Mbunge wa Ngorongoro bado anashikiliwa na Polisi. Anahojiwa kuhusu Waandishi wa habari kupigwa

kisulisuli

Member
Oct 20, 2019
37
71
Habari kutoka Ngorongoro ni kwamba Mbunge wa Jimbo hilo, Emanuel Ole Shangai amechukuliwa na wasiojulikana.

Habari ni kwamba amepakiwa kwenye gari jeusi na kutokomea naye kusiko julikana. Vyanzo vya habari zinasema alikuwa akitokea mjini arusha alivyofika karibia na mji wa karatu eneo la rhotia ilikuja gari nyeusi iliyo waovateki ikaenda mbele ikawablock wakamshusha wakampakiza kwenye gari yao wakaondoka naye.hadi sasa hajulikani alipo

=====

Mbunge wa Ngorongoro bado ashikiliwa na polisi

Arusha. Mbunge wa jimbo la Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangay anashikiliwa na Jeshi la Polisi kuanzia jana Agosti 21, 2023 kutokana na tuhuma za kuhusishwa kupanga tukio la kushambuliwa waandishi wa habari.

Shangay alijisalimisha polisi baada ya kupokea wito wa kufika polisi ofisi ya Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Arusha (RCO) na baadae alitakiwa kuripoti kituo cha Polisi Karatu.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ngorongoro, Lucas Ole Seina amethibitisha leo Agosti 22, 2023 kwamba ni kweli mbunge huyo alikamatwa alipokwenda kuripoti polisi ili kuhojiwa kwa sababu kuna shida ilitokea mnadani wa Eblini kwa waandishi wa habari kupigwa.

“Baada ya kuhojiwa, ndugu na jamaa waliambiwa waende kesho asubuhi (leo) kwa ajili ya kuwekewa dhamana lakini walipofika asubuhi, hakuweza kujulikana mahali alipo. Kwa hiyo hatujui kama yupo kituoni Karatu au Arusha, kwa hiyo bado tunafuatilia kujua yuko wapi,” amesema Seina.

Hata hivyo, jitihada za Mwananchi kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo kuzungumzia kushikiliwa kwa mbunge huyu hazikuzaa matunda.

Hata hivyo, diwani wa CCM kata ya Elelai, James Moringe amedai wakati wakiwa njiani na mbunge huyo kukaribia Karatu katika eneo la Rhotia walisimamishwa na Polisi ambao walimchukuwa mbunge huyo kwenye gari lao.

Wakili Joseph Ole Shangay ambaye alikuwa ameambatana na mbunge huyo amedai baada ya mbunge kufikishwa polisi alielezwa anashikiliwa kwa tuhuma za kujeruhi watu wawili.

"Baada ya hapo aliendelea na mahojiano hadi saa tatu usiku na baadae polisi walisema leo wangetoka dhamana lakini hadi Sasa (leo mchana) hajapewa dhamana na hajulikani alipo,” amedai.

Wakili mwingine wa mbunge huyo, Jonas Masyaya amedai mbunge huyo alikuwa anashikiliwa na Polisi na amesafirishwa Jana usiku kupelekwa Arusha.

"Hivi sasa Mbunge amepelekwa Arusha kituo cha Chekeleni,” amedai.

Hata hivyo, Wakili anayemtetea mbunge huyo, Simon Mwambo kupitia Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) amesema kuwa walipata taarifa ya mbunge huyo kufikishwa kituo cha Chekeleni Arusha.

"Hadi muda huu bado hatujuwi alipo mbunge na tunamsubiri RCO afike kwani anahudhuria kikao".

Pia soma:
-
Mbunge wa Ngorongoro (CCM): Maisha yangu yapo hatarini
 
Habari kutoka Ngorongoro ni kwamba Mbunge wa Jimbo hilo, Emanuel Ole Shangai amechukuliwa na wasiojulikana.

Habari ni kwamba amepakiwa kwenye gari jeusi na kutokomea naye kusiko julikana

Pia soma: Mbunge wa Ngorongoro (CCM): Maisha yangu yapo hatarini
Mlimsingizia sana JPM kumbe kuna watu ama wana vyeo vinavyojulikana au kutojulikana ndio wenye nguvu ya kuamuru wasiojulikana watekeleze unyama wao kinyume na sheria. Ndio maana juzi wamepitisha sheria ya kinga ya kutoshitakiwa kwa matendo wanayofanya kwa kisingizio cha kukabili ugaidi au (uhaini)
 
Mlimsingizia sana JPM kumbe kuna watu ama wana vyeo vinavyojulikana au kutojulikana ndio wenye nguvu ya kuamuru wasiojulikana watekeleze unyama wao kinyume na sheria. Ndio maana juzi wamepitisha sheria ya kinga ya kutoshitakiwa kwa matendo wanayofanya kwa kisingizio cha kukabili ugaidi au (uhaini)
CCM ndiyo utamaduni wao na Magufuri alikuwa mmojawapo.
 
Kwann mambo haya ya kiwendawazimu?? mbona kuongoza Nchi sio kugumu kama baadh ya viongoz wanataka ionekane ni ngumu!!
 
1692629605867.png
 
Back
Top Bottom