Mchango wa Dini katika ustawi wa maisha ya Binadamu

Mchango wa Dini katika ustawi wa maisha ya Binadamu

Kijana kuendelea kujadiliana na mimi ni kujichimbia shimo. Swali langu liko wazi na halijamfunga niliye muuliza, maana yake hakuna jibu kinyume chake.

Imani ni kusadiki juu ya jambo fulani pasi na shaka yoyote na kufungamana na jambo hilo. Mathalani, ukana Mungu ni imani sababu wao wanaamini kwa sababu zao ya kuwa hakuna Mungu.

Kwa ziada ya matumizi ya tamko imani si tu katika Dini bali hata katika maisha ya kawaida tunalitumia tamko hili kinyume na imani za kidini, nakupa mfano, huwa kuna kauli zifuatazo katika jamii zetu.

1. Usimuamini Mwanasiasa. (Hapa tamko hili halijaja kwa munasaba wa dini bali kwa muktadha wa hali ya watu hao)

2. Watoto wa kike hawaaminiki (Kadhalika limetumika tamko imani kwa sifa yake).

Mifano iko mingi sana juu ya tamko hilo, kwahiyo narudia tena swali langu halikumfunga muulizwaji. Kwahiyo swali langu lilimili juu ya kile anachokiamini kile anacho kijua kile anacho ishi nacho kile alochofungamana nacho kuhusu chanzo cha ulimwengu na maisha.
hiyo ni fallacy of argumentum ad hominem, shambulia hoja usimshambulie mtoa hoja.

hiyo mifano uliyoiweka haijajibu swali langu hili "kwanini umsetie majibu ya swali yawe katika mfumo wa kiimani?"
 
Safi kabisa naelekea kukuthibitishia jambo hili, ila kuna vitu tuwekane sawa. Wewe Historia unayo irejea ni ipi na ilianza kuandikwa lini na nani ?

Dondoo kuhusu Ithibati ya mwezi kupasuka na nukta muhimu

1. Kwanza unatakiwa ujue ya kuwa tukio la kupasuka kwa mwezi ni tukio lililo hadithiwa na watu wengi kwa zama husika mpaka habari hii kutufikia sisi, katika istilahi za uhakiko wa habari hali hii ya masimulizi tunaiita "Mutawatir".

2. Tukio hili lilikuwa ni muujiza kwa wale walio mtaka mtume afanye muujiza ili wathibitishe ya liwa yeue ni mtume kweli.

3. Naweka kiporo nukta hii nitakapo kuja kukujibu juu ya marejeo yako ya Historia.

4. Siyo kwamba tukio limekaa mithili ya hadithi za Abuu Nawasi (Usahihi wa jina lake ni hili, na visa vyake si vya kweli kwa kumnasibishia yeye). Habari za Abuu Nawas zinaelezeka kielimu sababu sababu yeye amezuliwa habari hizo.
hapo hujathibitisha bali umeonesha shaka zaidi kwamba habari hizi zipo katika kundi la "hearsay" na hivyo ni ngumu sana kutosheleza kama ushahidi
 
Twende taratibu, nitalifanya baada ya wewe kujibu swali langu hapo juu, kwamba hicho ulichokiandika dhidi ya Dini yangu unaweza kukipinga kielimu ? Ukijibu ndiyo au hapana. Nathibitisha kisha narudi kwenye swali langu hili "Pinga kielimu".

Ithibati ya hicho ulichokitaka tunakipata katika Qur'aan na Hadithi za mtume wa Allah.
sasa hii ndio nini?

kwamba ni sahihi kukubali kila kitu unachoambiwa kua ni cha kweli endapo utashindwa kukipinga?

pointi yako ni nini hapa?
 
Dini husaidia sana indawa pia hltunazofata sasa nadhani zina utofauti mkubwa wa ufahamu kati ya sasa na kipindi kile cha yesu na muhammad.

Kwasasa dini ni alama ya unyonyaji. Wakati histotia za kale zinaonyrsha hizi dini za asili zilikuwa ni mifumo ya maisha kama vile ujamaa, ubepari nk.

