Mbunge Justin Nyamoga katika Ziara Jimbo la Kilolo Mkoa wa Iringa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
WhatsApp Image 2023-04-02 at 19.34.05.jpeg

Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Mhe. Justin Lazaro Nyamoga alifanya ziara katika jimbo lake Wilaya ya Kilolo kwa Kata za Masisiwe, Kijiji cha Masege Kata ya Ng’uruhe, na Kata ya Nyalumbu ambapo alikijita kuzungumza na wananchi wa Kilolo na kutatua changamoto.

Akiwa Kijiji cha Masege kilichopo Kata ya Ng’uruhe Mhe. Nyamoga aliambatana na Mhe. Nancy Nyalusi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa na Mhe. Pancras Kihanga Diwani wa Kata ya Ng’uruhe kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo na kufanya mkutano wa hadhara.

WhatsApp Image 2023-04-02 at 19.34.09(1).jpeg
Vituo vya Afya - Zahanati
Waliipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha Tsh. Milioni 50 za kukamilisha ujenzi wa Zahanati na kuwapangia kazi wahudumu wawili ambao sasa wanaendeleo kutoa huduma katika Zahanati. Kwa kituo cha Afya cha Ng’uruhe kupitia mfuko wa jimbo Mhe. Nyamoga alichangia Mabati 90 kwa ajili ya kusaidia upauaji wa nyumba ya daktari.

Miradi ya Maji
Mradi wa Maji wa Kijiji cha Masege unatarajiwa kuanza kutekelezwa ndani ya mwaka huu wa fedha 2022/2023 kwani tayari fedha zaidi ya Tsh. Bilioni 2 zimeshatengwa na Wizara ya Maji ili kuanza na kukamilisha mradi huo na kuondoa kabisa kero ya Maji ndani ya Kijiji hicho na maeneo ya jirani

WhatsApp Image 2023-04-02 at 19.34.09(1).jpeg
Miradi ya Elimu
Shule ya Msingi Masege imeendelea na ujenzi wa matundu 16 ya vyoo vya wanafunzi mwaka 2022 kupitia mfuko wa jimbo Wabunge walichangia mifuko 40 ya kuanza ujenzi wa vyoo na kupokea mchango wa Tsh. Milioni 1 uliotolewa na Mhe. Nancy Nyalusi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa za kusaidia umaliziaji wa ujenzi wa vyoo Shule ya Msingi Masege.

Vifaa vya TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kupitia Idara ya TEHAMA wakishirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Upendo waligawa Laptops (Kompyuta Mpakato) na Desktop (Kompyuta za mezanj) 160 kwa Shule 11 za Sekondari za Jimbo la Kilolo ambazo ni Shule ya Sekondari Mawambala; Ilula; Nyanzwa; Mtitu; Ukwega; Udekwa; Madege; Dabaga; Mlafu; Kilolo; Makwema.

WhatsApp Image 2023-04-02 at 19.34.07.jpeg
Miradi ya Barabara
Barabara ya kutoka Kijiji cha Masege kuelekea Kijiji cha Ukumbi ukarabati wake unaendelea na sasa tayari mkandarasi ameanza kuikwangua barabara hiyo kwa maeneo korofi na kuweka kifusi cha changarawe na ndani ya wiki mbili zijazo mkandarasi anayesimamiwa na TARURA anatarajiwa kukamilisha marekebisho hayo.

Aidha, Mhe. Justin Lazaro Nyamoga aliambatana na Mhe. Yohanis Mhanga Diwani wa Kata ya Nyalumbu na Ndugu Amani Mdeka Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kilolo ambapo walikutana na viongozi wa madereva Bajaji na Bodada Kata za Nyalumbu na Ilula na kufanya nao mazungumzo yenye lengo la kusikiliza kero, maoni na ushauri katika uboreshaji wa shughuli zao za usafirishaji ili waweze kufanya kazi kwenye mazingira rafiki na kuongeza vipato vyao.

WhatsApp Image 2023-04-02 at 19.34.05(1).jpeg
Mhe. Nyamoga alifika Kata ya Masisiwe ambapo waliahidi kutachangia tofali za block 1500 ili kuwezesha ujenzi wa Shule Shikizi ya Kitemela. Waliipongeza Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mbawi.

Pia, Serikali kwa mwaka huu wa fedha itatekeleza ujenzi wa mnara wa simu ili kuboresha huduma ya mawasiliano ya simu kwa vijiji vya Mbawi na Masisiwe.

#KaziIendelee
#UongoziUnaoachaAlama
#KasiZaidiKaziZaidi
#KiloloInabadilika
#KuwatumikiaWatanzania
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-02 at 19.34.02.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-02 at 19.34.02.jpeg
    47 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-04-02 at 19.34.15.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-02 at 19.34.15.jpeg
    38.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom