Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,898
- 943
MBUNGE JUDITH KAPINGA ASISITIZA UTARATIBU UFUATWE BAINA YA TWIGA CEMENT NA TANGA CEMENT
Mbunge wa Viti Maalmu Vijana Kupitia Kundi la Vijna, Mhe. Judith Kapinga jana tarehe 04 Mei, 2023 amechangia Bungeni suala la Twiga Cement kuinunua Tanga Cement katika hoja ya bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Baishara iliyosomwa na Waziri Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
"Kigezo kikubwa ambacho Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara (FCT) imetuongoza tukifuate katika sakata la Tanga Cement kununuliwa na Twiga Cement ni kigezo cha utawala wa soko kwamba nani atauza zaidi, ukichukua hisa za Tanga Cement na Twiga Cement kwa pamoja yatauza asilimia 52 katika soko, na inatuonesha kuwa kanda nne kati ya tano kubwa zitatawaliwa na kampuni hizi mbili kubwa" - Mhe. Judith Kapinga, Mbunge Viti Maalum kupitia kundi la Vijana
"Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCC) wamefanya utafiti na wana taarifa zinazoonesha kwamba kampuni ya Twiga Cement na Tanga Cement zikiungana kwa pamoja zitapelekea utawala wa soko kwa asilimia 35" - Mhe. Judith Kapinga, Mbunge Viti Maalum kupitia kundi la Vijana
Ni jambo la heri kampuni ya Scancem (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Twiga Cement) inataka kununua hisa za Afrisam (kampuni yenye hisa nyingi katika kiwanda cha Tanga Cement) lakini mgogoro ulianzia pale ambapo kumejiridhisha kwamba Twiga Cement na Tanga Cement wakiungana wanazidi utawala wa soko kwa 35" - Mhe. Judith Kapinga, Mbunge Viti Maalum kupitia kundi la Vijana
"Sababu ya sheria ya ushindani kuweka taratibu ni kudhibiti soko dhidi ya ushindani, kuhakikisha walaji wanapata bidhaa na bidhaa ni lazima ziwe stahimilivu katika soko. Tusipohakikisha taratibu zinafuatwa linakuwa ni jambo ambalo linazua maswali mengi sana" - Mhe. Judith Kapinga, Mbunge Viti Maalum kupitia kundi la Vijana
"Hakuna mwekezaji anayekatazwa kununua hisa za kampuni yoyote, ishu kubwa ni kwamba taratibu ambazo tumejiwekea ni lazima zifuatwe" - Mhe. Judith Kapinga, Mbunge Viti Maalum kupitia kundi la Vijana
"Sheria ya Ushindani inasema wazi kabisa kwenye makubaliano yoyote ambayo yanachagiza kuathiri soko kwa maana ya ushindani au yanajikita katika kuharibu ushindani ni makubaliano ambayo hayakubaliki kisheria" - Mhe. Judith Kapinga, Mbunge wa Viti Maalum kupitia kundi la vijana