Mbunge wa Bunda (CHADEMA), Ester Bulaya ang'ang'aniwa Polisi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,258
2,000
bulaya1.jpg

MBUNGE wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (CHADEMA) ameshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Central) kwa madai amebakishwa kwa ajili ya upelelezi.

Bulaya aliripoti leo kituoni hapo baada ya kutakiwa kufanya hivyo, akiongozana na Viongozi wengine wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe ikiwa ni moja ya sharti la dhamana yao katika kesi inayowakabiri.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Vincent Mashinji amesema kuwa baada ya kuripoti kituoni hapo viongozi wote waliruhusiwa kuondoka lakini Bulaya alitakiwa kubaki kwa sababu ya upelelezi.

“Mbunge Bulaya amebaki mahabusu kwa sababu za kiupelelezi lakini tumeambiwa ataunganishwa katika shauri letu lililokuwa mahakamani Kisutu,” amesema Mashinji.

Hata hivyo ameeleza kuwa upelelezi utakapokamilika Bulaya atafikishwa mahakamani na kuunganishwa katika shauri la viongozi wengine ambao walishafikishwa mahakamani.

Kuripoti kwa viongozi hao ni moja ya sharti la dhamana katika kesi yao namba 112/2018 katika mahakama ya Kisutu Dar es Salaam.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
9,629
2,000
View attachment 743431

Wanahakikisha hawafanyi kazi za ubunge, raha kuwaweka ndani usiku tutagonganisha gilasi.
 
kilambalambila

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
8,927
2,000
Mahabusu ni ishu ndogo sana kwa Bulaya kamanda! Hata akikaa mwezi makamanda wa jf tunakuunga mkono nyuma ya keyboard
 
Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,302
2,000
Anataka tumsaidiaje sasa
Wa kusaidiwa hapo hao polisi ambao kwa makusudi wanataka alale ndani hadi Jumatatu. Polisi wanatutia aibu Watanzania tunaojielewa, ingawa mazuzu wanawajaza upepo na kuwashangilia kwa ujinga wanaoufanya.

Vv
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom