Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,446
- 7,817
Mwanahisa mkubwa zaidi anayemiliki 70% ya hisa kwenye kiwanda cha Tanga Cement ameamua kuuza hisa zake zote kwa kampuni ya Scancem inayomiliki kiwanda cha Twiga Cement, Wazo Dar es Salaam.
Wawekezaji hao wa Afrisam wamesema kikwazo kikubwa wanachokutana nacho ni kiasi na ubora wa umeme unaopatikana nchini vinavyoathiri uwezo wao wa uzalishaji. Wamesema kutatua tatizo la umeme ni gharama kubwa sana kwa muwekezaji na inahitaji uwekezaji mkubwa kuweza kutatua kutokana na gharama kubwa za kuagiza na kuingiza nchini majenereta makubwa.
Wamesema pia hatua hiyo inapelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa gharama za uzalishaji ambayo mwisho inakuwa na athari hasi kwa mtumiaji wa mwisho.
Mwenyekiti wa bodi ya Tanga Cement, Patrick Rutabanzibwa amesema Afrisam amekubali kuachia hisa zake na kuziuza kwa Scancem na waliitisha mikutano miwili na wameridhia.
Miaka 8 iliyopita, Tanga Cement ilichukua mkopo mkubwa kujenga tanuri lake la pili kuongeza uzalishaji lakini ikakumbana na changamoto kubwa walipofika sokoni ya viwanda vipya vilivyoibuka nchini huku Tanga pekee kwasasa kukiwa na viwanda vinne vya Tanga cement, Huaxin, Kilimanjaro na Sungura.
Soko la cement likapata ushindani mkubwa na bei zikashuka hivyo Tanga Cement wakashindwa kupandisha bei, mwaka jana Tanga cement walirokedi hasara. Tanga Cement haijatoa gawio kwa wanahisa wake takriban miaka mitano sasa.
Octoba 2021 Scancem walifikia makubaliano ya kununua aslimia 68 ya hisa za Tanga cement kwa thamani ya bilioni 137 huku sababu kubwa wakati huo ikiwa madeni yaliyokuwa yanakikabili kiwanda hicho yaliyofikia bilioni 230 na kupelekea uwezekano wa kufilisika.
Pamoja na ombi hilo kupitishwa na tume ya ushindani lilikumbana na kizingiti kutoka bodi ya ushindani baada ya Chalinze Cement na TCAS kuweka mapingamizi mwaka 2022.
Bodi ya ushindani ilisema muungano wa Twiga na Tanga Cement utaleta utawala sokoni hivyo kupelekea uwezekano wa kupanga bei.
Scancem ameahidi kuweka mtaji kununua mitambo na kukarabati mashine na viwanda hivyo viwili kufanya kazi kama kitu kimoja.