Mchango wa Dini katika ustawi wa maisha ya Binadamu

Mchango wa Dini katika ustawi wa maisha ya Binadamu

Naam, naam.

Nimejitahidi sana kusoma dini.Binafsi nyumbani kwa mzee wangu alipotokea ni kanisani. Kwa kuwa baba yake alikuwa mchungaji.
Kwa hivyo, yeye alikuwa si tu anaenda kanisani, bali aliishi kanisani...

Nakubaliana na uliyoyasema, na kwa mtazamo wangu, ili dini itumike vizuri ni lazima wale wanaoitumia wawe na upeo fulani wa uelewa, na kiwango fulani cha maendeleo.

Mimi hua nafananisha dini na filosofia zingine kama vile "demokrasia". Kwa watu wenye upeo mdogo, dini lazima itazusha mikingamo na vurugu kubwa sana, kama jinsi ambavyo demokrasia inazusha vurugu!

Ukishakua na watu wenye upeo mdogo wa kufikiri na kiwango cha chini cha maendeleo, uwezekano wa dini kutumika vizuri ni mdogo sana. Badala yake utaibuka uadui kati ya dini moja na nyingine, watu watatengana, undugu utavunjika, vita zitatokea nk. Na pia watatokea wajanja wachache wataoitumia hii nafasi kujinufaisha kwa namna moja ama nyingine.
 
Kama si dini hii dunia pangekuwa ni uwanja wa vita

Utafiti mdogo tu utakuonyesha kuwa watu wasio na dini kabisa, au wenye dini tofauti na ukristo au uislamu, ni watu wa amani sana. On the contrary, vita zote kubwa duniani, matukio makubwa ya uhalifu wa kila aina, yanafanywa na watu wenye dini!

Wewe umewahi kusikia wapi vita ya kidini ambayo haihusishi ama wakristo na waislamu, au dini hizo mbili na wasio na dini au wenye dini zingine? Mfano, umewahi kusikia vita kati ya rastafarians na wahindu? Au kati ya wabuddha na wapagani?

Tafakari.
 
Dini imepeleka huduma kama hospitali na mashule, umeme, barabara, usafiri hasa huko vijijini ndanindani.

Kuna vijiji nilienda miaka fulan walikua hawana usafir kabisa ukitaka kusafir unamngoja padre aje jumapili kusalisha hlf unaomba lifti akuache tauni.
 
Utafiti mdogo tu utakuonyesha kuwa watu wasio na dini kabisa, au wenye dini tofauti na ukristo au uislamu, ni watu wa amani sana. On the contrary, vita zote kubwa duniani, matukio makubwa ya uhalifu wa kila aina, yanafanywa na watu wenye dini!..
Inaonekana hujui maana ya Dini. Kwanza nakupa kazi wakina hawana Dini halafu ni watu wa Amani ? Maana hata "Atheism" nayo ni Dini.
 
Wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia dini ilikuwa imejaa duniani,vita vya Mashariki ya kati, Vietnam, Sri Lanka, Congo, Angola, Sudan, Uganda , CAR, India na Pakistan vimepeganwa na vingine vinaendelea kupiganwa dini ikiwa imejaa tele duniani.
Kama si dini hii dunia pangekuwa ni uwanja wa vita
 
Atheism sio dini
Inaonekana hujui maana ya Dini. Kwanza nakupa kazi wakina hawana Dini halafu ni watu wa Amani ? Maana hata "Atheism" nayo ni Dini.
 
Wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia dini ilikuwa imejaa duniani,vita vya Mashariki ya kati,Vietnam,Sri Lanka,Congo,Angola,Sudan,Uganda ,CAR,India na Pakistan vimepeganwa na vingine vinaendelea kupiganwa dini ikiwa imejaa tele duniani.
Sasa mbona unajijibu mwenyewe mzee ? Mbona unataja uchache kisha unahitimisha kwa dunia nzima ?

Ina maana unataka kuniambia hujui maana ya Vita ya Dunia ? Kwani vilipiganwa Dunia nzima vita hivyo ? Hayo ni majina tu mzee yasiyo na uhalisia wowote.
 
Kwa nini imani hii haiondoi dhulma na manyanyaso wanayofanyiana binadamu? Iko kwa ajili ya kutunza amani tu?
Dini imeleta mazuri na mabaya ila kimizania mazuri ni mengi zaidi.

