Hematidrosis: Hali ya kutokwa jasho la damu

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,795
10,209
Hematidrosis ni hali inayojitikeza kwa nadra sana ambayo humfanya mtu atokwe na jasho la damu. Pia kitaalamu inafahamika kama hematohidrosis and hemidrosis.

Ni hali ya nadra sana kiasi kwamba watu hudhani haijawahi kutokea au haipo tu kabisa, lakini hali hii ya kutokwa na jasho la damu imeshawatokea watu mbalimbali katika historia. Biblia imemtaja Yesu kuwa alitokwa na jasho la damu alipokuwa akisali kabla ya saa za kusulibishwa.

Hali hii inaweza kutokeza kwa mtu anayepitia kiwango kikubwa sana cha mawazo (stress). Sababu nyingine zinazotajwa zaweza kusababisha hali hiyo ni kama magonjwa ya kimfumo, aina fulani za hedhi, kutokwa jasho kulichozidi kiwango cha kawaida, Matatizo ya kisaikolojia, na kadha nyingine zisizojulikana.

images (24).jpeg
 
Back
Top Bottom