Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,858
7,847
Inasemekana kuwa mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Simanjiro.

Amekimbizwa hospitali katika juhudi za kupambania maisha yake.
Taarifa zaidi zitakujia baadae.
Hakuna alie salama..!!

---

Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amenusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana kuliahambulia gari lake kwa risasi mapema leo jioni hii.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo wameeleza kwamba walisikia milio ya risasi ikishambulia gari hilo kabla ya washambuliaji kutokomea kusikojulikana.

Taarifa za uhakika kutoka Simanjiro zinaeleza kwamba mbunge huyo pamoja na dereva wake wote wamenusurika baada ya gari lao kushambuliwa kwa risasi wakati wakiwa jimboni humo.




Soma pia >
Viongozi na Wanasiasa wengine waliowahi kukumbana na matukio ya kupigwa riasasi
- DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

- Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa-TISS)

- Kifo chenye utata cha Waziri Nicas Mahinda

- John Mwankenja auawa kwa risasi

- Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

- Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

- Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

- TANZIA - Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

- Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

- Maandamano ya CHADEMA: Aqulina Akwilini Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika

- Askari polisi aliyepigwa risasi na majambazi Tanga afariki
 
Mbunge wa Simanjiro Olesendeka ashambuliwa Kwa Risasi usiku huu na watu wasiojulikana. Amefutwa na gari Kwa muda na alipofika katikati ya Ng'abolok na Irkiushi, Kibaya, gari iliyokuwa ikimfuatilia ilijifanya kama inataka kupita na ghafla kuanza kumimina risasi kadhaa kuelekea mlango wa dreva.

Olesendeka na Dreva wote wako salama. Kwa Sasa wapo Kituo cha Polisi Kibaya. Taatifa pia imeshatolewa Kwa RPC -Manyara
View: https://x.com/mariastsehai/status/1773779899175584037?s=46&t=vDlGjN3mpXpeCEHCuyoPFg
 
Back
Top Bottom