Lkn kwasasa dini zipo kwa ajili ya kupumbaza na kunyonya wafuasi waliotengenezwa na wakapumbaa na kunyonywa
 
hiyo ni fallacy of argumentum ad hominem, shambulia hoja usimshambulie mtoa hoja.

hiyo mifano uliyoiweka haijajibu swali langu hili "kwanini umsetie majibu ya swali yawe katika mfumo wa kiimani?"
Sasa unataka nianze kukufundisha somo la Logic. Kauli niliyo kuambia ni uhalisia wa mambo na haihusiani na kiini cha hoja.

Hakuna Ad Hominem hapo, bali wewe sasa umetumia "Strawman arguments" kuleta swali lingine kwa kubabatiza kwenye hoja yangu. Yaani swali lako ni mfu na hoja yako kadhalika.

Nakukumbusha tu ya kuwa swali langu lilikiwa hivi "Unaamini nini juu ya chanzo cha ulimwengu na maisha". Tamko hilo kama mifano niliyo kuwekea huko nyuma halihusiani na imani kama sifa. Sasa unachotakiwa wewe uonyeshe ya kuwa mifano niliyo itoa inapingana na maana ya tamko kuamini katika swali nililo muuliza.

Fanya kazi hiyo, kusema bila kuonyesha udhaifu ni uoga ulio wazi kabisa.
 
hapo hujathibitisha bali umeonesha shaka zaidi kwamba habari hizi zipo katika kundi la "hearsay" na hivyo ni ngumu sana kutosheleza kama ushahidi
Kijana punguza kukurupuka, naposema naelekea kuthibitisha na kutoa dondoo ujue bado ithibati sijaweka, ila naweka utangulizi kupunguza maswali ya kipuuzi yasiwe mengi.

Kijana uwe unasoma kisha uelewe.
 
sasa hii ndio nini?

kwamba ni sahihi kukubali kila kitu unachoambiwa kua ni cha kweli endapo utashindwa kukipinga?

pointi yako ni nini hapa?
Kinyume chake utakuwa ni ubishi na utaishi katika ile kauli ya "Mimi sijui lakini hunidanganyi". Sasa ushakiri hujui vipi usidanganywe ?

Sasa utakataa vipi jambo la kielimu huku huna elimu ? Nionyeshe kwa namna gani hili linawezekana ? Naona mmefundishwa kuwa wabishi na kubebeshwa ujinga vichwani mwenu bila kutafakari
 
Unajinasuaje kutoka katika unyonyaji wa dini?
Dini husaidia sana indawa pia hltunazofata sasa nadhani zina utofauti mkubwa wa ufahamu kati ya sasa na kipindi kile cha yesu na muhammad.

Kwasasa dini ni alama ya unyonyaji. Wakati histotia za kale zinaonyrsha hizi dini za asili zilikuwa ni mifumo ya maisha kama vile ujamaa, ubepari nk.

Lkn kwasasa dini zipo kwa ajili ya kupumbaza na kunyonya wafuasi waliotengenezwa na wakapumbaa na kunyonywa
 
Sasa unataka nianze kukufundisha somo la Logic. Kauli niliyo kuambia ni uhalisia wa mambo na haihusiani na kiini cha hoja.

Hakuna Ad Hominem hapo, bali wewe sasa umetumia "Strawman arguments" kuleta swali lingine kwa kubabatiza kwenye hoja yangu. Yaani swali lako ni mfu na hoja yako kadhalika.

Nakukumbusha tu ya kuwa swali langu lilikiwa hivi "Unaamini nini juu ya chanzo cha ulimwengu na maisha". Tamko hilo kama mifano niliyo kuwekea huko nyuma halihusiani na imani kama sifa. Sasa unachotakiwa wewe uonyeshe ya kuwa mifano niliyo itoa inapingana na maana ya tamko kuamini katika swali nililo muuliza.

Fanya kazi hiyo, kusema bila kuonyesha udhaifu ni uoga ulio wazi kabisa.
kabla ya kunifundisha mimi kajifunze kutofautisha kwanza kati ya strawman arguments na fallacy of irrelevant, ulichokiandika hapa hakina uhusiano wowote na strawman fallacy.

1602087147143.png

hapa nakuonesha ulipoiacha hoja na kumshambulia mtoa hoja, because the personal character of an individual is logically irrelevant to the truth or falseness of the argument itself

sijapinga kua swali lako halikua hivyo. Nimejua liko hivyo na ndio maana nimekuuliza kwanini umsetie category ya jibu liwe katika msingi wa kiimani?
 
