Mchakato kupata Katiba Mpya: Hakuna Maandamano, Upinzani kwa hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchakato kupata Katiba Mpya: Hakuna Maandamano, Upinzani kwa hili!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimox Kimokole, Nov 19, 2011.

 1. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimetazama upepo unavyokwenda kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Katiba (Katiba Mpya: Masikhara haya), nimeona na kusikia maneno ya JK jana pale PTA, nimesikiliza mahojiano ya Deus Kibamba Channel Ten, Maoni ya Wana CUF na wananchi, wengi wamekata tamaa na kukubaliana na hali halisi, woga, hofu na unyonge umetujaa.

  Kwa hali halisi naona kabisa hakuna mabadiliko yatakayotokea, tutakubaliana na Tume itakayoundwa, tutakubaliana na mchakato huo, tutapiga kura za maoni na mwishowe kupata katiba CCM waliyoitaka. Ndio tutapata katiba hiyo na maoni yetu mengi hayatachukuliwa, tutarudi hapa kulalamika kama ilivyo ada yetu, tutarudi hapa tena kusema tulisema sisi ona kilichotokea, hapa tulipojikwaa ndipo patakapotugharimu, UKONDOO wetu ndiyo chumo letu.

  Hakika tutarudi hapa tena kulalama. NDIYO TUTARUDI na hakika Tulichokisubiri kwa muda mrefu hatutakipata. Hongereni Watanzania kwa moyo wa uvumilivu na tuendelee kuomba Mwenyezi Mungu aje atusaidie kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu, NDIYO TUOMBE MUNGU huenda atashuka atajumuika nasi na kututia ari thabiti ya kudai haki yetu.

  Heri, Mafanikio na Kusubiri Kwema Watanzania ( waliokuwa Watanganyika)!!
   
 2. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  wadanganyika siku zote huwa hawana msimamo!
   
 3. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mods tafadhali mngeipeleka jukwaa la siasa hii thread maana ni uzi wa ukweli!
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Hayo ni maoni yako, nameamua kukubali kutokukubaliana.
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Acha kulalamika hovyo.
   
 6. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Bado watanzania tunapata angalau mlo mmoja kwa siku, tunapewa pewa vihera kama wale vijana wanaosukuma gari la Jairo kwa kujipendekeza na kupata kununua gari ingawa ni wachache, bado watz tunaweza kupata kiwanja na kujenga angalau kakibanda, kwa hiyo hadi tutakapokosa hivyo vitu vyote au watoto wetu watakapoanza kuishi kama wako utumwani basi ndo uoga wetu utatutoka.
   
 7. MBUFYA

  MBUFYA JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Maisha bora kwa kila mtanzania, mh? nadhani katika nchi hii wengi si watanzania kama kauli mbiu hii imetimia
   
 8. M

  Mr. Clean Senior Member

  #8
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nani hataki kuwa na familia yake (hata kama ni katika nyumba za majani kama wale walotimuliwa juzi kule makao shinyanga?) aende kusota miaka mitatu jela?

  adhabu zipo wazi kwa atakaye pinga mswada, kafafanua werema jana!....btw, katiba mpya ipo tayari..inachosubiriwa ni kuchapishwa nakala za kutosha tuu mda ukifika, we ng'ang'ana na maoni feki yatakayo collectiwa!

  hivyo usishangae kumung'unya maneno kwa kibamba na wale wengine walokuwa front line kupendekeza mswada upingwe.
   
 9. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Maneno yako hata mimi nimeyakubali, Katiba imeshaandikwa bado kutyoa nakala za kutosha tu
   
 10. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nalalamika pia
   
 11. mbasajohn

  mbasajohn JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa kwamba watanzania tutaliacha hili nalo lipite kama hatuoni kisa tumetishwa na kuambiwa kuwa amani yetu ni muhimu sana kuliko katiba mpya yenye mambo tunayoyataka ndiyo tumekubali bila kujua kuwa amani ya sasa itageuka kuwa damu ya miaka ijayo kwa sababu tu tuliambiwa amani ni muhimu sana na sisi bila aibu tukaacha mchakato wa katiba utawaliwe na walewale walituharibia katiba mwaka 1977. Lakini bado hatujachelewa watanzania naomba tusikubali maana katiba ni yetu na lazi,ma watusikilize hata kama tutakuwa jela au makaburini lakini lazima watusikilize sisi ndiyo wenye hii nchi na vizazi vijavyo vitaishi maisha ya amani ya kweli na sio ya uoga kama leo hii saa hii mwaka huu tutafanya maamuzi magumu ya kusema kuwa katiba ni muhimu kuliko amani hii ya woga ambayo tumeendelea kuihubiri kwa miaka hamsini sasa. Hebu kila mtu ajiulize amefanya nn kuhakikisha tunapata katiba mpya yenye ubora tunaoutaka na je anaridhika na mchango wake na je anasemaje kuhusu mchakato unavyoenda? kama anaridhika na mchakato mzima basi amekamilisha kazi yake ya awali na ajiandae na awamu ya pili ya kutoa maoni kwa tume itakayoundwa na CCM(serikali) lakini kama hajaridhika basi kazi bado ni kubwa na sasa ndiyo wakati wa kuchukua hatua kuhakikisha anafanya kitu kwa nchi yake na watu wake maana nchi ni zaidi ya serikali au vyama vya siasa asilale na kulalamika tu maana hilo halitasaidia kupata katiba mpya anayoitaka na ambayo watanzania wanaitaka maana watanzania ni pamoja na yeye. Swali langu la leo ni je umefanya nini kuhakikisha tunapata katiba iliyo bora na je uko tayari kuchukua hatua na kufanya maamuzi magumu ili kupata katiba mpya unayoitaka na ambayo watanzania wote tunaitaka?
   
Loading...