Shauri la Kanisa la Gwajima laondolewa Mahakamani

Shauri la Kanisa la Gwajima laondolewa Mahakamani

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imeondoa shauri la awali lililofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church, maarufu kama Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima.

Maombi ya kuondoa shauri hilo yaliwasilishwa na waleta maombi kupitia kwa Wakili Peter Kibatala akiwakilishwa na Wakili Alphonce Nachipyangu, baada ya Serikali kuwasilisha barua rasmi na sahihi inayomtaja mteja wao kwa jina sahihi ambalo linatambulika kisheria.

Akizungumza mara baada ya uamuzi huo wa Mahakama Julai 14, 2025, Wakili Nachipyangu amesema:

“Hoja yetu ilikuwa ni kuondoa yale maombi ya awali ambayo tuliyaleta tangu mwanzo ili tuweze kuwasilisha upya maombi sahihi. Tulifika Mahakamani kwa mara ya kwanza kutokana na barua tuliyoiona mitandaoni, ambayo tuliona ina mapungufuhaikumtaja mteja wetu kwa usahihi na pia haikusainiwa. Hata hivyo, wakati tukiwa Mahakamani, Serikali iliwasilisha barua nyingine rasmi ambayo sasa inamtaja mteja wetu vile tunavyomtambua kisheria.” amesema Wakili Alphonce, Shauri hilo lilifunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa kanisa hilo kufuatia hatua ya Serikali ya kulifungia kanisa hilo.

Itakumbukwa kuwa Juni 2, 2025, waumini wa kanisa hilo walizuiwa kufanya ibada katika makanisa yao, baada ya vyombo vya dola kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya taasisi hiyo ya kidini.

Wakili Alphonce amesema kuwa baada ya kuondolewa kwa shauri hilo, wanatarajia kuwasilisha maombi mapya Mahakamani kwa kufuata taratibu zote stahiki. Shauri hilo lilikuwa linasikilizwa Mahakamani hapo mbele ya Jaji Juliana Masabo

​
 
downloadfile-1.jpg
 
Mawakili wanajua kula pesa wateja
Unatumiaje barua uliyooona mtandaoni kufungua mashitaka? Badala ya kuwaomba wateja wakupe barua halisi waliyopewa na msajili kwa despatch?
Wizi mtupu.Hapo wameshawachukulia pesa kibao hao waumini wa Gwajima wasiojua sheria

Hata kwa akili za kawaida tu wakili unaulizwa hiyo barua unafungulia kesi uliitoa wapi ? Unajibu mtandaoni

Wakili Kibatala Mungu anakuona ujue
 
Na kwa maana hii serikali ndio imetoa barua rasmi leo ya kulifutia kanisa la GCTC - Ufufuo na Uzima....

Swali bado liko palepale, hatua za kuzuia shughuli za kanisa kuendelea tangu tarehe 2/6/2025 na matendo ya polisi ya kunyanyasa na kupiga hovyo waumini wa kanisa hilo yalikuwa yanafanyika kwa sheria na mamlaka ipi..?

Serikali kupitia Jeshi lake la Polisi, walipaswa kwenda kwa mlengwa wa barua ile ya awali - kanisa la Glory of Church Tanzania (GCT) na siyo hapo Glory of Tanzania Church (GCTC) - Ufufuo na Uzima...

Na inashangaza zaidi barua rasmi ya kuwataarifu kuwa wamefutiwa usajili wao imepelekwa mahakamani leo tarehe 14/7/2025 badala ya kuwapelekea wahusika kwenye ofisi zao....!!

Hii ndiyo serikali ya Bi Kizimkazi Samia inavyofanya kazi zake na eti wanaomba miaka mitano mingine....

Wanafanya mambo hovyo hovyo utadhani watu wote ndani ya serikali hii ni wendawazimu ambao hawakwenda shule kabisa ya mambo ya utawala...!!

Tuwakatae na tuwatenge kwa namna zote. HAWAFAI...!!!!!!!!!
 
Mawakili wanajua kula pesa wateja
Unatumiaje barua uliyooona mtandaoni kufungua mashitaka?
Kwa sababu ndiyo hiyo inayotumiwa na serikali hiyo hiyo kupitia jeshi la polisi kusababisha athari za waumini wa kanisa la GCTC.
Badala ya kuwaomva wateja wakupe barua halisi waliyopewa na msajili kwa despatch?
Hawajawahi kupewa barua yoyote kwa njia yoyote zaidi ya hiyo ya mtandaoni.
Wizi mtupu.Hapo wameshawachukulia pesa kibao hao waumini wa Gwajima wasiojua sheria
Hakuna wizi wowote hapo. Ni utaratibu wa kawaida wa kisheria uliofuatwa na kanisa kuweka mambo sawa...

