Mchakato wa upatikanaji wa madereva walio bora na smart zaidi

Angyelile99

Member
Oct 9, 2023
12
7
Kati ya maeneo ambayo serikali inatakiwa kuendelea kutokea macho ni pamoja na usalama barabarani, sio tu kwa kuweka idadi kubwa ya askari wa usalama barabarani, wala sio tu kuhakikisha kila dereva eliyepo barabarani basi awe na leseni. Moja ya jambo kubwa ambalo serikali inatakiwa kulitolea macho sana, ni kuangalia namna ambavyo hizi leseni zinatolewa kwa hawa madereva.

Leo hii mtu anaenda VETA akapata ujuzi wa udereva halafu mchakato wa kutoa leseni unakuja kufanyika na kitengo kingine kabisa ambacho hakina uhusiano wa moja kwa moja na hizi taasisi za vyuo vya kiufundi dereva.

Hoja yangu ya msingi ni kwamba, ili kuendelea kupunguza idadi ya madereva wasio na ujuzi kutoka vyuo husika basi kuna haja ya kuanza matumizi ya cheti cha muhitimu wa mafunzo ya udereva kutoka chuo kinachotambulika rasmi ikiambatana na leseni.

Vyote Kwa pamoja kuwe na utaratibu wa kukagua humo barabarani. Kwani siku hizi kumekua na katabia kwamba mtu akiwa tu na laki nne basi kupata leseni kwa urahisi sana tena kwa daraja atakalo yeye, ambapo ni kinyume na sheria. Hivyo mimi binafsi naona kuna haja ya matumizi ya cheti na leseni kwa pamoja kama sehemu ya kuhakikisha tunakua na madereva makini na wenye taaluma.
 
Kati ya maeneo ambayo serikali inatakiwa kuendelea kutokea macho ni pamoja na usalama barabarani, sio tu kwa kuweka idadi kubwa ya askari wa usalama barabarani, wala sio tu kuhakikisha kila dereva eliyepo barabarani basi awe na leseni kwa pamoja kama sehemu ya kuhakikisha tunakua na madereva makini na wenye taaluma.
Sawa uko vizuri!Tunaanza kuona maoni yako kama yanamanufaa kwa taifa, maana umeanza kusema una homa🙂🙂
 
Back
Top Bottom