Mbunge wa Kilindi aipaka JamiiForums

BEATRICE SHELLUKINDO (CCM): MBUNGE WA KILINDI

BEATRICE+MATUMBO+SHELLUKINDO.jpg
BEATRICE SHELLUKINDO (CCM): MBUNGE WA KILINDI 2010

Mtu mwenyewe huyo hapo. Asiwaumize kichwa.
Nitawaletea kashfa zake mkizihitaji.


Lying


In most countries people lie for two reasons:

1) to prevent being accused of any wrong doing;
2) to gain something.

Not in Tanzania. Lying is a way of live, a means of communication. People lie about everything. Most of the time you wonder why they were lying in the first place because they did not gain anything out of it, on the contrary they just made other people being angry at them.

The most reasonable explanation seems to be that they say what they think you want to hear. People like to hear nice stories and expect you to tell them nice things, they do not want to hear that you refuse to do something or any other message they do not want to receive. In addition, telling people what they want to hear prevents you from entering into a conflict.
 
Mwache aendelee kupiga kelele,tutaelishana na kupeana taarifa vyovyote vile iwezekanavyo.
 
Kama wanafanya makosa yanayopelekea ugumu wa maisha kwa kila mtanzania wanaedai wanamuongoza na kumthamini tuwapigie makofi?Wanataka kola kitu ndio mzee ktk zama hizi!?
 
Mh, Shelukindo umetumwa kushambulia wapinzani kwa kusema wanakataa posho kwa kuwa hawafanyi kinachotakiwa lakini kama wangefanya kinachotokiwa wange dai posho na sikukataa posho kwani yeye wananchi wakilindi wanajua nini maana ya posho yake.

Lakini wakati akisema hayo ameishutumu JF eti inatumika kuwahadaa wananchi na kuchafuana. Eti kuna wapinzani wanaitumia JF kuchafuana.

Akuishia hapo eti wanaokataa posho wana wafadhili ndiyo maana wanakataa posho, hao wanaenda kuishitaki serikali kwa wafadhili ili wakate misaada kwa kisingizio cha kutokuwa na utawala bora.

Moja kwa moja kailenga CHADEMA Nakujaribu kuwasafisha walioanzisha CCJ, namwambia Mh Shelukindo kwa Jamii Forums haitumiwi kama anavyohisi Jamii Forums Inafikria nakuona msitakabari wanchi na kwakuwa nisehemu unayoweza kusema kwa uwazi bila woga ndiyo maana unaona JF nimwiba kwako.

Karibu JF

shelukindo yupi?

yule mama?

hahaha, anaogopa yasimkute ya mumewe tu huyo hana lolote.

mwambieni achangie JF...mkono mtupu haulambwi.
 
Mgombea ubunge CCM afikishwa Mahakamani

BY SONYO MWENKALE
20th September 2010

Kisa? Vidonda kura za maoni

Mgombea ubunge wa jimbo la Kilindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Beatrice Shellukindo na viongozi watatu wa chama hicho, wamefunguliwa mashitaka katika Mahakama Kuu mkoani Tanga.

Wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuvuruga uchaguzi wa kura za maoni, kwa ‘kuchakachua' matokeo yaliyompa ushindi dhidi ya waliokuwa washindani wake.

Shellukindo aliithibitisha NIPASHE kwa njia ya simu jana, kuhusu kupewa taarifa ya kuitwa mahakamani kwa shauri hilo.

Aliwataja viongozi wa CCM wilaya ya Kilindi walioshitakiwa pamoja naye na nyadhifa zao kwenye mabano kuwa ni Aluu Segamba (Katibu) na Mussa Mbota (Katibu Mwenezi).

Pia alisema Katibu wa Umoja wa Vijana aliyemtaja kwa jina moja la Mkoba na mpiga kura wake, Haji Abdallah ni miongoni mwa washitakiwa hao.

Shellukindo alisema kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanatakiwa kufika mahakamani hapo Alhamisi wiki hii.

Hata hivyo alielezea kusikitikishwa na hatua hiyo kwa madai kuwa sheria na kanuni za CCM haziruhusu mambo ya ndani ya chama kufikishwa mahakamani.

"Unapomshitaki mgombea wa CCM unakishitaki chama ambacho Mwenyekiti wake ni Rais," alisema.

Mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM jimboni humo, uliwahusisha wagombea saba ambapo Shellukindo ambaye ni mke wa Mbunge wa Bumbuli aliyemaliza muda wake, William Shellukindo, aliibuka mshindi.

Miongoni mwa waliokuwa wagombea katika kura za maoni ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda na aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 10, Juma Kidunda.

Wengine ni Abdallah Magawa, Rashid Majeni, Mohammed Zambo, Athuman Lusewa na Kimweri.

Naye Katibu Mwenezi wa CCM wilayani humo, Mussa Mbota, alisema viongozi hao wamepewa barua za kuitwa mahakamani Septemba 23, mwaka huu jijini Tanga ili kujibu tuhuma hizo.

