KERO Mchango wa Lazima wa Mwenge ni kero

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hii kitu inafaa walimu tu ndo wakatwe.
 
Acha upuuzi wew leo utaambiwa elfu tano mwakan utaambiwa elfu kumi na tano Kwasababu ya ujinga wa kutokuhoji mambo kwa undani, hawa watumishi wanakatwa mishahara yao inamaana hayo makato bado hayatoshi kuendeshea hzo shughuli zao.
Hata ingekuwa sh 100 ila siyo ichukuliwe kizembe.

Ndiyo hivyo hivyo mafisadi yanaiba, wanakuambia wakata tozo ya sh 50 tu kumbe wakijumlisha ni mamilioni
 
sisi watumishi wa Hospital ya mji kondoa tuna lazimishwa kuchangia mchango wa mwenge shilingi 5,000/= kwa kila mtumishi kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Mji Kondoa.

Mfano, Tarehe 07/05/2026 tumepewa posho za masaa ya ziada ila wametukata kwa lazima mchango wa mwenge tulipo uliza tumejibiwa ni maelekozo kutoka kwa Mganga mfawidhi na kama hautaki kukatwa basi uache kazi.

Tunaonekana kama ni wapinga kristo kwenye mamlaka hali hii huwa ni kila mwaka inapofika kipindi cha mwenge. Mwaka jana ilikuwa 3,000/=, mwaka huu ni 5,000/=.

Soma Pia: Mtendaji wa kata kunichangisha mchango wa mwenge kwa lazima imekaaje hii?

Inatuumiza sana, naomba mtusaidie kupaza sauti kwa mamlaka zinazohusika

View attachment 3585505
Siku mwenge ukifika kanywe bia nne ufidie mchango wako/bia Tsh.1250×4=5000 kwa bei bila tozo).Ukitaka kula,kubali uliwe kidogo.
 
Ukiwa junior staff hulazimishwi kutoa.ila ukiwa in charge na unakitakia wema cheo chako lazima utoe..na sare za mwenge ushone, Na kukesha ukeshe
 
Back
Top Bottom