Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Utangulizi Mchakato wa kurekebisha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulianza baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Vyama viwili vikuu vya upinzani nchini, CHADEMA na CUF ndivyo vilivyoanzisha vugu vugu ya kudai katiba mpya.
Umuhimu wa katiba mpya ndio ulikuwa msingi wa kampeni za uchaguzi za vyama hivyo. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliitikia wito huo kwa kuanzisha mchakato wa marekebisho ya Katiba. Hata hivyo mchakato huo ulisimama mwaka 2015, kupisha uchaguzi mkuu wa 2015, na haujaendelea tena tangu kipindi hicho. Mchakato wa marekebisho ya katiba ulipitia awamu kuu tatu.
Awamu ya kwanza ilikuwa ya kuundwa kwa Tume ya marekebisho ya Katiba. Hii iliundwa chini ya uongozi wa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na Tume hii ilisafiri nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi kuhusu muundo wa katiba mpya na ikachapisha rasimu yake ya kwanza baada ya kupata maoni ya wananchi.
Rasimu hii ilijulikana kama “rasimu ya Warioba” na ilichapishwa mwezi Disemba mwaka 2013. Miongoni mwa mambo yaliyopendekezwa katika rasimu hii ni kubadilisha muundo wa sasa wa serikali mbili (Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibari) na kuanzisha muundo wa serikali tatu (Serikali ya Muungano, Serikali ya Tanzania Bara, Serikali ya Zanzibari).
Taasisi ya TWAWEZA kupitia Sauti za Wananchi, ambao hukusanya maoni ya wananchi kupitia simu za mkononi kuhusu kinachoendelea nchini katika nyanja zote za maisha, inakuja kwa mara nyingine na Ripoti ya maoni ya wananchi yenye kichwa Zege limelala? Maoni ya Watanzania kuhusu kukwama kwa mchakato wa marekebisho ya katiba.
Ripoti hiyo ambayo itazinduliwa leo tarehe 19.10.2017 kuanzia saa 5 asubuhi hadi 7 mchana pale Makumbusho ya Taifa (Posta, Mkabala na chuo cha IFM), itabainisha maoni ya wananchi.