Alisema kesi imefunguliwa na mmoja wa wanachama wa CCM wilayani humo, anayetajwa kwa jina moja la Kikoti.

Alisema Kikoti anadai kuwa viongozi hao walihujumu uchaguzi wa kura za maoni, kwa kuuiba kura za wagombea wengine na kuziweka kwa Shellukindo.

"Hizo habari ni za kweli, tumeshitakiwa na mwanachama mmoja ambaye hata hivyo tunamshangaa kwa vile imebainika kuwa ni mkazi wa Gairo mkoani Morogoro, anaitwa Kikoti," alisema.

Alisema: "Madai yake ni kwamba tumevuruga uchaguzi katika mchakato wa kura za maoni, tumeiba kura za wagombea wengine tukampa Beatrice Shellukindo ndiyo maana alishinda, wakati si kweli."

Mbota alisema shauri hilo lilipaswa kuwasilishwa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) badala ya mahakamani kama alivyofanya Kikoti.

"Nec ni mamlaka iliyompitisha Shellukindo sasa Kikoti alistahili kuwasilisha madai yake huko," alisema.

Pia Mbota alisema Kikoti akiwa mwanachama wa CCM, alipaswa kuliwasilisha shauri hilo katika vikao halali vya chama ili yajadiliwe badala ya kuyakimbiza mahakamani.

Viongozi hao ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Tanga, Musa Shekimweli, Katibu Mwenezi wa wilaya hiyo, Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), na mwanachama mmoja ambaye hakufapatikana jina lake na kufanya idadi yao kufikia watano.

Katika hatua nyingine, Mbota alisema kuwa wiki iliyopita gari la Shellukindo, ilipata ajali baada ya kugongana uso kwa uso na gari la Halmashauri ya wilaya ya Kilindi.

Alisema watu kadhaa walijeruhiwa katika ajali hiyo ambayo ilipotokea, Shellukindo alikuwa ndani yake.

"Mheshimiwa Shellukindo karudi jana kutoka nje ya nchi, alikwenda kuchunguza afya yake kwa kuwa alipata ajali ya gari," alisema.
Kwa mujibu wa Mbota, ajali hiyo ilitokea wakati wa siku mbili za mapumziko ya kampeni ili kupisha mitihani ya darasa la saba kufanyika.

SOURCE: NIPASHE
 
I thnk anahitaji kudeclare grudges alizonazo dhidi ya JF, hata hivyo hataweza kuzuia flow ya updates tunazopeana hapa kwani zipo valid and powerful! je anafahamu kuwa wa2 wa kilindi kwa kiasi kikubwa hawajui jf inavyofanya kazi yake au ni kitu gani, anyway anajistukia khs discussions zetu!
JF FOREVER.
 
Namchafua sasa hivi...........

Shelukindo Wanguu si wajinga!


KAMA kuna Mbunge ambaye sina shaka atapoteza Jimbo kwa utashi wake mwenyewe si mwingine, bali ni mbunge wa Wilaya mpya ya Kilindi Beatrice Shelukindo.

Fikra Pevu leo imeamua kusema wazi moja kwa moja kutokana na kile ilichokishuhudia katika Wilaya hiyo mpya na Jimbo hilo la uchaguzi.

Kitakachomuangusha Mbunge huyo si kingine isipokuwa kutaka kwake kuwafanya wakazi wa Wilaya hiyo wengi wao wakiwa wa kabila la Wanguu, kama ni wajinga.

Kila kona unayopita ya Kilindi, kilio kikubwa cha wakazi wa huko ni kutokutimizwa kwa ahadi kadha wa kadha zilizopata kutolewa na Mbunge huyo.
Haiswii kuzitaja ahadi hizo kwa kuwa Beatrice Shelukindo mwenyewe anazifahamu, lakini pia haipendezi kuwafanya Wakilindi kuwa ni wajinga na kwamba siku zote watakuwa tayari kukubaliana na ahadi zisitotimizwa.

Hata watoto nyumbani wakidanganywa sana kupelekewa pipi na baba au mama yao, ufikia mahali wakang’amua janja hiyo na kutokukubaliana tena na ahadi zinazotolewa.

Hivi inaingia akilini kweli kwa Mbunge kusimama kwenye mkutano wa hadhara na kuwaeleza wananchi kuwa amewanunulia mabati na saruji ambayo iko njiani inakwenda, halafu mabati na saruji hiyo visifike hadi leo?

Kwani kuna umbali gani kutoka Dar es Salaam au hata Tanga hadi Kilindi, kiasi kwamba mabati na saruji yashindwe kufika hadi leo?
Huu ni ujanja, tena ujanja wa kizamani. Fikra Pevu haidhani kama ujanja wa aina hiyo unayo nafasi ya kuwashawishi wananchi wa Kilindi kuendelea kuwa na imani na Mbunge wao!

Kama hiyo haitoshi na hata baada ya kubaini kuwa ahadi zako hazina ukweli, kwanini basi usishuke chini na kuwaomba radhi Wanakilindi na badala yake kuanza kudai kuwa ahadi ulizotoa zilipokelewa na viongozi wengine ama wa kisiasa au Kiserikali Wilayani humo?

