Mbunge Stella Ikupa: Hatua gani zimechukuliwa kwa Halmashauri zisizonunua mafuta ya watu wenye Ualbino

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Mbunge Stella Ikupa: Hatua Gani Zimechukuliwa kwa Halmashauri Zisizonunua Mafuta ya Watu Wenye Ualbino.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Festo Dugange amesema hadi sasa ni halmashauri 41 pekee nchini zilizotenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa mafuta kwaajili ya watu wenye Ualbino, hivyo Serikali itaweka kipaumbele zaidi kwa mwaka wa fedha ujao kuhakikisha fedha hizo zinaendelea kutengwa.

Alikuwa akijibu swali Bungeni jijini Dodoma la Mbunge Stella Ikupa aliyetaka kufahamu ni hatua gani zimechukuliwa kwa halmashauri zisizonunua mafuta ya watu wenye Ualbino.

Naibu Waziri Dugange amesema Serikali inaendelea kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika uwekezaji wa mazao mbalimbali ambayo yatazalisha mafuta hayo.

Aidha, amesema changamoto iliyokuwepo hivi sasa ni baadhi ya maeneo kushindwa kukamilisha tathmini na utambuzi wa watu wenye Ualbino kwenye maeneo hayo ili kuwezesha utengaji wa fedha za kununua mafuta hayo.
 

Attachments

  • ikuQASZXSC.jpg
    ikuQASZXSC.jpg
    207.8 KB · Views: 1
  • mbunge-pic-data.jpg
    mbunge-pic-data.jpg
    210 KB · Views: 1
Back
Top Bottom