Point yake ni nzuri sana ingawa mfano huo wa viwango vya kubadilishia fedha ulioutoa hapo juu una kasoro. Kwa kifupi katika kipindi cha miaka miwili (2007 mpaka Nov 2009) uwezo wa manunuzi wa shilingi mia moja ulipungua hadi kufikia shilingi 87 ( takwimu hizi na grafu yake nilishaweka hapa wiki kadhaa zilizopita kipindi kile cha sakata la TUCTA na hizi ni takwimu ni za kutoka NBS).
Hoja za waheshimiwa kama Zitto na Slaa zinaonyesha ukomavu wa hali ya juu katika haya maswala ila tatizo ni hao wavivu wa CCM wanaojaza nafasi huko Bungeni. Bajeti hii ni busu la mauti.