Kama madai yanayotolewa na maelezo yanayoelezwa na wananchi ni ya kweli, Fikra Pevu haina shaka kusema wazi kuwa ubunge wa Jimbo hilo umekwisha kuanza kuupoteza.

Kama mimi ningekuwa wewe, na kwa kigezo cha Kilindi kuwa Wilaya Mpya, hakika ningekuwa Mbunge kwa hadi hata vipindi vitatu.

Kwanza upya wa Wilaya ungenibeba. Pili uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuifanya Wilaya hiyo kuongozwa na wanawake, kingekuwa kigezo muhimu. Tatu, ningefanya kazi kwa ukaribu na viongozi waliopo Wilayani kuhakikisha kuwa tarafa zote nne zinafikiwa na huduma za kijamii kwa uwiano ulio sawa na nne ningeongeza ukaribu wangu na wananchi kwa kuepuka kuwahadaa.

Kumbuka, miaka ile ya kuwaongopewa wananchi haipo, kama ilikuwepo basi ni zamani. Wanguu wamefumbuka macho. Ulipaswa kuwaeleza ukweli kuwa ubunge ni uongozi tu na si hakika ya kila jambo. Huenda hapo ndipo ulipokosea, na ndipo patakapokugharimu.

Pamoja na kuanza kupoteza kwako umaarufu katika jimbo la Kilindi huku wananchi wakiinung’unikia CCM kwa chini chini kuwachagulia mtu wa tatu katika kura za maoni kuwa mbunge wao, bado unayo nafasi ya kujirudi.

Ndiyo, zipo jitihada za wanaCCM kadhaa kuwania jimbo hilo na tayari wengine wameanza kampeni za chini chini. Hilo lisikuogofye kama una nia ya dhati ya kuendelea kuongoza Jimbo la Kilindi.

Tumia muda uliopo kwa umakini mkubwa kama ukiweza, lakini huna budi kuondokana na mawazo kwamba Wanguu watanunuliwa tu kwa fedha. Kusema ukweli fedha zako watakula, na kura hawatakupa.

Kila la kheri Shelukindo katika kumalizia ngwe hii ya miaka mitano ya Ubunge, ukikumbuka kuwa Wanguu si wajinga na hawastahili kudanganywa kirahisi.

Wasalaam


*Kwa maoni tumia barua pepe: kamalamo@gmail.com au simu: 0754 468229
 
Naangalia bunge muda huu JF imesemwa kuwa inawachafua wabunge,kauli hiyo imesewa na Beatrice Shellukindo!Kulikoni?


Kwa hiyo na wewe umeacha shughuli zako zote umekaa kuangalia bunge ili upate UMBEYA wa kuleta JF, usiwe MBEYA fanya kazi ulijenge taifa...!!!

Na ndiyo kusema umekuja kumshitaki Beatrice Sherukindo humu JF....??? umbeya mtupuuu...
 
Kakosa hoja ya kuongea,angekuwa specific,kachafuliwa nani au anapiga debe ili aandikwe sana hapa JF ili ajipayushe
 
JF haipo kulamba miguu yao bali ipo kutetea taifa la watanzania kwa maslai ya Taifa sio Chama. Kama ana ishu na macreat-thinker alete hoja yake au zake hapa. Halafu hili bunge letu limeshuka hadhi kwa ajili ya watu kama hao wasiokuwa na hoja, hasa wa Magamba wanashangilia hata ujinga utafikiri wapo kwenye uwanja.
 
Huyu Shelukindo si ndio yule aliyemshukuru Lowassa kwa kumsaidia sanaaaaaaaaaaaaaa!!! kupata ubunge? Kampeni za 2015 zimeanza nini na JF inaonekana ni kikwazo?
 
Mgombea ubunge CCM afikishwa Mahakamani

Mgombea ubunge wa jimbo la Kilindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Beatrice Shellukindo na viongozi watatu wa chama hicho, wamefunguliwa mashitaka katika Mahakama Kuu mkoani Tanga.

Wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuvuruga uchaguzi wa kura za maoni, kwa ‘kuchakachua' matokeo yaliyompa ushindi dhidi ya waliokuwa washindani wake.

Shellukindo aliithibitisha NIPASHE kwa njia ya simu jana, kuhusu kupewa taarifa ya kuitwa mahakamani kwa shauri hilo.

Aliwataja viongozi wa CCM wilaya ya Kilindi walioshitakiwa pamoja naye na nyadhifa zao kwenye mabano kuwa ni Aluu Segamba (Katibu) na Mussa Mbota (Katibu Mwenezi).

SOURCE: NIPASHE
[/LEFT]
kumbe mchafu huyu mama
 
Na wanakasumba ya kuwa wao wanaimmune kwasababu ni wabunge.

No no lazima waambiwe ukweli ili wajirekebishe !

Ukweli kwa wabunge wa CCM na wanachama wao ni matusi hawapendi kusikia ukweli wanapenda kusifiwa na kuambiwa uongo mwingi
 
Back
Top Bottom