Kijana punguza kukurupuka, naposema naelekea kuthibitisha na kutoa dondoo ujue bado ithibati sijaweka, ila naweka utangulizi kupunguza maswali ya kipuuzi yasiwe mengi.

Kijana uwe unasoma kisha uelewe.
sasa hapo unanikosoa vipi kua siko sahihi kukuambia hujathibitisha wakati we mwenyewe umesema unaelekea kuthibitisha?

haya thibitisha
 
Kinyume chake utakuwa ni ubishi na utaishi katika ile kauli ya "Mimi sijui lakini hunidanganyi". Sasa ushakiri hujui vipi usidanganywe ?

Sasa utakataa vipi jambo la kielimu huku huna elimu ? Nionyeshe kwa namna gani hili linawezekana ? Naona mmefundishwa kuwa wabishi na kubebeshwa ujinga vichwani mwenu bila kutafakari
hakuna jambo la kielimu linalokuja kwa kuanza na "thibitisha hakipo", "pinga kielimu" au "kanusha hakipo"

hiyo ni elimu ya kindezi na ujinga
 
kabla ya kunifundisha mimi kajifunze kutofautisha kwanza kati ya strawman arguments na fallacy of irrelevant, ulichokiandika hapa hakina uhusiano wowote na strawman fallacy.

View attachment 1593287
hapa nakuonesha ulipoiacha hoja na kumshambulia mtoa hoja, because the personal character of an individual is logically irrelevant to the truth or falseness of the argument itself

sijapinga kua swali lako halikua hivyo. Nimejua liko hivyo na ndio maana nimekuuliza kwanini umsetie category ya jibu liwe katika msingi wa kiimani?
Jifunze kunukuu hoja kwa ukamilifu, nitakuuliza baada ya kukupa unachostahiki, vioi hoja yako sikuidhoofisha ?

Ad Hominem inahusu hoja nzima mwanzo mpaka mwisho. Nakuonyesha sasa ya kuwa wewe umejenga "Strawman Argument". Nilipo muuliza muulizwaji swali la "Je unaamini nini juu ya chanzo cha ulimwengu". Aidha kwa kutokujua kwako (Hili nina hakika zaidi) ukajenga hoja mfu juu ya kile nilicho uliza,kisha ukauliza "Kwanini nimemsetia niliye muuliza swali katika mlengo wa kiimani" (Au kama ulivyo andika). Hii ni hoja mfu ambayo kiuhalisia hailengi nilicho muuliza niliye muuliza, badala yake ukaunda swali ambalo kiuhalisia halipo ili kudhoofisha ni"icho kiandika. Mfano wa swali lako mfu (Strawman Argument) ni kama walimu wawili hawa :

Mwalimu A : Inabidi tuwawekee wanafunzi wetu ratiba nzuri na kuwafundisha kwa bidii ili wapate kufaulu vizuri masomo yao.

Kisha mwalimu B anajengs hoja mfu kwa mwalimu A ili adhoofishe hoja yake.

Kisha...
Mwalimu B : Hatuwezi kuruhusu A zipatikane kizembe zembe sisi.

Huu sasa ndiyo mfano wa "Strawman Argument" ambao unaukuta katika swali lako, yaani nauliza swali kulia unaleta hoja mfu kulazimisha ya kuwa nimekusudia kushoto.
 
sijapinga kua swali lako halikua hivyo. Nimejua liko hivyo na ndio maana nimekuuliza kwanini umsetie category ya jibu liwe katika msingi wa kiimani?
Sababu hoja imekushinda hii na unazidi kumili katika hoja mfu yako (Strawman Argument), nakuuliza swali ni imani gani kwayo nimemlengesha niliyemuuliza lile swali ? Je ni imani ya kidini au kinyume chake na kisha uthibitishe hilo.

Nimeamua kukufundisha sasa na kuuliza maswali ambayo kwa namna yoyote huwezi kutoka zaidi ya kujenga hoja ambazo ukiziweka katika kile nilicho kiandika hakikai.
 
sasa hapo unanikosoa vipi kua siko sahihi kukuambia hujathibitisha wakati we mwenyewe umesema unaelekea kuthibitisha?

haya thibitisha
Sasa kuthibitisha ni sawa na kuelekea kuthibitisha ?

