Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Ndugulile aipongeza TFF kwa kujenga Kituo cha Maendeleo ya mpira wa miguu Kigamboni

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
DKT NDUGULILE AWAPONGEZA TFF KWA KUJENGA KITUO CHA MAENDELEO YA MPIRA WA MIGUU KIGAMBONI

Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile (Mb) amekipongeza Chama Cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kujenga kijiji cha maendeleo ya mchezo mpira wa miguu katika Kata ya Kisarawe II, Wilaya ya Kigamboni.

Dkt Ndugulile aliyasema hayo baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa kituo hicho hivi karibuni.

Katika awamu ya kwanza, TFF wanajenga viwanja viwili, kimoja nyasi na kingine cha nyasi bandia. Pia, wanajenga ofisi ya utawala, madarasa pamoja na hosteli. Mradi unatarajia kukamilika mapema mwakani. Awamu ya pili, itahusisha ujenzi wa viwanja vingine viwili (nyasi na nyasi bandia), hosteli nyingine sita pamoja na hoteli ya nyota tano.

Dkt Ndugulile amewashukuru sana TFF kwa kuichagua Kigamboni kama sehemu ya kufanya uwekezaji huu katika sekta ya michezo. Mradi kama huu unafanyika pia katika mkoa wa Tanga.

Mwisho, Dkt Ndugulile ametoa rai kwa vyama na klabu za michezo mbalimbali kuwekeza Kigamboni.

IMG-20211211-WA0003.jpg


IMG-20211211-WA0004.jpg


IMG-20211211-WA0005.jpg


IMG-20211211-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom