Mch. Gwajima amgomea Makonda

Mch. Gwajima amgomea Makonda

Ile Ni Taacc Ya Watu Sio Ya Gwajima, Ndiomaana Alipokuwa Anaumwa Huduma, Iliendelea Kama Kawaida Chini Ya Wachungaji Wasiopungua 70, Yeye Makondakta Ninani Mpaka Acheze Na Taacc Ya Watu?
 
Mchungaji wa makanisa ya kipentekoste mch. Josephat Gwajima amesema hatapoteza muda wake kwenda kumuona Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

Amesema barua aliyoipata toka kwa Mkuu wa Wilaya imemfedhehesha na kasema hataijibu itajibiwa na maombi ya mnyororo yanayoendelea.

Chanzo: Kutoka magazetini.
safi sana gwajima , Who is Makonda by the way ?
 
naandika kutoka ndani ya moyo wangu kabisa , mimi kama Mwana UKAWA nitahakikisha hiki cheo cha ukuu wa wilaya kinatokomezwa ifikapo january 2016 .
 
Uahauri......kwa vile polisi bado wanaendelea na uchunguzi na si ajabu pia TISS,DC Makonda angeachana nae kwani inaweza leta mtafaruku mkubwa wa kidini.Sasa hivi upo kwa nini tuengeze mwingine
 
Hivi kunakuwaga na maombi ya kisasi?!makonda huyu afundishwe misingi ya uongozi(rule of law) yeye sio polisi wala mahakama

Ingawa sijui msingi wa maombi ya kanisa la Gwajima naweza kusema hakuna maombi ya kisasi. Biblia inasema kisasi ni cha Mungu mwenyewe. Hata hivyo watu wanaweza kumwomba Mungu aingilie kati mateso wanayopata au dhuluma wanazofanyiwa. Yeye anatufundisha tuyainue macho yetu juu kwani msaada unatoka kwake. Kwa hiyo kama kweli kuna uonevu au dhulumati Mungu hujibu kwa kadiri anavyoona inafaa.
 
Gwajima kachemka.Mkuu wa wilaya aweza futa au omba NGO fulani ifutwe au isifanye kazi wilayani kwake.hajui role ya mkuu wa wilaya kwenye NGO? ASUBIRI MUZIKI WAKE

Peleka upuuzi huko,kwani ndio mtu wa kwnza kutukana nyerere, alitukanwa na mtikila mbona mkuu wa wilaya hakumuita,mwinyi alizabwa kibao mbona mkuu wa wilaya hakutoa tamko.Mkuu wa wilaya ni mwenyekiti wa ulinzi na usalam wa wilaya polisi anaowasimamia wameshachukua atua yeye kiherehere cha nini?
 
SORRY WAHESHIMIWA...HIVI ILE SHERIA ILIYOPITISHWA JANA YA MITANDAO INAANZA KUTUMIKA LINI???...NIJUWE KABISA ILI SIKU IKIFIKA NIJITOE KWENYE ULIMWENGU WA MITANDAO NA ELECTRONICS NIRUDI ZAMA ZA S.L.P na kulamba vijikaratasi vya posta.

nahisi muda si mrefu kwa sheria zile naweza kujikuta nafungwa miaka kumi au faini milioni 50.
Ha! Ha! Haaaa!!!!! kuna vitu vimepigwa marufuku nchi hii tangu mwaka 61 lakini bado vinadunda !
 
wakuu wetu wengi upenda kujihusisha na mambo mepesi ambayo ni level ya afsa mtendaji wa kata.haya ya level yao kama migogoro ya viwanja na miundombinu mibovu uyakwepa.wanapenda kujitokeza kwenye matukio ambayo yatawauza kwenye magazeti.Ndo tunaona issue ipo police lakin ata mkuu wa wilaya na yeye yumo.nashindwa kuelewa ameshindwa nn kusubili police wakaifanyia kazi then akapewa taarifa.

YAANI...
 
Japo simuungi mkono Gwajima kwa maneno yaliyopelekea sakata lote hili,lakini namuunga mkono asiende kumuona makonda.Kwanza makonda mwenyewe hana usafi/nidhamu kiasi kwamba atatue suala la Gwajima.Kwanza amuombe radhi jaji Warioba then aanze kufuatilia issue za nidhamu.Makonda toa boriti kwenye jicho lako kwanza ndipo uone kibanzi kwenye jicho la Gwajima.
 
Ndio maana Makonda kwa kuzingatia taratibu kuwa utaratibu wa kwanza ni kumwita mhusika ajieleze kamwita.Akikataa wanaenda utaratibu unavyotaka sehemu ya pili hadi kieleweke.

Hata akikataa kuja hakumpi mamlaka ya kufuta organization yake... Kwani kutokuja kwake na organization yake
Kunahusiana nn??
 
Uahauri......kwa vile polisi bado wanaendelea na uchunguzi na si ajabu pia TISS,DC Makonda angeachana nae kwani inaweza leta mtafaruku mkubwa wa kidini.Sasa hivi upo kwa nini tuengeze mwingine
Uelewa wa Makonda ni mdogo sana anafikiri kuandikwa magazetini ni kumuuongezea umaarufu, hiki kitendo cha kugomewa hadharani kinazidi kumshushia heshima na bado itazidi kushuka pale atakapopandishwa mahakamani kwa kitendo cha aibu cha kutoa matusi.
 
Huyu hana cha Biblia wala nini si umemsikia kwenye ile video aliyotukana pengo?yeye hajali bunge,serikali wala polisi.Anaishi kwenye dunia yake ya kufikirika ambayo haiko katika dunia hii

Katika post zako zote unaonesha una chuki binafsi na Gwajima.
 
Nae ni 'mwokovu' mwenzie hivo wanajuana

Yeye ni mkuu wa wilaya cheo kisicho na dini sababu serikali haina dini.Makonda hata kama aliwahi kwenda kwa Gwajima kuondolewa misukule hewa lakini kwenye hili la kumwita Gwajima yuko sahihi.Ni sawa na mkuu wa wilaya anaenda kwa daktari kutibiwa na akapona lakini baadaye akiambiwa yule daktari aliyemtibu ni gaidi lazima yeye kama mkuu wa wilaya amshughulikia huyo daktari gaidi kikamilifu bila kujali tiba yake aliyotoa.

Gwajima ajue anaitwa na mkuu wa wilaya haitwi na muumini wake au mwanae hata angekuwa muumini wake au mwanae wa kumzaa.
 
Hivi katiba mpya itaruhusu vibaraka,watapiaelimu na wasio na uwezo wa kujaji kama Makonda wawepo?jamani wanasheria hebu nisaidien nianze kujua napiga NDIO au HAPANA.Maana huu ukuu wa wilaya watu hupeana kama takrima.
 
Back
Top Bottom