Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE SUBIRA MGALU AKIWA KATIKA ZIARA MBALIMBALI NDANI TANZANIA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mhe. Subira Mgalu ameendelea na ziara mbalimbali na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika mikoa mbalimbali nchini.

Mhe. Subira Mgalu katika kilele cha Sikukuu ya NaneNane ametembelea Vijiji vitatu katika Kata za Talawanda na Ubena ambapo Talawanda aliendelea kuunga mkono jitahada za ujenzi wa zahanati ya Kisanga na kuchangia Mifuko 30 ya Saruji ili kupandisha kozi tatu kwaajili ya kuweka paa. Zahanati hii amechangia tangu kuchimba msingi Mifuko 50 ya Sementi mwaka 2018.

Mbunge Subira Mgalu ametembelea Moja ya mradi mkubwa wa Maji Kata ya Matimila wa Bilioni 1.3 ambao umetekelezwa Mwaka 2022 ambapo kwa mara ya kwanza wanapata Maji ya bomba.

Vilevile, Mhe. Subira mgalu ameshuhudia Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere unaoendelea na mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa zaidi ya Trilioni 5 kati ya Trillion 6.5 kutoka Asilimia 36 ya utekelezaji Machi 2021 mpaka Asilimia 91 Julai 2023.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.33.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.33.jpeg
    66.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.33(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.33(1).jpeg
    54.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.34.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.34.jpeg
    51.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.36(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.36(1).jpeg
    65 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.38(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-13 at 16.36.38(1).jpeg
    57.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom