Mbunge wa Kilindi aipaka JamiiForums

Mbunge wa Kilindi aipaka JamiiForums

Hawa watu sijui wanachaguliwa kwa vigezo gan jaman wana JF wenzangu? wananchi 2we makin 2taizika nchi yetu na kusababisha generation yetu kuwa ya kitumwa
 
walisema wakina msekwa

Akawaja nape akapandikiza na vibaraka wake

Sembuse shelukindo?? Kwanza nilikua simjui mpaka alipoi Dis jF.

Naomba uniPM we lukindo upate ushauri wa bure,au nambie nije CHAKO NI CHAKO upate ushauri.

Kiukweli Shelukindo tumekushika pabaya.

Eti jamani Huyu si ndo baba ake alipewa kamati kipindikile?na mzee wake alikua makin sana sasa sijui kama huyu Beatrice ni wake au kapakaziwa.
 
Enzi za nyerere zilishapitwa wewe mama soma alama za nyakati saizi hata waarabu wanajitambua refer to Egypt,TUNISIA,SYRIA &now Yemen ukikosea lazima tukukosoe umekuwa mungu hadi usikosolewe ushauri mdogo jadili matatizo ya jimboni kwako na Tanzania kwa ujumla sio kuijadili jamii forums.
 
wanazidi kuipaisha JF

zinga la promo hilo ndani ya Bunge, Watanzania wasioifahamu JF watataka kuifahamu zaidi hii JF inayotukana Waheshimiwa na pia kuwachafua halafu wakishakuja hapa na kuona mwelekeo wanaona hakuna matusi wali uchafuzi wa hao wanaojiita waheshimiwa bali kusema kweli tupu kuhusu matatizo makubwa ya nchi yetu yanayosababishwa na viongozi wasanii ndani ya chama cha magamba.
 
First of all she's Ugly..

Alaf nahisi hamjamshtukia, kuna wabunge wengine hawana tofauti na wack celebrities ambao wako tayari hata kupiga picha za utupu na kuzituma kwenye magazeti ya udaku kwa kujifanya wao ni mtu wa kawaida alieziokota ilimradi tu na yeye aonekane anazungumziwa kwa siku nzima. Hicho ndicho anachofanya huyu bi-mkubwa, kila siku anaingia JF anakuta thread zote zinaongelea watu wenye akili timamu ambao wanakubali kukosolewa matokeo yake anatafuta atoke vipi ili na yeye a-make headline. Na kafanikiwa, si unaona mpaka sasa kuna comments zaidi ya mia na mwisho wa siku zitafika hata elfu moja.. tayari kashakuwa trending topic. Najua lazima atakuja kusoma hapa,

USHAURI WANGU: Mama Bite acha kushindana na historia, JF is here to stay wether u like it or not. Tutaendelea kuusema upuuzi wenu wote mnaoufanya kwa kutumia mwanvuli wa vyeo mlivyopewa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Kama wewe na Green-Yellow wenzako mnaona JF haiwatendei haki basi waambie vijana wenu wafungue site ya kuwasifia.

Ni hayo tu...

 
Hajasema kuwa Jf inatafuta umaarufu? Maana siku iz ndio defensive slogan yao.
 
Wana JF kuweni makini sana na wabunge/Viongozi, wengine hasa hawa uchwara wanatafuta publicity maana wameona hawana vigezo vya kujulikana hivyo ili wajulikane wanatumia mgongo wa JF ili tuwajadili na ndipo wanakuwa wamepata nafasi ya kujitangaza, ckuwa najua kama kuna mtu kama huyu ni mbunge maana sioni umuhimu wake pale mjengoni, Sasa kaamua kuisema JF akitambua dhahili kuwa tutamdiscuss na kwa namna moja ama nyingine kwake ni Publicity.

Nashauri hawa wengine tusiwe hata tunathubutu kutaja majina yao humu ndani, wameamua kurithi kauli za yule Makamu wao(b4 6)juu ya mtazamio wake kwa JF, Ni vizuri pia asome Vision ya JF ndipo aanze ''kuropoka'', Anambambo mengi sdana ya kuongelea na cc cyo type yake coz we are GREAT THINKERS- Nadhani pia amekoswa ufahamu wa kujua ni nini tunakuwa tunaongelea maana nina wasiwasi na ufahamu wake wa kutambua na kuchambua mambo.