Leo ndiyo wameleta barua sahihi na insyowalenga wahusika. Hujiulizi kwanini hivyo leo..??
Hata kwa akili za kawaida tu wakili unaulizwa hiyo barua unafungulia kesi uliitoa wapi ? Unajibu mtandaoni
Kwani hao wanaotekeleza amri hiyo iliyotolewa kupitia barua hiyo wao wanatumia barua gani?

Wanatumia amri ya mahakama ipi kufanya wanayofanya?

Huoni kuwa hizo ni fujo zilizo nje ya sheria?

Polisi wamefanya kosa la tresspassing kuingilia na kufanya uharibifu kwenye mali za mtu (taasisi) pasipo kufuata sheria...!!
Wakili Kibatala Mungu anakuona ujue
Serikali imefanya kosa na itashindwa mchana kweupe kwenye kesi..

Watashika weee, mwisho wataachia wenyewe...

Mungu kweli anamuona Peter Kibatala kama mpigania haki. Na walio HAKI ni wa Mungu Jehovah..!
 
Hawajawahi kupewa barua yoyote kwa njia yoyote zaidi ya hiyo ya mtandaoni.
Acha uongo wewe afisa wa serikali na mkuu wa wilaya walienda kukabidhi barua tena kwa despatch

Gwajima na uongozi wake wakakataa kupokea hiyo barua original kwa mkono officially .utoto wakili kama sio mpenda pesa alitakiwa kuwabana kwa nini hamkupokea barua original? Kawalia pesa zao bure kwa kitu kidogo tu wangepokea ile barua original kesi ingeendelea vizuri sasa ona kitendo chao cha kukataa kupokea barua originali .Mawakili wanaanza kesi upya baada ya kulamba pesa kwa kesi hewa ya mwanzo

Msikilize mkuu wa wilaya akiongea kuhusu barua original

View: https://youtu.be/-cRt45zOdPQ?si=fgYOt6qoSnc0a10v
 
Mawakili wanajua kula pesa wateja
Unatumiaje barua uliyooona mtandaoni kufungua mashitaka? Badala ya kuwaomva wateja wakupe barua halisi waliyopewa na msajili kwa despatch?
Wizi mtupu.Hapo wameshawachukulia pesa kibao hao waumini wa Gwajima wasiojua sheria

Hata kwa akili za kawaida tu wakili unaulizwa hiyo barua unafungulia kesi uliitoa wapi ? Unajibu mtandaoni

Wakili Kibatala Mungu anakuona ujue

Wewe ndo huna akili
 
Acha uongo wewe afisa wa serikali na mkuu wa wilaya walienda kukabidhi barua tena kwa despatch
Sio ishu ya uongo hapa..

Kama walikabidhi hiyo barua kwa dispatch, nani alipokea? Wapi na wakati gani...?

Wewe hujiulizi kwanini ndo wamekabidhi barua halisi ikwa - address wahusika halisi leo tena mahakamani..??

Tumia vyema akili yako kufkiri. Acha kuwa chawa tu asiye na akili...
Gwajima na uongozi wake wakakataa kupokea hiyo barua original kwa mkono officially .
Walikataa? Halafu ukachukua hatua gani? Walipeleka hata kwa serikali ya mtaa lilipo hilo kanisa? Eeh, ikawaje..?

Kama ni hivi, wewe unadhani kwanini ndio wanaitoa barua halisi wahusika tena mahakamani? Hiyo damage waliokwisha ifanya watairekebishaje?
utoto wakili kama sio mpenda pesa alitakiwa kuwabana kwa nini hamkupokea barua original? Kawalia pesa zao bure kwa kitu kidogo tu wangepokea ile barua original kesi ingeendelea vizuri sasa ona kitendo chao cha kukataa kupokea barua originali .Mawakili wanaanza kesi upya baada ya kulamba pesa kwa kesi hewa ya mwanzo
Wakili gani ambane nani?

Nyie mliofanya uhuni huo ndio wa kubanwa kueleza hiyo barua yetu halisi iko wapi na mliipeleka wapi maana mnayoifanyia kazi na iliyoko mitandaoni tena ikiitaja taasisi nyingine ni hii?
Msikilize mkuu wa wilaya akiongea kuhusu barua original

View: https://youtu.be/-cRt45zOdPQ?si=fgYOt6qoSnc0a10v

Huyu mpumbavu huyu, mshirika wa uhuni nani amsikilize?

Anapaswa kupeleka utetezi na maelezo haya mahakamani sio kubwabwaja hovyo ndani ya ofisi yake...!!
 
siamini kama haya yanatokea Tanzania, raia kunyimwa haki ya kuabudu. hii dhambi Mungu ndiye atakuwa hakimu.
 
Hawajui watendalo hao viongozi wa Serikali. Wameamua kabisa kugombana na Mungu. Muda si mrefu majibu watakutana nayo.
 
Back
Top Bottom