Mchakato wa Twiga Cement Kuinunua Tanga Cement Uwekwe Wazi ili Kuondoa Malalamiko

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MHE. TIMOTHE MNZAVA - MCHAKATO WA TWIGA CEMENT KUINUNUA TANGA CEMENT UWEKWE WAZI KUONDOA MALALAMIKO

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Paul Mnzava leo Bungeni wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara amesema Mchakato wa Kampuni ya Twiga Cement kuinunua Kampuni ya Tanga Cement uwekwe wazi ili kuondoa malalamiko

"Mwezi Oktoba, 2021 kampuni ya Scancem International DA (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement) na Afrisam (kampuni yenye hisa nyingi 68% katika kiwanda cha Tanga Cement) walitoa tamko la pamoja kwamba wamemaliza vigezo na makubaliano ya kuhamisha hisa za Afrisam kwenda Scancem" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Novemba 02, 2021 kampuni ya Scancem International DA (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement) wakaindikia Tume ya Ushindani (FCC) kuomba kuthibitishwa. FCC wakapokea na kuchakata na kisha wakaridhia kuhamisha hisa kutoka Afrisam kwenda Scancem lakini FCC walitoa masharti" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Nchi yetu inafuata utawala wa sheria lakini siku za karibuni kumekuwa na matukio ambayo yanafanywa na baadhi ya taasisi za serikali, na kupelekea nijaribu kuamini pengine zinapoelekea ni kutokutii utawala wa sheria katika nchi yetu" Timotheo Mnzava, mbunge wa Korogwe vijijini

"Hakuna mwekezaji anaweza kuja kuwekeza katika nchi ambayo ana wasiwasi na utawala wa sheria unavyotekelezwa katika nchi" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Moja ya njia nzuri ya kuvutia na kushawishi wawekezaji ni kuwahakikishia utulivu katika nchi na kuwahakikishia kwamba nchi yetu inafuata utawala wa sheria" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Wadau watatu hawakuridhiswa na mchakato wa kuhamisha hisa za Afrisam (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Tanga Cement) kwenda Scancem (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement), hivyo walikwenda mahakamani kufungua kesi katika Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara na Haki" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Wadau waliokwenda kufungua kesi katika Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara na Haki kuhusu #SakataLaTwigaCementTangaCement , mdau wa kwanza ni kampuni ya Scancem (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement) kwa kutoridhishwa na masharti aliyowekewa na Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCC)" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Mdau wa pili aliyekwenda mahakamani kufungua kesi katika Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara na Haki kuhusu #SakataLaTwigaCementTangaCement ni kampuni ya Chalinze Cement na mdau watatu ni Chama cha Walaji Tanzania (TCAS), shauri likasikilizwa." Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Mnamo tarehe 23 Septemba, 2022 Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara na Haki ikatoa uamuzi kuhusu #SakataLaTwigaCementTangaCement , kwamba baada ya kupima hoja zote na kwa kutumia ripoti kuu ya uchambuzi ya Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCC) likazuia mchakato wa kuhamisha hisa za Afrisam (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Tanga) kwenda Scancem (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement)" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Mnamo tarehe 23 Septemba, 2022 Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara na Haki ikatoa uamuzi kuhusu #SakataLaTwigaCementTangaCement , kwamba baada ya kupima hoja zote na kwa kutumia ripoti kuu ya uchambuzi ya Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCC) likazuia mchakato wa kuhamisha hisa za Afrisam (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Tanga) kwenda Scancem (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement)" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Uamuzi wa mahakama (Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara na Haki) ukishatolewa kuna namna mbili tu, moja ni kuomba mapitio katika mahakama hii au kukata rufaa kwenda mahakama ya rufani. Jambo hilo halikufanyika" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini #SakataLaTwigaCementTangaCement

"Mwezi Desemba, 2022 kampuni ya Scancem (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement) imeiandikia Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCC) kuomba kupewa kibali cha ya kuhamisha hisa za Afrisam (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Tanga Cement) kwenda Scancem" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini #SakataLaTwigaCementTangaCement

