Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu ununuzi wa hisa za Tanga Cement unaofanywa na Twiga Cement

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

SERIKALI IMETOA UFAFANUZI KUHUSU UNUNUZI WA TANGA CEMENT UNAOFANYWA NA TWIGA CEMENT

Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu ununuzi wa hisa za Tanga Cement unaofanywa na Twiga Cement, kuwa umefuata taratibu za kisheria na kwamba kampuni inayopinga ununuzi huo ya Chalinze Cement imeshafutiwa usajili kwa udanganyifu.

Mawaziri watatu walijibu hoja za wabunge 23 waliochangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2023/24 ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambao baadhi yao walipinga ununuzi huo huku wengine wakiuunga mkono.

Akihitimisha hoja yake iliyopitishwa bungeni Dodoma Mei 4, 2023, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji alieleza kuwa hoja za wabunge hao zilijikita katika eneo la kwanini Tume ya Ushindani (FCC) imeruhusu muungano wa kampuni za Twiga na Tanga ambazo awali zilizuiwa na Baraza la Ushindani (FTC)

“Jibu sahihi ni kwamba FCC haikushughulika na ombi la muungano wa kampuni mbili ambao ulizuiwa na FTC. Tunaheshimu sheria zote za nchi hii na kama waziri niliyebeba Katiba ya nchi hii nikaapa, kuzilinda nitazilinda,” alisisitiza.

Alisema kilichofanyika ni kwamba Desemba 22, mwaka 2022 kampuni ya Scancem International DA (Scancem) – kampuni tanzu ya Heidelberg Cement AG, inayomiliki Twiga Cement inayomiliki asilimia 69 Twiga iliomba kununua asilimia 68.33 za AfriSam Mauritius Investment Holdings Limited, mmiliki wa Tanga Cement.

“Taratibu zote za kisheria zilifuatwa katika kuwasilisha na kuchambua ombi hili. Kwa mujibu wa Sheria za Ushindani na kanuni zake inatoa wajibu kwa kampuni zinazotaka kuungana na kukidhi vigezo kuwasilisha maombi yao bila kujali kama maombi yao ya awali yalikataliwa au kukubaliwa,” alieleza.

Alifafanua kuwa ombi hilo lililoruhusiwa ni ombi jipya kwa mujibu wa sheria na kanuni lililopokelewa kwa barua yenye kumbukumbu namba CBC 127359/144 lililotoewa mbele ya FFC kwa kuzingatia takwimu za hali ya soko la saruji kwa mwaka 2022.

Waziri Kijaji alifafanua kuwa kwa sababu ombi hilo lilipokelewa mwaka 2022 hakukuwa na sababu ya kutumia takwimu za mwaka 2020 na hivyo kutumia takwimu za mwaka 2022.
 

Attachments

  • FvZQdwdWAAIodIEKO.jpg
    FvZQdwdWAAIodIEKO.jpg
    152.8 KB · Views: 9
  • FvZQdwfXwAEWh5_a.jpg
    FvZQdwfXwAEWh5_a.jpg
    136.8 KB · Views: 9
  • FvRpBTpWwAAN1cZPOI.jpg
    FvRpBTpWwAAN1cZPOI.jpg
    124.6 KB · Views: 7
Ngoja nisubiri wajuzi! Maana sijaelewa hii sinema! Na hii chalinze cement kiwanda chake kipo wapo!!?
 
Hii si habari njema kwa wanunuaji wa cement - japo ni jambo halali. Maana ushindani wa wazalishaji unapungua, jambo ambalo linaweza kuzivutia juu bei za cement na bidhaa zake.
 
Back
Top Bottom