Natamani cku moja JF iwe na TV/Redio ili haya yote yawe yanawafikia wapiga kura wao kule vijijini kwetu kusikokuwa na Internet ambako Babu/Bibi bado wanaamini Nyerere yupo na ''ETI'' Kiongozi mzuri ni yule anayetoa kofia na Kitenge wakati wa uchaguzi.
Ahsanteni ngoja nile mrenda wangu na michembe
 
Heri wale wenye akili zinazoweza kupimwa kuliko wenye akili zisizoweza kubebeka
 
Heri wale wenye akili zinazoweza kupimwa kuliko wenye akili zisizoweza kubebeka
 
A United Nations report released Friday declares Internet access a human right. Presented to the General Assembly, the report by UN Special Rapporteur Frank La Rue states that, "the Internet has become a key means by which individuals can exercise their right to freedom and expression."


angalia jimbo lako achana na JF.......Mama unawaona hawa watoto hapo chini? ni jmbo lako na bado picha zinakuja
attachment.php


attachment.php






na hapa umchafuliwa? tukusifie kwa lipi?

Shelukindo Wanguu si wajinga!


KAMA kuna Mbunge ambaye sina shaka atapoteza Jimbo kwa utashi wake mwenyewe si mwingine, bali ni mbunge wa Wilaya mpya ya Kilindi Beatrice Shelukindo.

Fikra Pevu leo imeamua kusema wazi moja kwa moja kutokana na kile ilichokishuhudia katika Wilaya hiyo mpya na Jimbo hilo la uchaguzi.

Kitakachomuangusha Mbunge huyo si kingine isipokuwa kutaka kwake kuwafanya wakazi wa Wilaya hiyo wengi wao wakiwa wa kabila la Wanguu, kama ni wajinga.

Kila kona unayopita ya Kilindi, kilio kikubwa cha wakazi wa huko ni kutokutimizwa kwa ahadi kadha wa kadha zilizopata kutolewa na Mbunge huyo.
Haiswii kuzitaja ahadi hizo kwa kuwa Beatrice Shelukindo mwenyewe anazifahamu, lakini pia haipendezi kuwafanya Wakilindi kuwa ni wajinga na kwamba siku zote watakuwa tayari kukubaliana na ahadi zisitotimizwa.

Hata watoto nyumbani wakidanganywa sana kupelekewa pipi na baba au mama yao, ufikia mahali wakang'amua janja hiyo na kutokukubaliana tena na ahadi zinazotolewa.

Hivi inaingia akilini kweli kwa Mbunge kusimama kwenye mkutano wa hadhara na kuwaeleza wananchi kuwa amewanunulia mabati na saruji ambayo iko njiani inakwenda, halafu mabati na saruji hiyo visifike hadi leo?

Kwani kuna umbali gani kutoka Dar es Salaam au hata Tanga hadi Kilindi, kiasi kwamba mabati na saruji yashindwe kufika hadi leo?
Huu ni ujanja, tena ujanja wa kizamani. Fikra Pevu haidhani kama ujanja wa aina hiyo unayo nafasi ya kuwashawishi wananchi wa Kilindi kuendelea kuwa na imani na Mbunge wao!

Kama hiyo haitoshi na hata baada ya kubaini kuwa ahadi zako hazina ukweli, kwanini basi usishuke chini na kuwaomba radhi Wanakilindi na badala yake kuanza kudai kuwa ahadi ulizotoa zilipokelewa na viongozi wengine ama wa kisiasa au Kiserikali Wilayani humo?

Kama madai yanayotolewa na maelezo yanayoelezwa na wananchi ni ya kweli, Fikra Pevu haina shaka kusema wazi kuwa ubunge wa Jimbo hilo umekwisha kuanza kuupoteza.

Kama mimi ningekuwa wewe, na kwa kigezo cha Kilindi kuwa Wilaya Mpya, hakika ningekuwa Mbunge kwa hadi hata vipindi vitatu.

