Eng Kimox Kimokole
JF-Expert Member
- Jun 9, 2010
- 1,032
- 759
Nimetazama upepo unavyokwenda kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Katiba (Katiba Mpya: Masikhara haya), nimeona na kusikia maneno ya JK jana pale PTA, nimesikiliza mahojiano ya Deus Kibamba Channel Ten, Maoni ya Wana CUF na wananchi, wengi wamekata tamaa na kukubaliana na hali halisi, woga, hofu na unyonge umetujaa.
Kwa hali halisi naona kabisa hakuna mabadiliko yatakayotokea, tutakubaliana na Tume itakayoundwa, tutakubaliana na mchakato huo, tutapiga kura za maoni na mwishowe kupata katiba CCM waliyoitaka. Ndio tutapata katiba hiyo na maoni yetu mengi hayatachukuliwa, tutarudi hapa kulalamika kama ilivyo ada yetu, tutarudi hapa tena kusema tulisema sisi ona kilichotokea, hapa tulipojikwaa ndipo patakapotugharimu, UKONDOO wetu ndiyo chumo letu.
Hakika tutarudi hapa tena kulalama. NDIYO TUTARUDI na hakika Tulichokisubiri kwa muda mrefu hatutakipata. Hongereni Watanzania kwa moyo wa uvumilivu na tuendelee kuomba Mwenyezi Mungu aje atusaidie kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu, NDIYO TUOMBE MUNGU huenda atashuka atajumuika nasi na kututia ari thabiti ya kudai haki yetu.
Heri, Mafanikio na Kusubiri Kwema Watanzania ( waliokuwa Watanganyika)!!