Mbunge Stella Ikupa Alex Aitaka Serikali Kusimamia Kanuni ya Kupata Mikopo kwa Watu Wenye Ulemavu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE STELLA IKUPA AITAKA SERIKALI KUSIMAMIA KANUNI YA KUPATA MIKOPO KWA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Stella Ikupa Alex Bungeni jijini Dodoma ameishauri Serikali kuhakikisha Halmashauri na Manispaa zinasimamia muongozo na kanuni ya kutoa mikopo kwa watu wenye ulemavu mmoja mmoja

"Je, kuna muongozo unaruhusu watu wenye ulemavu mmoja mmoja kukopeshwa fedha za Halmashauri" - Mhe. Stella Ikupa, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam

"Serikali inatambua umuhimu wa mtu mwenye ulemavu mmoja mmoja kuweza kupata mkopo ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza mchango wake katika maendeleo ya Taifa. Mwaka 2021 Serikali ilitoa muongozo wa kumuwezesha mtu mmoja mmoja kukopa kwa kufanya maboresho ya kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Walemavu za mwaka 2019 za Sheria ya fedha za Serikali za Mitaa ambapo maboresho hayo yalihusisha kuongeza kifungu kipya cha 6(a)(i)(a) ambacho kwa sasa kinatoa fursa kwa mtu mmoja mmoja mwenye ulemavu kukopa kutoka katika mikopo inayotolewa na Halmashauri. Naomba kutoa wito kwa waheshimiwa wabunge kuendelea kutoa elimu juu ya uwepo wa fursa hii kwa watu wenye ulemavu nchini kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kujiongezea kipato" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI

"Serikali imetoa wito kuwa wabunge watoe Elimu. Mimi kama Mbunge wa kundi hili nimetoa Elimu sana na kundi hili limekuwa likiitikia lakini Halmashauri na Manispaa huwa hazitekelezi muongozo. Nini Kauli ya Serikali kwa Halmashauri na Manispaa zetu nchini?" - Mhe. Stella Ikupa Alex, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam

"Ninatambua kwamba huenda kukawa kuna mabadiriko ya jinsi ya utolewaji wa mikopo, niendelee kuiomba Serikali kwa kundi la watu wenye ulemavu liendelee kufikiriwa kukopesheka mtu mmoja mmoja" - Mhe. Stella Ikupa Alex, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam

"Nawaelekeza Wakurugenzi wote wa Halmashauri nchini kuhakikisha wanatekeleza mabadiriko ya Sheria kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata mkopo kwa mtu mmoja mmoja. Katika mapitio mapya kwa Maelekezo ya Rais tutaweka kipaumbele kwenye kundi la Walemavu" - Mhe. Deo Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI
 

Attachments

  • walemavu-piclop.jpg
    walemavu-piclop.jpg
    155 KB · Views: 1
Back
Top Bottom