Kijana hujawahi kuwa makini hasa unapojadiliana na mimi, punguza uoga na usome kile ninacho kiandika. Ajabu najaribu kukiandikia Kiswahili chepesi sana.

Suala la kuthibitisha naendelea nalo, kwa kufata mtiririko wa yule niliye anza naye, ndiyo maana nimeamua niende naye taratibu ili asije kuuliza maswali ya kipuuzi huko mbeleni na kunipotezea muda.Kwahiyo hapa namsubiri akija naendelea naye. (Fatilia hatua kwa hatua huu mjadala).
 
hakuna jambo la kielimu linalokuja kwa kuanza na "thibitisha hakipo", "pinga kielimu" au "kanusha hakipo"

hiyo ni elimu ya kindezi na ujinga
Nimecheka hivi, huwa unakihariri unachokiandika au unaandika ilimradi ?

Kijana unapoteza muda katika jambo ambalo liko wazi sana. Yaani laiti kama ungefikiria kwa umakini usingeandika jambo hili.

Fatilia kile kilicho fanya nikafikia hapo, sasa nitaanzaje kuandika "Pinga kielimu bila kutangulia na kile alichopinga yule aliye pinga ". Sasa kama hili dogo limekushinda kujia kama umepoteza muda vipi kuhusu hili la mada husika ?

Ulitakiwa ufate mtiririko mpaka ujue imekuwaje nikamwambia "Apinge kielimu" ,sababu kuna sehemu tumeanzia na pale ndiyo naelekea kuhitimisha hoja.

Kwa masikitiko makubwa kwa kukosa kwako umakini, unaendelea kuandika hoja mfu, yaani nianze tu kutoka pasi na kujulikana "Pinga kielimu ?". Swali litakuja nipinge nini ?
 
Jifunze kunukuu hoja kwa ukamilifu, nitakuuliza baada ya kukupa unachostahiki, vioi hoja yako sikuidhoofisha ?

Ad Hominem inahusu hoja nzima mwanzo mpaka mwisho. Nakuonyesha sasa ya kuwa wewe umejenga "Strawman Argument". Nilipo muuliza muulizwaji swali la "Je unaamini nini juu ya chanzo cha ulimwengu". Aidha kwa kutokujua kwako (Hili nina hakika zaidi) ukajenga hoja mfu juu ya kile nilicho uliza,kisha ukauliza "Kwanini nimemsetia niliye muuliza swali katika mlengo wa kiimani" (Au kama ulivyo andika). Hii ni hoja mfu ambayo kiuhalisia hailengi nilicho muuliza niliye muuliza, badala yake ukaunda swali ambalo kiuhalisia halipo ili kudhoofisha ni"icho kiandika. Mfano wa swali lako mfu (Strawman Argument) ni kama walimu wawili hawa :

Mwalimu A : Inabidi tuwawekee wanafunzi wetu ratiba nzuri na kuwafundisha kwa bidii ili wapate kufaulu vizuri masomo yao.

Kisha mwalimu B anajengs hoja mfu kwa mwalimu A ili adhoofishe hoja yake.

Kisha...
Mwalimu B : Hatuwezi kuruhusu A zipatikane kizembe zembe sisi.

Huu sasa ndiyo mfano wa "Strawman Argument" ambao unaukuta katika swali lako, yaani nauliza swali kulia unaleta hoja mfu kulazimisha ya kuwa nimekusudia kushoto.

kwanza sio kweli kwamba ad hominen inahusu hoja nzima mwanzo mpaka mwisho kama wewe unavyopotosha. Ad hominiem haigusi hoja bali ni shambulio binafsi (persnal attack) au ("Poisoning the Well") kumshambulia mpinzani aliyeleta hoja badala ya kujikita kuijadili hoja yenyewe.

