Mbunge wa Kilolo ahoji ni lini Serikali itashusha gharama za vifurushi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Kilolo, Justin Nyamoga akiwa Bungeni Dodoma leo amehoji ni lini Serikali itarudia mpango wake wa awali wa kushusha vifurushi ili Watanzania wavipate kwa bei nafuu.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew, amesema changamoto ya Biashara ya Mawasiliano ipo katika kuangalia usawa kati ya watumiaji, Serikali na watoa huduma.

Ameeleza "Ni lazima tuangalie 'Production Cost' aweze kufanya Biashara katika kiwango ambacho anaweza kupata faida ili Serikali pia iendelee kupata Kodi, lakini Kodi hizo ziweze kurudi kujenga barabara na Zahanati"
 
Kwa nini hilo alilojibu ina maana hawatashusha bei ya vifurushi si ndio maana yake...?

Mbona kauli zaidi zinatofautiana na boss wapi Mh. Rais wakati alishatoa agizo kuwa bei zishushwe halafu anakinzana na kauli ya Mh. Rais...?
 
Kwa hiyo serikali imepandisha kodi ili kutukomoa wananchi kwa ajili ya kutuletea maendeleo?
... angalau sasa sababu imeeleweka ni kwanini vifurushi vilipanda exponentially! KODI, KODI, KODI.
 
Kwa majibu aliyotoa ni wazi swala la kupandisha gharama lilitoka serikalini na sio kwa makampuni ya simu, ni kawaida yao kutengeneza tatizo na kutaka kick kulitatua
 
Hajajibu swali, siasa tu,
Aseme lini bei inarudi kama kabla ya april 2021
Hivi ile kitu "amri ya rais ni sheria" ilienda na mwendazake?
 
Kwa nini hilo alilojibu ina maana hawatashusha bei ya vifurushi si ndio maana yake...?

Mbona kauli zaidi zinatofautiana na boss wapi Mh. Raise wakati alishatoa agizo kuwa bei zishushwe halafu anakinzana na kauli ya Mh. Rais...?

Hilo la kupandisha vifurushi ilikuwa ni jambo limeshapangwa na utawala wa Magufuli, na hata mama juzi alivyosema vifurushi vishuke bei au kurejea kwenye bei za awali, nilijua analeta siasa tu.

Mapato ya serikali yanazidi kushuka, hivyo serikali ikaona ipandishe huko kwenye mawasiliano ili kupata fedha. Kimsingi hakuna bei itashuka maana wananchi wanaendelea kutumia bei hizi mpya kwa maumivu makubwa, huku wakiwa kimya.
 
Hajajibu swali, siasa tu,
Aseme lini bei inarudi kama kabla ya april 2021
Hivi ile kitu "amri ya rais ni sheria" ilienda na mwendazake?

Amri ya rais ni sheria inapokuwa ni ya kukomoa wananchi.
 
Hilo la kupandisha vifurushi ilikuwa ni jambo limeshapangwa na utawala wa Magufuli, na hata mama juzi alivyosema vifurushi vishuke bei au kurejea kwenye bei za awali, nilijua analeta siasa tu. Mapato ya serikali yanazidi kushuka, hivyo serikali ikaona ipandishe huko kwenye mawasiliano ili kupata fedha. Kimsingi hakuna bei itashuka maana wananchi wanaendelea kutumia bei hizi mpya kwa maumivu makubwa, huku wakiwa kimya.

Hatari sana kiongozi ila nimeskia kuna baadhi ya makampuni wameshusha bei na kuongeza packages mkuu...!
 
Mbunge pumbavu sana huyu!

Gharama za vifurushi ni bei rahisi sana. Mtu sh. 1500 unapata gb 1 na madakika kibao wiki nzima alafu mtu bado unalalamika?

Wana kilolo wana kero nyingi sana hasa suala la barabara kule Dabaga ni kilio cha kila siku alafu yeye anakuja kuongelea ishu nyepesi ya vufurushi?

Bure kabisa
 
........Ameeleza "Ni lazima tuangalie 'Production Cost' aweze kufanya Biashara katika kiwango ambacho anaweza kupata faida ili Serikali pia iendelee kupata Kodi, lakini Kodi hizo ziweze kurudi kujenga barabara na Zahanati"

Shida ya viongozi wetu hawapo creative na wakishauriwa wanapuuza.

Hivi hakuna sehemu nyingine kodi unaweza kukusanywa kuwa relief wananchi kwenye mambo mengine?

Kuna sehemu nyingi ambazo serikali ingejioanga vzr ingepata sehemu ya ku compensate kama gharama kubwa za vifurushi na kwingineko.

Mfano;
Madalali wa nyumba ambao wanakusanya pesa ya mwezi mmoja kwa kila nyumba/ chumba wanachopangisha mpangaji, kwa nn asitozwe kodi? Wawe registered ili wawe taxed pia.
Wapo pia madalali wa viwanja na mashamba etc....
 
Mbunge pumbavu sana huyu!

Gharama za vifurushi ni bei rahisi sana. Mtu sh. 1500 unapata gb 1 na madakika kibao wiki nzima alafu mtu bado unalalamika?

Wana kilolo wana kero nyingi sana hasa suala la barabara kule Dabaga ni kilio cha kila siku alafu yeye anakuja kuongelea ishu nyepesi ya vufurushi?

Bure kabisa
Mbunge anakwenda na trending issue....atakuja kivingine baadae
 
Mbunge wa Kilolo, Justin Nyamoga akiwa Bungeni Dodoma leo amehoji ni lini Serikali itarudia mpango wake wa awali wa kushusha vifurushi ili Watanzania wavipate kwa bei nafuu.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew, amesema changamoto ya Biashara ya Mawasiliano ipo katika kuangalia usawa kati ya watumiaji, Serikali na watoa huduma.

Ameeleza "Ni lazima tuangalie 'Production Cost' aweze kufanya Biashara katika kiwango ambacho anaweza kupata faida ili Serikali pia iendelee kupata Kodi, lakini Kodi hizo ziweze kurudi kujenga barabara na Zahanati"
 
Mbunge pumbavu sana huyu!

Gharama za vifurushi ni bei rahisi sana. Mtu sh. 1500 unapata gb 1 na madakika kibao wiki nzima alafu mtu bado unalalamika?

Wana kilolo wana kero nyingi sana hasa suala la barabara kule Dabaga ni kilio cha kila siku alafu yeye anakuja kuongelea ishu nyepesi ya vufurushi?

Bure kabisa
Mtandao gani huu mkuu?
 
Back
Top Bottom