Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro inamchunguza Mbunge wa Viti MAALUM (CCM) Dk.Christine Ishengoma, kutokana na tuhuma za kugawa rushwa kwa wapiga kura huku ikiwahoji watu mbalimbali kutokana na tuhuma hizo.
Aidha TAKUKURU imewafikisha mahakamani aliyewahi kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani Kata ya Boma, Amir Nondo, na wenzake watatu kutokana na makosa ya uhujumu uchumi baada ya kudaiwa kubadili matumizi ya kiwanja eneo la Msamvu bila kufuata taratibu za mipango miji, kosa analodaiwa kufanya wakati akiwa kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, Bi Janet Machulya wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo akaonya wananchi wanaotaka nafasi za uongozi kuacha kupitapita na kugawa rushwa au watumishi wanaoaminiwa wakiwemo wenye dhamana ya usimamizi wa ardhi kuacha kufanya udanganyifu.