beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Ni hatari kumpunguzia Rais Madaraka. Ni hatari sana hasa kwa nchi zetu hizi.. Ni hatari kweli kweli.. Natamani ungenielewa!Hiyo siyo sahihi! Kumpunguzia rais madaraka kunamfanya rais afanye kazi kwa weledi na uaminifu zaidi. Sababu akifanya kinyume, wawakilishi wa wananchi na wananchi wenyewe waliomchagua ndiyo watamwajibisha. Hata kwa katiba mpya ataendelea kufanya vizuri kama rais ilimradi atafanya kazi yake kwa misingi ya sheria na katiba. Siyo kukurupuka tu hatutaki mambo hayo.