Strawman inajihusisha katika disproving against opponent arguments kwa kuzidisha (misrepresented) maneno au kutia chumvi, yatakayo mpa urahisi mpinzani kurahisisha hoja za upande unaopinga kwa kum critique. Hizi ni hoja ambazo zinakua na conclusion inayo finalize kua opponent hayuko sahihi

Mara nyingi ni watu ambao wanakuwekea maneno mdomoni ambayo wewe hukuyasema wala kuyaandika kisha kupitia hayo hayo maneno waliyoweka wanaanza kutengeneza njama kukuonesha hoja yako ni potofu

Mfano ni huu, kumiliki silaha kwa ajili ya kujilinda ni jambo zuri

We unakuja kusema, aah sio kweli nina ushahidi katika hilo silaha zinatumiwa na majambazi kuua watu kila siku matukio ya kihalifu yanafanyika na watu wanaomiliki silaha hivyo umiliki wa silaha ni jambo la hatari na sio zuri

Sasa wewe umeuliza swali kua unaamini nini juu ya uwepo wa mbingu? Mimi nikaona swali lako umelilengesha kwenye majibu unayoyataka wewe umetengeneza hoja kwa kutumia assumption kwamba jibu lake ni lazima liwe katika imani pekee when actually seems there are several

Swali langu la mimi kukutaka wewe ufafanue kwanini ulitumia imani kama ndio nguzo ya kupewa jibu halipo kwenye strawman argument wala logical fallacy yeyote ile kwasababu kwanza swali langu linakutaka uinyambue hoja yako ieleweke vizuri.

Pili strawaman ina deal kwenye kupandikiza maneno ya uongo ambayo na kuhitimisha kua kilichodaiwa na opponent ni uongo.

Mimi sijakuzushia maneno ya uongo ambayo hujayaandika hapo, bali nimeuliza swali, sijahitimisha kwamba wewe ni muongo kwa ku twist maneno ambayo nimeyapachika ili kunipa urahisi wa ku-shut down hoja yako. Sasa hapo utasemaje swali langu linalokutaka ufafanue ulichokiuliza ni strawman argument?
 
Sababu hoja imekushinda hii na unazidi kumili katika hoja mfu yako (Strawman Argument), nakuuliza swali ni imani gani kwayo nimemlengesha niliyemuuliza lile swali ? Je ni imani ya kidini au kinyume chake na kisha uthibitishe hilo.

Nimeamua kukufundisha sasa na kuuliza maswali ambayo kwa namna yoyote huwezi kutoka zaidi ya kujenga hoja ambazo ukiziweka katika kile nilicho kiandika hakikai.
Usiniulize mimi habari za imani wakati mimi ndio nimeanza kukuuliza habari hizo hizo baada ya kuona umeandika kwenye post yako

Kwanini imani iwe ndio path ya kufikia jibu juu ya kile ulichokiuliza?

Kwanini ujisetie majibu kwenye njia hiyo?
 
Sasa wewe umeuliza swali kua unaamini nini juu ya uwepo wa mbingu?
Mzee naona unanichosha na kunipotezea muda.

Wapi nimeandika haya ? Kama una uwezo mdogo wa kumbukumbu na umakini, basi jaribu uwe una copy kisha una paste kile nilichokiandika.

Hayo mengine niliyo acha kuyanukuu hukutakiwa kuandika sababu nilicho kiandika juu ya "Strawman Argument" kimejitosheleza.
 
Usiniulize mimi habari za imani wakati mimi ndio nimeanza kukuuliza habari hizo hizo baada ya kuona umeandika kwenye post yako

Kwanini imani iwe ndio path ya kufikia jibu juu ya kile ulichokiuliza?

Kwanini ujisetie majibu kwenye njia hiyo?
Nawajibika nikuulize wewe sababu ukichokiandika siyo kile nilichokiandika mimi. Yaani wewe umeleta lako ndiyo maana unakimbia swali nililo kuuliza.

Sababu nilikupa na mifano miwili juu ya tamko tena kwa munasaba hasa, ambao huwezi kuukanusha kwa hoja zaidi ya kubisha na kupotea.

Swali langu ni "Una amini nini juu ya chanzo cha ulimwengu na maisha" ? Hili swali liko wazi sana. Swali linamtaka muulizwaji aseme kile anakisadiki juu ya chanzo cha ulimwengu kile anacho kiamini kile anacho kijua. Ndiyo maana nikikupa miaka kumo ukosoe ile mifano kwa swalo langu huwezi zaidi ya kusema "mifabo haijajibu swali lako" . Kijana ongeza umakini.
 
Back
Top Bottom