Mbwa Mwitu anapoanikiwa nyama bila jasho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbwa Mwitu anapoanikiwa nyama bila jasho

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, Sep 2, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mega kipande kimbilia kando kujinafsi
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Huo ni mtego, hiyo nyama ina sumu kali sana.
   
 4. Kanyapini

  Kanyapini JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukiiwekea sumu hiyo haponi hata mmjoja.
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  By the way kuna aliyeelewa mantiki ya kuwahifadhi hawa mbwa mwitu kwa mwaka mmoja na kuwaachia huru? Inaonekana dola 450,000 zimetumika kuwahifadhi, what was the essence?
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Halafu eti tunawasifia kwa kuchezea fedha. Inaonesha ni jinsi gani tunashindwa kuweka vipaumbele. Hizo dolas zingepelekwa kwenye nyanja ambazo jamii inaweza kufaidika kirahisi ingeeleweka.
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  May be tusilaumu sana. Wako hatarini kutoweka kwa sasa. Kwenye maeneo mbalimbali ya mbuga zetu hawa mbwa mwitu hawaonekani tena baada ya kushambuliwa na magonjwa. Mpango uliwekwa wahifadhiwe na kutunzwa. May be na gharama zimekuwa kubwa sana kuwatunza maana na wabongo wanafaidkia huko huko. Ila mpango ni mzuri though wa gharama sana.
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sasa mbona wamewarudisha mbugani, hiyo hatari imeondoka?
  Wastani wa gharama ni kama dola elfu 8 kwa mbwa mwitu mmoja kwa mwezi hii na sawa na sh. mil 12 kwa mwezi. Yaani huyu mbwa mwitu mmoja anatunzwa kwa gharama kubwa kuliko mishahara ya waalimu 40!
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Mkuu ZeMarcopolo nafikiri wengi wahehifhadhiwa Mkomazi ndiko walikopelekwa baada ya tishio hilo pamoja na Rhino.
  Gharama kweli ni kubwa ila hapo tegemea pia kuchakachuliwa maana kila mmoja atatafuta ulaji aise.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kilichonishtua zaidi ni kwamba gharama hii imetolewa na VODACOM, sasa swali ni je, voda hawatumii hii kukwepa kodi!?
  Katika report waliyotoa wanasema wamewarudisha mbugani kwenye regular wild life...
   
 11. m

  markj JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  jamani! hawa si ndiyo wale mh. rais jk, aliowasifia voda kwa kuwafadhili kweye hili swala la kuwatunza mmbwa mwitu? daah! voda bana kama core value yao ya social responsibility ndo hii, mmh! basi sijui tanapa na mali asili wanafanya kitu gani kwenye hii nchi, haya waache voda wajipendekeze wakija kushtuka wote jao washasafirishwa
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  vodacom wanadhamini huo mpango wa kuhifadhi hao mbwa mwitu. So wanalishwa ili waweze kuzaliana
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280

  Mkuu hapo tegemea vyote wala usitarajie moja
  Na hizo gharama sijui zinatoka wapi maana kama ni nyama na treatment nyingine hizo cost bado ni kubwa sana.
  So kuna kuchakachua gharama halisi na mambo mengine as u know hii ni tanzania bana kila kitu kinawezekana
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Katika hilo ndugu yangu tujaribu kuwa wapana na wapembuzi. Halipo Tanzania tu, bali duniani kote na nimeshuhudia hivyo. Ukwepaji wa kodi wa aina hii una manufaa kwa taifa kukliko ule unaoingiza pesa kwenye mifuko ya watu binafsi. Njia hii ni halali kwani iko wazi na pesa zinazotolewa zinaelekezwa moja kwa moja kwenye huduma inayotambuliwa kitaifa sawa na kupeleka huduma kwa watu maskini, kusaidia watoto wenye mazingira magumu mitaani nk.

  Vodacom wako sahihi katika hili na hapo pesa walizozitoa kwa huduma hiyo hawatatozwa kodi kama lilivyo popote duniani kwa vile ni kwa ajili ya huduma za kijamii na kitaifa mambo ambayo yalitakiwa yafanywe na serikali yenyewe. Ukiwadai kodi nis awa na serikali kudaiwa kodi.
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Rocky,Tanzania hata binadamu wa kawaida na wao wanatoweka kwa kasi sana, vodacom wangeanza na hao. Binadamu wanaoshindwa ( kutokana na umaskini) kwenda shule kupata elimu ya kweli, binadamu wanaoshindwa a( kutokana na umaskini na serikali kutotoa futrsa hiyo) kupata huduma ya afya, binadamu anayeweza kuishi bila kuiba, binadamu anayeshindwa kusubiri dakika moja ili taa za barabarani ziwe kijani ili yeye apite.

  Watanzania tumshambuliwa na ufisadi, mpaka binadamu wa kawaida anatoweka,

  Vodacom wangeshughulikia hilo kwanza.
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Ngambo Ngali nakubaliana na wewe. Gharama hizo zingeelekzwa kwa huduma ambazo zinaenda kwa wananchi wa kawaida. Wananchi wanaoteswa na lindi la umaskini na kukosa huduma muhimu.
  Tatizo jingine ninaloliona na vipaumbele. Wale wanaopanga vipaumbele hawajafanya hivyo na ndo maana unaona mbwa mwitu wanaonekana bora kuliko hata binadam
  @
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Wenzenu wanatumia kisingizio cha kukwepa kodi, nyie mnalalamikia mbwa mwitu.
  kama mmoja kwa mwezi anatumia $ 8000, wenye zoo wanatengeneza tshs ngapi hadi wanamanage kwa viingilionvya buku tatu?
  Kodi wanatozwa kwenye faida. Hela yote waliyokusanya wanasema wamefanyia matumizi ya kununua madawati na kutunza mbweha, kiji-chenji kinachobaki vitabuni kinakatiwa kiji-kodi, kwisha habari yake
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Shame, big shame,

  Unachukuaje hela ndogo ambayo mkulima wa viazi gairo kaihangaikia na kumpa mbwa mwitu.

  Ninaachoweza kusema ni kuwa makampuni makubwa yaliyovimbiwa na faida ya kunyonya wanyonge, yana njia nyingi za kututukana na hii ni njia mojawapo.
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Expences on CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY are tax deductable; wakuu unapozungumzia SCIAL RESPONSIBILITY does that include the care of wild animals? Mimi nadhani hili lilikuwa ombi maalum kutoka kwa Mkweree kwenda Vodacom kuwa kwenye ile hoteli yao ya BILILA kule Serengeti ,mbwa mwitu wametoweka basi watoe fungu la kuwalea ili waongezeke na ndio maana mkuu wa Vodacom alikwenda Magogoni kutoa progress report!!
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sawa, lakini tatizo ni pale mtu anapojenga darasa moja na kusema katumia milioni 200. Je, kweli voda wametumia kiasi hicho kama corporate social responsibility au kiasi sahihi ni just a fraction of it. Najaribu kuchanganua jinsi USD 450,000 zinavyoweza kutumika kutunza mbwa mwitu 11 kwa miaka mitatu naona hesabu hazikubali.Nafananisha na darasa la milioni 200 la matofali ya kuchoma...
   
Loading...