Mbunge wetu Gwajima tunaomba kujua imekuaje uhamiaji kukamata mama ntilie na machinga pale mbuyuni

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,067
709
Wakuu jana nilishudia askari wa uhamiaji wakifanya ambush kukamata wafanya biashara wadogo wadogo pale mbuyuni. Picha lilianza baada ya bus moja likiwa na watu walio valia sare za uhamiaji kufika km vile picha ya MAFIA VS NINJA likisdinidkizwa na gari ndogo. Walipofika waliwaweka chini ya ulinzi wafanyabiashara wote huku wakipewa amri ya kupanda bus huku wakiacha biashara zao sadaka kwa watu.

Ushauri kwa mama SAMIA Rais wetu mpendwa hawa ndiyo wapiga kura wako na CCM.

Tunaomba mbunge wetu Gwajima atupe maelezo ya hii kitu km ni sawa.
 
Mbuyuni ya kuelekea Tegeta kona ya kwenda salasala
Hiyo itakuwa ni MISAKO, kwani nasikia maeneo hayo kuna warundi wengi sana, wanafanya biashara zao hapo, kwa kujiita waha!!!ni Tz pekee tu ndipo unapokuta uhamiaji wanafanya kazi zao , huku raia wanawalaumu!!usiombe yakukute huko kwao utatamani hata ardhi ipasuke, kwa kutembea tu bila hati ya kusafiria , wakukamate, hata kama umeisahau tu sehemu ulipofikia!!kwa mtu anayeishi nchini bila kibali sio wa kumuonea huruma hatà kidogo.
 
Kabla hujapayuka unazijuwa uniform za Auxiliary Police?
 
Wakuu jana nilishudia askari wa uhamiaji wakifanya ambush kukamata wafanya biashara wadogo wadogo pale mbuyuni. Picha lilianza baada ya bus moja likiwa na watu walio valia sare za uhamiaji kufika km vile picha ya MAFIA VS NINJA likisdinidkizwa na gari ndogo. Walipofika waliwaweka chini ya ulinzi wafanyabiashara wote huku wakipewa amri ya kupanda bus huku wakiacha biashara zao sadaka kwa watu.

Ushauri kwa mama SAMIA Rais wetu mpendwa hawa ndiyo wapiga kura wako na CCM.

Tunaomba mbunge wetu Gwajima atupe maelezo ya hii kitu km ni sawa.
Wananchi wamenyang'anywa uhuru wa kufanya shughuli halali sio Mbuyuni pekee hata ndani ndani huko Chasimba, Chatembo, Chachui, machimbo, magereza kote wanawafagia cha ajabu kuna baadhi wametundika bendera za CCM wameachwa!!!!

Utawala uliolaaniwa na Mungu atashusha hasira ambayo viongozi wake watasaga meno
 
Back
Top Bottom