Mnakumbuka last time ktk BUNGE alikuwa anapiga nyundo kisha TBC wakazima mitambo?
Mnyika akiingia bungeni tutakuwa na nyongeza ya wawakilishi makini
Serikali na Watanzania itambue kuwa hawa wanaowaita wapinzani si wapinzani wa maendeleo bali ni fikra mbadala kwa kuendeleza gurudumu la maendeleo na ustawi wa nchi yetu mbele.
Ninawaunga mkono wapinzani makini yes.
Basi inawezekana waliokata matangazo sio TBC bali king'amuzi, kama unauhakika uliisikia hotuba ya Dr. Slaa mwanzo-mwisho, then ni kingamuzi changu, naiomba msamaha TBC , na kwa niaba ya wale wote walioilaumu.labda ilikata maramoja na kurudi wakati anaanza, kwani mimi nimeisikiliza sehemu kubwa ya hotuba hiyo kwenye TBC mpaka anamaliza mida ya mchana hivi.
ilikuwa nzuri sana na alionyesha kipengele kwa kipengele namna serikali isivyokuwa makini kwenye maeneo mbalimbali. Thanks Invincible kwa kutupa doc nzima
Basi inawezekana waliokata matangazo sio TBC bali king'amuzi, kama unauhakika uliisikia hotuba ya Dr. Slaa mwanzo-mwisho, then ni kingamuzi changu, naiomba msamaha TBC , na kwa niaba ya wale wote walioilaumu.
Wakuu,
Jamani mmeweza kuupitia mchango wa Dr. Slaa vizuri?...
Nimewahi kuwaambia kwama Mkapa alivurunda kabisa ktk Ukusanyaji wa kodi na Ukimsoma Dr.Dlaa toka kifungu cha 39 mtachoka wenyewe... Yaani Serikali inakusanya kodi zake toka Wafanyabishara wasiozidi 570,000 (wenye TIN) na kati ya hawa asilimia 75 wanatoka Dar es Salaam kisha kodi ya Wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi wasiozidi 1,000,000.
Duh! yaani nchi nzima wananchi walipa kodi hawafiki millioni 2 na hawa ndo wanabeba mzigo woote - I knew something was very wrong!
Je, hii kweli inaonyesha ufanisi ktk muundo wa kukusanya kodi? Nambieni mnaosifia pengine kuna kitu sikuwahi kukiona...
1st post updated, tumepata nakala toka kwa Dr. Slaa
Katika mengi nimeshtushwa pia na serikali kununua samani kila mwaka.!!!!!! Nadhani itakuwa ni manunuzi hewa
Nimeisoma yote ni nzuri isiyo mfano.
Anatoa tafsiri hii kuhusu kilimo: Anasema mwaka 2009/2010 Wizara ya Kilimo ilitengewa Jumla ya Tshs 92,694,254,000 na mwaka 2010/2011 imetengewa Tshs 103,952,371,000.
Lakini mwaka 2009/2010 Dola ya Marekani ilikuwa inabadilishwa kwa $1= Tshs 1200, leo $ 1 ni sawa na Tshs 1,450 Hivyo uwezo na nguvu ya manunuzi ya Shillingi imeshuka kwa zaidi ya Tshs 250 hivyo kwa fedha hizo kazi unazofanya inaweza kufanana na zile za mwaka jana au hata chini ya hapo.
Kwa tafsiri rahisi budget ya kilimo imeongezeka kwa 11.2% lakini thamani ya pesa imeshuka kwa 12%. kwa maana hiyo budget ya kilimo kwanza ya mwaka huu purchasing power yake ni ndogo kuliko ya mwaka jana.
Point yake ni nzuri sana ingawa mfano huo wa viwango vya kubadilishia fedha ulioutoa hapo juu una kasoro. Kwa kifupi katika kipindi cha miaka miwili (2007 mpaka Nov 2009) uwezo wa manunuzi wa shilingi mia moja ulipungua hadi kufikia shilingi 87 ( takwimu hizi na grafu yake nilishaweka hapa wiki kadhaa zilizopita kipindi kile cha sakata la TUCTA na hizi ni takwimu ni za kutoka NBS).
Hoja za waheshimiwa kama Zitto na Slaa zinaonyesha ukomavu wa hali ya juu katika haya maswala ila tatizo ni hao wavivu wa CCM wanaojaza nafasi huko Bungeni. Bajeti hii ni busu la mauti.