"Tarehe 11 Februari, 2023, Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCC) imetoa tamko watu wapeleke maoni kuhusu #SakataLaTwigaCementTangaCement .Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara na Haki ni ya kwetu na imeundwa kisheria, utaratibu wa ku-challenge uamuzi wa mahakama hii upo, kwanini utaratibu huo haukufuatwa" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Moja ya jambo ambalo Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara na Haki katika kutoa hukumu kwenye sakata la kuhamisha hisa za Afrisam (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Tanga) kwenda Scancem (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement) ni ripoti kuu ya Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCC) kuhusu uchambuzi wa #SakataLaTwigaCementTangaCement" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Uchambuzi kuhusu #SakataLaTwigaCementTangaCement ulionesha kwamba Afrisam (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Tanga Cement) na Scancem (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement) wakiungana watakuwa na hisa nyingi katika soko la saruji nchini . Watakuwa na 42.27% ya hisa zote za biashara ya saruji nchini, kitu ambacho ni hatari na kinyume na kifungu cha 11 (1) cha sheria ya ushindani" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini

"Kinachotutisha zaidi ni kwamba mwezi Machi, mwaka huu BRELLA (Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wameifutia usajili kampuni ya Chalinze Cement ambayo ni mmoja wa wadau waliokwenda mahakamani kupinga mchakato wa kuhamisha hisa za Tanga Cement kwenda Twiga Cement kwa waliachodai kuwa hawakuwasilisha ritani za mwaka" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini #SakataLaTwigaCementTangaCement

"Binafsi sikatai mchakato wa Twiga Cement kuinunua Tanga Cement au kuungana, ni mchakato wa kawaida katika biashara ili kuyafanya makampuni yaendelee kufanya kazi vizuri, lakini kwenye sakata la Twiga Cement kutaka kuinunua Tanga Cement mbona kuna hali ya kulazimisha sana, mbona jambo hili halikuwa wazi. Twiga Cement wamesajiliwa katika soko la hisa watangaze wawekezaji waje na ili kuwe na ushindani" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini #SakataLaTwigaCementTangaCement

"Eneo la kiwanda cha Tanga Cement ndio eneo la kiwanda pekee chenye hifadhi kubwa ya kutosha ya malighafi ya kuzalisha saruji kutoka eneo lingine kokote nchini, huyu Twiga Cement hana hifadhi ya kiwango kilichopo katika kiwanda cha Tanga Cement" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini
#SakataLaTwigaCementTangaCement

"Hofu yetu ni kwamba Twiga Cement inapomchukua Tanga Cement, je biashara itaendelea? brand ya Tanga Cement itaendelea kuwepo?" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini #SakataLaTwigaCementTangaCement

"Kama Tanga Cement imesajiliwa katika soko la hisa, kuna watu wengi wana hisa katika kiwanda hiki, kuna shida ya kutangaza mchakato wa kuhamisha hisa za Tanga Cement kwenda Twiga Cement na ukaenda vizuri, mchakato ukitangazwa utaondoa usiri na malalamiko na tutapata mwekezaji atakayetoa fedha nyingi na atakuwa serious na biashara ya saruji nchini" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini #SakataLaTwigaCementTangaCement

"Maamuzi ambayo Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCC) iliyoyabariki na Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara ikayakataa katika mchakato wa Twiga Cement kuinunua Tanga Cement ni kwamba walitaka kuuza hisa moja kwa shilingi 3,100 jumla kwa hisa zote ingekuwa ni shilingi bilioni 137" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini #SakataLaTwigaCementTangaCement

"Twiga Cement na Tanga Cement wakiungana, watakuwa na asilimia kubwa ya hisa katika soko la saruji nchini kuzidi asilimia inayotakiwa ni kinyume na sheria. Serikali mnalioanje hili suala" Timotheo Mnzava, mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini #SakataLaTwigaCementTangaCement
 

Attachments

  • FvRdmyaWAAEfOIa.jpg
    FvRdmyaWAAEfOIa.jpg
    50.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom