Nini husababisha jasho jingi kwa watoto?

Kobe la Makobe

Senior Member
Feb 3, 2024
129
141
Salamuni ndugu zangu, niende moja kwa moja kwenye topic, ni nini husababisha baadhi ya watoto na hata wakati mwingine watu wazima kutoa jasho lisilo la kawaida?

Nina mdogo wangu watoto wake mmoja miaka minne wa kike na mwingine miaka miwili wa kiume huwa wanatokwa sana na jasho hata kipindi ambacho sio cha joto kiasi cha kutoa jasho kama hilo. Wakilala yaani sehemu walipolala huwa hadi panaloa kabisa kwa jasho.

Wana afya nzuri tu ila tatizo ni hilo jasho, wakivaa ndala lisaa tu zote zinakuwa zimeloa. Vile vile shemeji yangu nae ambae ni mama wa watoto hawa nae akivaa ndala kwa muda mrefu nae hujikuta miguu imeloa na kama anatembea kwenye vumbi basi akifika miguu inakuwa kama katembea kwenye matope

Je, hili linaweza kuwa ni tatizo gani na nini dawa yake?

Natanguliza shukrani.
 
Wanaishi mkoa gani?

Kama ni Dar es Salaam ni kawaida.

Kama ni Njombe hasa Makete hao ni wagonjwa.
 
Watoto wanakuwa active mda wote. Wanacheza sana au Jasho linatoka wakiwa hawachezi
 
Umenisemea ndg yaani mke wangu anasumbuliwa na hili jambo, anaweza kutoka bafuni hajapaka mafuta ashalowa jasho, kwenye kula ndo utamwonea huruma, na hapo yuko Arusha sa sijui siku akienda Dar
 
Back
Top Bottom