Kitendo cha CCM kutaka kuhodhi mchakato wa Katiba kama walivyofanya mwaka 1977 na 2014 kitasababisha tushindwe kupata Katiba Bora.

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,224
12,946
UPATIKANAJI WA KATIBA YASASA (1977)
Historia inatunesha Katiba hii ya tuliyonayo ya mwaka 1977 ilipatikana kutokana na tume ya Rais iliyokuwa nawajumbe 20, kwa idadi sawa toka pande zote za muungano ikiongozwa na Sheikh Thabit Kombo akisaidiwa na Pius Msekwa kama katibu wa tume hii ya Rais. Hata hivyo tume hii ni ileile iliyotunga katiba ya CCM. Katiba hii ilipitishwa ndani ya masaa matatu na bunge maalumu lililoteuliwa na Rais kutokana na bunge la kawaida.

Pamoja na kupatikana kwa Katiba yenye chama kimoja tu Bara na Visiwani, tabia ile iliyorithiwa tangu mwanzo wa mabadiliko ya Katiba miaka ya nyuma haikufichwa bali iliwekewa mazingira mazuri zaidi na yaliyowaondoa wengi katika ushiriki. Kwa wakati huo, kwa mfano, Kamati ya Chama ambayo ilikuwa imehusika katika jukumu la kuandaa na kuwasilisha mapendekezo ya kuwepo kwa Chama kimoja tu kwa pande zote za Muungano ndiyo iliyogeuzwa kwa maagizo ya Kamati Kuu ya Chama (National Executive Committee (NEC)) kufanyika kuwa Tume ya Katiba (Constitutional Commission) na kutakiwa kuandaa na kuwasilisha mapendekezo ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ripoti ya mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwa Kamati Kuu ya Chama (NEC) na sio Bunge kwa vile chama ndicho kilicho kuwa na maamuzi ya mwisho.

Ndipo baadae, NEC ikaliagiza baraza la mawaziri (cabinet)kuandaa rasimu ya muswada ambao ungewasilishwa kwa Bunge la Katiba(constituent assembly) kuhusu kutungwa kwa Katiba Mpya. Muswada huo ukapitishwa moja kwa moja Bungeni na Katiba mpya ikapatikana mwaka 1977. Mfumo wa chama kimoja ukazidi kujikita na dhana yake ya Chama kushika hatamu ikaneemeka zaidi. Kwa hali hii ni dhahiri kuwa hata Katibatuliyo nayo hivi leo haikuwashirikisha wananchi wote kwani si wotewaliokuwa wanachama wa chama tawala. Hivyo utaratibu wa kutungaKatiba mpya kwa kuitisha kongamano la Katiba (constitutional conference) haujawahi kufanyika wala kuwa sehemu ya desturi nchini Tanzania hadi leo.
Rejea:-

KILICHOKWAMISHA MCHAKATO WA KATIBA MPYA MWAKA 2014.
Hakukuwa na tabu kabisa wakati tume ya mabadiliko ya Katiba ikifanya kazi yake! ila shughuli ilikuja kwenye upatikanaji wa wajumbe wa Bunge maalum la Katiba, hapa CCM wenzetu walijisahau na kuamini kama ule mchakato wa katiba mpya ulikuwa wa kwao na kuamua kuvua Utanzania wao na kujivisha UCCM kwanza.
Moja ya vifungu vilivyoleta taflani katika Rasimu ya 2 ya Katiba mpya iliyotelewa na Tume ya Mbadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba ni TUNU ZA TAIFA.

TUNU ni nini?
Maana rahisi kueleweka ni "Zawadi au mambo muhimu ya kujivunia kuwanayo, na ikitokea yamekutoka basi utapata shida sana kuyarejesha" Jaji Warioba alienda mbali zaidi na kusema kuwa kuwa Tunu ndiyo msingi wa maadili na utaaduni wa jamii.
Rasimu ya 2 ya Katiiba ilikuja na TUNU za Taifa kama zifuatavyo.


Ibara 5. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa zifuatazo.
1. Utu
2. Uzalendo
3. Uadilifu
4. Umoja
5. Uwazi
6. Uwajibikaji na
7. Lugha ya Taifa.
Ajabu wajumbe wa Bunge la Katiba wakiongozwa na CCM walikataa kutambua Uzalendo, Uadilifu na Uwajibika kama Tunu za Taifa! unaweza kujiuliza CCM wakiongozwa na Marehemu Mzee SIta na pamoja Samia Suluhu Hassan walikataa kutambua Uwajibikaji, Uzalendo na Uadilifu kama tunu za Taifa kwasababu zipi hasa?

CCM wako tayari kulinda chama chao kuliko kulinda na kuipigania Tanzania iliyo bora yenye Katiba bora itakayoweza kila mtu kuwa chini ya sheria zetu. Sioni kama tuendako kuna mwanga juu ya upatikanaji wa Katiba Mpya iliyo bora kama CCM hawataacha kujitishwa mchakato wa Katiba kuwa wao na wafanye juu chini kulinda chama chao kisitoke madalakani kwa njia yoyote ata ya uchaguzi wanayoiamini wao.
 
Back
Top Bottom