Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,586
- 4,274
Kwa watu wanaosafiri kwa magari mara kwa mara watakubaliana na mimi kuwa, madereva wa Malori ni kati ya madereva walio iva kimafunzo pengine kuliko kundi lingine lolote barabarani.
Huwa wapo makini, waangalifu, na hawafanyi maamuzi ya hovyo hovyo kama hawa wengine wanao tusafirisha.
TATIZO; WANAENDESHA MALORI CHAKAVU!
Nafikiri ipo haja ya Serikali kuangalia upya vigezo vya malori yanayo agizwa na kuingia Nchini. Lori sijui limetembea kms milioni tano hilo ni scraper kabisa halafu tunategemea likapande milima ya Kitonga!!!!
Kuhusu Leseni za Madereva wa malori; hata kwa akili ya kawaida, sio rahisi kwa mmiliki kumpa dereva kanjanja akaendeshe Lori la shs milioni 700 + eti akiwa na leseni ambayo haieleweki; wazungu husema " it doesn't connect....na maanisha, leseni zao sio changamoto....
KWA KUWASAIDIA - kwa waombaji wapya, Leseni za daraja C mngeongeza kigezo cha ufaulu wa elimu ya kawaida ili kupima uelewa. Udereva wa abiria ni kazi na sio ubabaishaji.....
Najua visabisha ajali vipo vingi ila kwa leo nimeongelea uchakavu wa malori kwani kwa kiasi kikubwa ndio yamekuwa yanaua watu wengi kwa pamoja