Kwanza upya wa Wilaya ungenibeba. Pili uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuifanya Wilaya hiyo kuongozwa na wanawake, kingekuwa kigezo muhimu. Tatu, ningefanya kazi kwa ukaribu na viongozi waliopo Wilayani kuhakikisha kuwa tarafa zote nne zinafikiwa na huduma za kijamii kwa uwiano ulio sawa na nne ningeongeza ukaribu wangu na wananchi kwa kuepuka kuwahadaa.

Kumbuka, miaka ile ya kuwaongopewa wananchi haipo, kama ilikuwepo basi ni zamani. Wanguu wamefumbuka macho. Ulipaswa kuwaeleza ukweli kuwa ubunge ni uongozi tu na si hakika ya kila jambo. Huenda hapo ndipo ulipokosea, na ndipo patakapokugharimu.

Pamoja na kuanza kupoteza kwako umaarufu katika jimbo la Kilindi huku wananchi wakiinung'unikia CCM kwa chini chini kuwachagulia mtu wa tatu katika kura za maoni kuwa mbunge wao, bado unayo nafasi ya kujirudi.

Ndiyo, zipo jitihada za wanaCCM kadhaa kuwania jimbo hilo na tayari wengine wameanza kampeni za chini chini. Hilo lisikuogofye kama una nia ya dhati ya kuendelea kuongoza Jimbo la Kilindi.

Tumia muda uliopo kwa umakini mkubwa kama ukiweza, lakini huna budi kuondokana na mawazo kwamba Wanguu watanunuliwa tu kwa fedha. Kusema ukweli fedha zako watakula, na kura hawatakupa.

Kila la kheri Shelukindo katika kumalizia ngwe hii ya miaka mitano ya Ubunge, ukikumbuka kuwa Wanguu si wajinga na hawastahili kudanganywa kirahisi.

Wasalaam


*Kwa maoni tumia barua pepe: kamalamo@gmail.com au simu: 0754 468229
Mama waambie wenzako JF hatupigii watu amakofi burebure tu
 
wewe mama nenda kasomeshe wananchi wako achana na jf .you better join us ,nimefanya research ndogo tu hapa JF nikauliza nani humu ndani aanatoka kwenye jimbo lako? sijapata ...ina maana kwenye jimbo lako mtu mwenye accsess ya internet ni wewe tu . nenda kwenye jimbo lako kawasaidie wananchi wako wanalogana tu hospital hazina madawa na shule hazina waalimu.
 
Kwa hiyo na wewe umeacha shughuli zako zote umekaa kuangalia bunge ili upate UMBEYA wa kuleta JF, usiwe MBEYA fanya kazi ulijenge taifa...!!!

Na ndiyo kusema umekuja kumshitaki Beatrice Sherukindo humu JF....??? umbeya mtupuuu...

Yaani ukianza kutest polepole uwezi subiri kutokea kwa coloured ppt, hapa tu nikajua kumbe Shangiguku = Shangingi THAT IS WHY UMEKIMBILIA KWENYE uMBEA WEWE aUNT NANI VILE.
 
Namfahamu mama huyu tukimuita mama Matumbo. Akiwa mtu wa kuvaa mini na mapaja nje nje!
Badaye akahangaika na viti maalumu akakwama. alalama kila kona kwamba wanagawa vyeo kwa upendeleo wa dada na wake zao.

Hatimaye akaingia mjengoni. kaonyesha ushujaa wa kutetea wanyonge. Kumbe kichwa kitupu. Kila siku an topic mpya anayodhani itapata makofi ya wenzake!
 
wewe mama nenda kasomeshe wananchi wako achana na jf .you better join us ,nimefanya research ndogo tu hapa JF nikauliza nani humu ndani aanatoka kwenye jimbo lako? sijapata ...ina maana kwenye jimbo lako mtu mwenye accsess ya internet ni wewe tu . nenda kwenye jimbo lako kawasaidie wananchi wako wanalogana tu hospital hazina madawa na shule hazina waalimu.

Na hospitali yao ya wilaya imefungwa kwa kukosa vigezo.
 
Kwa kasi hii sijui kama tutafika !!!!! Kweli muda kidogo wa kuchangia wanaoupata hapo mjengoni wanamalizia kuisema vibaya JF !!!! Tuna safari ndefu!!!
 
Back
Top Bottom