Hizi Dini zimesaidia watu wajue kuna nguvu kuu iliyo juu yao (Mungu/mwenye enzi/God/Mulungu) na mwishowe kila mtu atawajibika kutoa majibu kwa yale aliyofanya hapa duniani.

Imani hii ndo muhimili wa Amani tuliyonayo duniani leo hii. Vinginevo dunia ingekuwa sehemu hatari sana.
 
Nini maana ya dini
Dini ni tamko lenye asili ya Kiarabu, lenye maana ya njia au mwenendo au mfumo wa maisha anao endana nao mtu fulani katika shughuli zake za kila siku.
 
Dini ni tamko lenye asili ya Kiarabu, lenye maana ya njia au mwenendo au mfumo wa maisha anao endana nao mtu fulani katika shughuli zake za kila siku.
Hiyo definition ime base katika muktadha wa kiarabu au in generally?

Hii tafsiri umeitoa kwenye chanzo kipi?
 
Hiyo definition ime base katika muktadha wa kiarabu au in generally?

Hii tafsiri umeitoa kwenye chanzo kipi?
Hii kwa ujumla wake. Nimeitoa katika Kamusi "Maajim al Maan".
 
Inaonekana hujui maana ya Dini. Kwanza nakupa kazi wakina hawana Dini halafu ni watu wa Amani ? Maana hata "Atheism" nayo ni Dini.

Atheists wachache ninaowafahamu wako very peaceful compared na wenye dini wengi ninaowafahamu. Washika dini wengi sana ninaowafahamu nikiwepo na mimi ni wanafki wakubwa, wasengenyaji, waongo, waasherati, wezi, wapiga dili, wachawi, walevi, wagomvi, wabaguzi, wenye wivu, husuda na kila aina ya uovu unaoujua wewe.
 
Shukrani mkuu
Upo deep Sana kwenye upambanuzi wa mada tofauti tofauti
Binafsi nakukubali sana Jf,najiulizaga huu uwezo sijui uliupatia wapi!
Nimejitahidi kusoma na kujifunza vingi, na bado nina vingi zaidi vya kusoma na kujifunza.

Shukurani.
 
Atheists wachache ninaowafahamu wako very peaceful compared na wenye dini wengi ninaowafahamu. Washika dini wengi sana ninaowafahamu nikiwepo na mimi ni wanafki wakubwa, wasengenyaji, waongo, waasherati, wezi, wapiga dili, wachawi, walevi, wagomvi, wabaguzi, wenye wivu, husuda na kila aina ya uovu unaoujua wewe.
Tunaongelea dini hatuongelei watu wa Dini. Kwani Dini gani katika hizi dini zinazo amini uwepo wa Mola muumba zinafundisha unafiki, uzinzi, uongo,kupiga dili, uchawi ?
 
Utafiti mdogo tu utakuonyesha kuwa watu wasio na dini kabisa, au wenye dini tofauti na ukristo au uislamu, ni watu wa amani sana. On the contrary, vita zote kubwa duniani, matukio makubwa ya uhalifu wa kila aina, yanafanywa na watu wenye dini!

Wewe umewahi kusikia wapi vita ya kidini ambayo haihusishi ama wakristo na waislamu, au dini hizo mbili na wasio na dini au wenye dini zingine? Mfano, umewahi kusikia vita kati ya rastafarians na wahindu? Au kati ya wabuddha na wapagani?

Tafakari.
Sio hizo mbili tu, Wahindu wanawapiga waislam huko India mkuu.
 
Bila shaka ni kiarabu sivyo?
Kijana mbona una ruka ruka sana. Kwani Dini kwa Kiswahili ni nini mzee ?

Siyo Kiarabu.

Pili, unapo sema Kiarabu una maanisha ya kuwa Kiarabu kinakosea au Kiarabu siyo Lugha au nini ? Nieleweshe hapo maana naona umeanza kuogopa mapema sana.
 
Nakubaliana na uliyoyasema, na kwa mtazamo wangu, ili dini itumike vizuri ni lazima wale wanaoitumia wawe na upeo fulani wa uelewa, na kiwango fulani cha maendeleo..
Maneno yako ni kweli kabisa.

Dini bila elimu na upeo ni rahisi sana kutumika vibaya.
 
Back
Top Bottom