Naam, naam.
Nimejitahidi sana kusoma dini.Binafsi nyumbani kwa mzee wangu alipotokea ni kanisani. Kwa kuwa baba yake alikuwa mchungaji.
Kwa hivyo, yeye alikuwa si tu anaenda kanisani, bali aliishi kanisani.
Nimejitahidi kusoma Ukristo, Uislamu, Uyahudi, Uhindu, Ubuddha, na dini nyingine nyingi.
Dini kwa upande mmoja, ni kitu kizuri sana. Inarudisha watu kwenye mstari wa kuishi kwa upendo, kukataza mabaya, kuhimiza mema na kumtofautisha mtu na hayawani.
Upande huu wa dini naupenda sana.
Ila, pia, dini ina upande mwingine, mbaya. Wa kubaguana, kuona watu wa dini yako ndio wenye ukweli na wengine wapotofu, kuhalalisha mambo mabaya kwa kigezo cha dini, vita vya kidini, dini kutumika kama siasa, dini kutumika ku manipulate watu kwa uongo, dini kupinga maendeleo ya elimu na kudumaza fikra za watu kwa ujinga, na mambo kem kem kama hayo.
Kiukweli, dini ni nyenzo, kama moto.
Moto si mzuri wala mbaya. Moto upo tu.
Jinsi gani unautumia moto ndiyo inaweza kuwa nzuri au mbaya.
Unaweza kuutumi moto kupika chakula watu wakala wakashiba. Hapo moto umetumika vizuri.
Moto huo huo, unaweza kuutumia, ukaunguza nyumba, ukaua watu. Hapo moto umeutumia vibaya.
Vivyo hivyo kwenye dini.
Unaweza kutumia dini ukawaunganisha watu, ukapunguza uhalifu katika jamii. Hapo umeitumia dini vizuri.
Unaweza pia kutumia dini kuwagawanya watu, ukaanzisha vita ya kidini, watu wakauana kwa mamilioni. Hapo umeitumia dini vibaya.
Dini kama dini haina maana. Si mbaya wala nzuri. Maana ya dini unaipa wewe muumini.
Moto kama moto si mbaya au mzuri. Ubaya au uzuri wa moto unakuja kulingana na mtumiaji anavyoutumia.